All in all Harmonize baada ya kujitoa ndipo amepanda zaidi hata kama hamfikii Diamond, na angeendelea kukaa pale angekuwa anamfanyia kazi Diamond tu ambaye kila kizuri anataka awe ni yeye. Huwezi kumlinganisha Harmonize na wooote waliopo chini ya lebo ya WCB.
Na ndio maana hata wale walio nje ya lebo yake wanapotoa ngoma za maana yeye anatoa hela kuhakikisha hazi trend kwenye Media. Mtu wa hivi ni hatari sana katika ukuaji wa wasanii wengine
Respect Harmonize uliona mbali na upo huru.
Namkubali Diamond sana lakini siukubali UKOLONI WAKE kwa anaowasaini
Sasa kama WCB wakoloni,hizo Label nyingine zipoje.
Msanii anatoka WCB tayari anabrand, brand tu ni hela tosha na anaweza kuilipa hela ya uwekezaji yy mwenyewe.
Hebu niambie hao wasanii waliotoka label nyingine wa nini sasa hivi.
Kaka hamna kitu kigumu kama kuwekeza hela kwa mtu husiye mjua na ndio maana label nyingi kibongo bongo zipo zipo tu,maboss hawaweki hata shilingi kumi.
Konde yule Label anaitumia tu kuonekana nae ana label ila hana time ya kuwekeza hata Senti kwa Ibra,ndio maana kila siku anasikika yy Ibrah hajulikani yupo wapi kwa kifupi jamaa ni mbinafsi.
Kiba wale madogo ndio wanao muandikia nyimbo siku hizi,Utu ile imeandika na Vanilla,pamoja na ukubwa wa ile nyimbo hajalipwa hata shilingi kumi. Alichofanya Kiba kumsainisha kwenye label,ila ile nyimba angeiimba mwenyewe sasa hivi anagekuwa na hela ndefu, kwani yupo kwenye label ambayo haijawekeza chochote kwake, Tony nae kazi yake kama Vanila kumwandikia nyimbo Kiba,kwani nae kisha waandikia wasanii wakubwa mmojawapo Nandy.K2ga yupo King mwaka wa tano,ana nini leo label ikimtema hushaiuliza atakuwa na hali gani,hapo sasa ndipo uone ugumu na moyo wa kuwekeza hela kwa mtu husiye mjua.
Ukitizama ndipo utajua Mondi anamoyo wa kusaidia,hamna kitu kigumu kuwekeza hela kwa mtu husiye mjua,hao ndugu zetu wa ukoo watu wanaogopa kuwasaidia.
Wale madogo wameondoka Konde wamechoka hata hits songs hawana,brand hawana wanashindwa hata kuitwa kwenye show za vipaimara. Wanagalie wasanii wanaovunja mkataba na WCB,wanatoka na brand zao ambazo zimejengwa na WCB ma hela za kusurvive wanazo.
Bongo hamna msanii mwenye upendo anaye mzidi Diamond hayupo,kuwekeza kwa mtu husiye mjua ni watu wachache mno wenye mioyo hiyo.