Diamond aachia wimbo mpya "Acha nikae kimya"

Nimesikiliza wimbo wa Diamond mpya wa acha nikae kimya nimejiuliza maswali kadhaa. Anasema ana kaa kimya huku tayari kaongea. Kingine anatuona wote tunaojadili habari za bashite hatuna kazi ila yeye tu ndio ana kazi. Sijamwelewa.

Kingine anasema haya tunayoyajadili yanatokana na kupambizwa na watu watatu kama sio wawili yaan Gwajima na Mangekimambi. Kwa lugha rahis sisi tumeshikiwa akili na hawa watu wawili jambo ambalo si kweli. Tumeanza kujadili elim ya bashite tangu 2015. Tunajadili bashite kuvamia clous tumeona kwa macho yetu. Tunajadili mali za bashite tunaziona kwa macho yetu. Kwann atuone tumeshikiwa akili??

Kuna mengi ameongea hebu mskilizen wenyewe ila binafs naona kwa sasa Diamond anapotea. Urafiki wake na makonda uishie huko huko wanakopata hela GSM . Huku anaingia siko.

Asitufundishe tuwe na aman huku wenzetu hatujui wako wap. # free Roma na wenzake. Tuonyeshen japo kaburi la Ben saa8.

Wimbo huu hapa

 
Ninachosikitika siasa zimetugawa, yaani imekuwa kama uadui, na hii sumu wanaisambaza watu wa upinzani ni sumu mbaya sana, itafika kipindi utashindwa kumsaidia mtu tu kisa itikadi zenu tofauti, sasa kosa la diamond platnumz lipo wapi, hii inchi kila mtu yupo free kuchagua anachokitaka ili mradi asivunje sheria, diamond kawasilisha maoni yake kupitia mziki. Kuwa na itikadi tofauti isiwe tatizo, ila Ninachosikitika sana wanasiasa na mitandao ya kijamii inatugawa vibaya sana, mpaka inafikia Kipindi tunaomba mabaya yatokee kwa nchi yetu, ili kuikomoa serikali, yaani mpaka kwenye kusifia tunakosoa na kwenye kukosoa tunasifia.Watu wanaomponda diamond platnumz ndio hao wanalalamika kila siku inchi haina demokrasia, lkn hawajui diamond platnumz ametumia haki yake ya msingi ya demokrasia kawasilisha mawazo yake kupitia mziki wake. Tanzania kwanza, tusilichukulie hili swala la ROMA kisiasa eti ni la upande fulani. Nammlaani sana kimambi, kwani hii sumu anayoisambaza, haina tofauti na kile kituo cha radio Rwanda kilichorusha habari za kibaguzi, mwisho wake kukawa na mauwaji ya Kimbari. Watanzania tuwe makini sana tusiruhusu mitandao ya jamii na wanasiasa watugawe.
 
Ndio anapotea kimuziki huyo..hayo maneno amwambie Mzee Kipara aliyewapiga mkwara watanzania wasiende kumuona mtanzania mwenzao Lema alipokuwa gerezani
Mbona kawaida tu,kila kitu kina mwanzo na mwisho,ila dogo kaongea point!
 
Aisee ila naamini huyu mond hamjui bashite kwani huyo sio wakucheza nae atakuja kumgeuka tu siku moja cc CMG, time will tell kwani huyo bashite naamin anakoelekea atakuja kumteka mtu mwenye wadhifa kama mond akijua media zitaandika ndani na nje ya bongo na pale atapomrudisha aonekane amefanya kaz nakupata ujiko. mond watch it!
 
Acheni upuuzi,, peleka jukwaa husika kule,, tunatafakari yanayoendelea nchini unatoletea mambo ya viuno huku,, πŸ™πŸ™πŸ˜‘πŸ˜‘
 
Daimond,

Ni bora ungemsikiliza mama ako then ukakaa kimya kivyako, ni upumbavu wa hali ya juu kuja kwenye kikao cha wanaume wenzio wanaojadili kitu fulani then ww unakuja unasema mama kanambia nisicheze na nyie eti nyie na wachochezi,
Hivi wote hatuna wazazi? hv huyo mama ake akimwambia awaue watoto wake atafanya hvyo?
Au tuchukulie mama yake huyo kapotea siku nne hatoanzisha # zake?
Kweli adhabu ya kaburi aijuaye maiti,
we've long way to freedom kama wasemaji wetu wenyewe ndo hawa kazi ipo
 
Ndio maana huwa nakishangaa sana kizazi cha watoto wa vyuoni na hawa wa sekondari wanaovaa suruali za kubana mpaka magotini halafu juu zipo kawaida. Ni rahisi sana kuteka akili zao na hisia zao.

Unatazama nani ni mtu mwenye ushawishi kwao (idol) halafu unabaki kucheka peke yako!. Diamond ni tajiri sana kwa maana ya vipaji alivyojaliwa na Mungu, uwezo wa kujituma binafsi, uwezo wa kutokata tamaa. Ni kijana ambaye yupo tofauti sana na wengi wa sasa, ambao wanadhani wanajua mengi kumbe vichwani zero.

Labda tatizo lao ni kukua katika nyakati ambazo uhuru wa kuongea na mkubwa sana, na nyakati ambazo dunia ni kijiji haswa, kwa maana ya mawasiliano ya hali ya juu sana. Ndio maana inakuwa rahisi kwa wao kupumbazwa hata na fikra ambazo ni nyepesi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…