Diamond aachia wimbo mpya "Acha nikae kimya"

Diamond aachia wimbo mpya "Acha nikae kimya"

Ni jambo la kushangaza wasanii wenzako wanatekwa halafu unasema ukae kimya!!!! Huyu ni mnafiki sana, kufoji vyeti, clouds kuvamiwa, Nay kukamatwa hauoni ni tatizo kwa hiyo umetumia fursa kutafuta pesa kwa kutunga wimbo unauza mia 300/- dahh!!!!! Kweli dai ni kiboko,
Jiunge na wenzako @ #AkinaRomaWakoWapi# paza sauti kukaa kimya kwa msanii mkubwa kama dai ni shida jamii haitokuelewa
 
Ni katika wimbo wake mpya uitwao bora nikae kimya. Diamond amegusia ugomvi wa Makonda na Gwajima na ushiriki wa Mange. Amegusia tatizo la vyeti la Makonda na shinikizo la kutaka atenguliwe.
Katika wimbo huo mpya amegusia wimbo wa Ney na kukamatwa kwa Ney, kupotea kwa Roma.

Ametumia fasihi ya hali ya juu lakini wimbo huu unamuweka kwenye kundi la waoga wanaohofia maisha yao. Diamond anasema kwenye wimbo huo ameonywa na mama yake juu ya kusema chochote kwa yanayotokea.

Anasema kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mashabiki wakimtaka aseme chochote kuhusiana na yanayoendelea na wengine wakimtuhumu kuwa anaogopa kusema kwa kuwa Makonda ni mlezi wa Wasafi.

Diamond anasema alishindwa kupost wimbo wa nay japo ni rafiki yake wa karibu (kwa sababu ya maudhui) lakini aliumia sana Nay alipokamatwa.

Amegusia pia mgogoro ya CCM na CHADEMA.

Ametumia ufundi wa kisanaa hasa kuwasilisha ujumbe wake, lakini wimbo huu unaweza kutafsiriwa kuwa anaonyesha woga katika kuipigania jamii yake na kukemea maovu katika jamii.

Pia udhaifu mwingine ni kwamba kutumia neno "eti" kwenye swala la kuvamiwa kwa clouds media kunamuweka upande wa wavamizi kwani anatilia shaka swala ambalo ni dhahiri lilitokea

Hata mimi nimeamua kukaa kimya rasmi

Ukijifanya unajua kuongea, utapotezwa [emoji22][emoji22][emoji22]
 
Diamond ni mnafiki.,ask me why,nitajibu kwa kifupi

1.kama mama yake amemwambia akae kimya kwanini katunga wimbo??Huo ndio ukimya??

Nyerere ambaye ndiye aliwekwa kwa cover ya Huo wimbo alikuwa hakai kimya,alikuwa anaonya,kukemea na Tena akawaencourage vijana wawe na ujasiri WA kuhoji,,Leo hii diamond anasema tukae kimya.,,ubashite huu.

Pia,ameonesha kukerwa na swala la kudiscuss vyeti vya bashite!!,hivyo hakupenda wimbo WA naytruboy!!!,hivyo alitaka wasanii wote wakae kimya!!!!wasihoji,,huyu kijana anawaangusha watz,,sisi tunahoji alipo Roma,wasanii wenzake wamekusanyika kutia juhudi ili mwenzao apatikane,yeye itakuwa alikuwa anarecord(hakutokea pale)

Kwahiyo tiffa akipotelea pasipofahamika napo atakaa kimya?au ni kwa sababu hayajamkuta yeye,??
Unatakiwa ujue kutafsiri ujumbe through wimbo mzima na sio neno moja.....kwa ujumla anakemea mambo yote yanayoendelea Tanzania km taifa tunaenda wapi? tumepoteza upendo na utaifa.tushikamane tuijenge Tanzania.

Mfate mwalimu wako wa kiswahili akufundishe kazi ya sanaa popoma wewe!
 
Wewe ndio unasema juu ya uoga.

Mjifunze kuheshimu maamuzi ya binadamu wengine, sio lazima kila mtu atafute pesa kupitia kiki ya Kiongozi kwa kufata mkumbo wa uongo unaotungwa.

Mnapenda kuamulia watu kama vile, nyie mnaishi kwa kuamuliwa.

Amewapa ukweli na maisha ni yake.

Makonda oyeeeeee
Hamnaga shida, na yeye tumemsikia na tutamfikia Kama mpiganaji wa kijani -Nape!
 
Utafika muda nae atasema tu ngoja atajwe kwenye orodha
 
Bora tu angekaa kimya kuliko kutoa huu wimbo,tayari kashaonyesha anamtetea bashite ambaye anatiliwa mashaka kutokana na ishu za kufoji vyeti,kumiliki magari ya watu aliowataja kwenye matumizi/biashara ya madawa,kuvamia clouds media,tukumbuke alimpiga Warioba........
Bora kukaa kimya kuliko kuongea pumba ukaharibu cv yako,mondi kaonyesha kuwa ni pumba
Kuna tatizo akimtetea? Kama wewe ulivyo na uhuru wa kutomtetea yeye pia ana uhuru wa kumtetea.
 
Back
Top Bottom