Dhuluma za wauza machungwa

Dhuluma za wauza machungwa

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Habari za asubuhi,

Ni kitambo sijafanya mambo humu jukwaani, mwenzenu nilikula block na nimejifunza 😎😎😎. Kuna ubadilifu mkubwa sana unafanywa na wauza machungwa, either kwa makusudi au kutokana na ujinga wa mambo ya uwiano. Hili jambo lapaswa kujadiliwa kwani madhara yake ni makubwa mno, kama wateja kukosa vitamini muhimu kutoka kwa machungwa, na pia kukosa kiburudisho, mchuzi wa chungwa. Sasa fuatilieni vipengele vinavyofuatia kujua zaidi juu ya uchunguzi, hatua zinazopaswa kuchukuliwa na mapendekezo ya ndugu mleta mada.

Okay, hii mada inatokana na mazao ya udadisi uliofanywa na mleta mada ndani ya miezi miwili, kati ya Mei na July. Wauza machungwa kuanzia kivukoni hadi tegeta walichunguzwa pasipo wao kujua. Mchunguzi alifika kwenye genge lengwa na kuagiza chungwa moja na kuomba akatiwe ili alile hapo hapo. Muuza 🍊 aliangaliwa kwa makini jinsi anavyokata chungwa, je anakata nusu kwa nusu, anakata robo kwa robo tatu, anakata theluthi kwa mbili ya tatu. Baada ya kukabithiwa vipande mchunguzi alikula chungwa kisha kulipa. Wakati wa kutupa makapi kwenye kapu mchunguzi alichunguza kwa makini makapi yaliyotangulia uwiano wa vipande.

Katika wauza machungwa 20 waliochunguzwa iligundulika wauzaji 13 walikata machungwa vipande visivyo na uwiano wa nusu kwa nusu. Katika hawa 13, wawili walionyesha kutokujua uwiano, hii inatokana na kapu la makapi yao kuonyesha vipande vyenye kila aina ya uwiano hadi moja ya nane kwa tano ya nane vilionekana. Hivi vipande visivyo na uwiano mbali na kuwanyima wateja vitamini na mchuzi husababisha ulaji wa chungwa kuwa mgumu KWELIKWELI yaani inakuwa ngumu kunyonya mpaka chini kipande ambacho ni zaidi ya nusu.

Hivyo, kutokana na kadhia tajwa mambo yafuatayo yapaswa kufanywa.

Mosi, kutoa elimu kwa vitendo kwa wauza machungwa wote jijini jinsi ya kukata nusu ya chungwa na umuhimu wa kukata nusu kwa nusu, hili swala wizara ya elimu na wizara ya afya zapaswa kushirikiana.

Mbili, mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam awe anafanya ziara za kushtukiza kuona kama kweli nusu kwa nusu yatekelezwa( atajichukulia ujiko sana hili na nitamsifia kwa kazi nzuri anayofanya).

Tatu, wateja wala machungwa yapaswa kutembea na kisu chako ili ukate mwenyewe nusu kwa nusu, la sivyo utaingizwa mjini ununue chungwa ushindwe kufyonza mchuzi wote.

Pia mwandishi anapendekeza uchunguzi zaidi ufanyike juu ya ukubwa au umbo la chungwa na jinsi mchuzi wake waweza fyonzwa kirahisi na mlaji. Kwani kuna wasiwasi chungwa likiwa na kipenyo kikubwa inakuwa ngumu kufika chini hata kama limekatwa vipande nusu kwa nusu.

Kuleni machungwa, kuleni sana.
 
Mtanyooka tuu
tapatalk_1595659759521.jpeg
 
Najuuta kupoteza muda kusoma ujinga huu. Ulistahili ban. Na hapa pia mods wakichunguza vzr ukakutwa unahamasisha watu watembee na visu,wikt serkali inazuia hata wauza vsu wasiuze kihorela,amejipandia baskel anauza mapanga au visu Ni kosa kubwa.

Hakika ban nyingine inakuhusu.
 
unaweza pia kubenua chungwa nje ndani na kula pulp lote, unaacha ganda na mbegu. Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom