Diamond afunga hospitali ya Amana kwa muda

Hili ni jambo zuri na la kuigwa kwa kweli...
 
Mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo kwa kutembelea hospitali ya Amana ambako amesababisha shughuli zisimame kwa muda.

Katika ziara yake hiyo aliyoifanya leo Jumatatu, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni.

Muda wote aliokuwa hospitalini hapo wagonjwa na waliokuwa wakiwahudumia walitoka kwa ajili ya kumuona msanii huyo.

Diamond ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya Hallelujah, amesema alifikia uamuzi wa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndiyo mahali alipozaliwa.

Amesema anajivunia kuwa na watu wazuri wa karibu ambao wanamshauri kurudisha kwenye jamii inayomzunguka.

"Najua hospitali kuna mahitaji mengi nikaona kwa uwezo wangu mdogo nami nishiriki kusaidia mahali nilipozaliwa siku ya leo ili nipate pia fursa ya kuwaona watoto waliozaliwa tarehe kama yangu,"

"Nafahamu kuna changamoto nyingi, niwasihi watu wengine waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia," amesema Diamond.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Shaany Mwaruka amempongeza Diamond kwa uamuzi huo na kutaka watu wengine waige mfano huo.

"Ungeweza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa kwa kufanya chochote kile, lakini ukakumbuka mahali ulipozaliwa."

Dk Mwaruka amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kutokana na idadi kubwa ya watu wanaowahudumia.

Kwenye ziara hiyo Diamond ameambatana na meneja wake, Said Fella.

Mwananchi
Huwa nawaambia watu kwamba huyu jamaa,anaona mbali sana,he is always one step ahead,lakini watu bado huwa wanataka kumringanisha na nani vile????,
 
Its good to be in position of giving than to be given, giving is God's ministry to give what you cherished most and not to give what you don't want or need naseeb Abdul (diamond platnumz) your hands and carrier will never run dry as sure as God lives, amen

Once again Happy birthday Tanzanian music icon SIMBA
 
Kama anatoa kwann asiwe na mafanikio aliyonayo???
 
3fceacdc490073f5afa4755be392bed1.jpg
 
nice...nazani kila aliyewahi kuingia leba kama mzazi lazima ataguswa na hiki alichokifanya chibu...
 
Mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo kwa kutembelea hospitali ya Amana ambako amesababisha shughuli zisimame kwa muda.

Katika ziara yake hiyo aliyoifanya leo Jumatatu, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni.

Muda wote aliokuwa hospitalini hapo wagonjwa na waliokuwa wakiwahudumia walitoka kwa ajili ya kumuona msanii huyo.

Diamond ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya Hallelujah, amesema alifikia uamuzi wa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndiyo mahali alipozaliwa.

Amesema anajivunia kuwa na watu wazuri wa karibu ambao wanamshauri kurudisha kwenye jamii inayomzunguka.

"Najua hospitali kuna mahitaji mengi nikaona kwa uwezo wangu mdogo nami nishiriki kusaidia mahali nilipozaliwa siku ya leo ili nipate pia fursa ya kuwaona watoto waliozaliwa tarehe kama yangu,"

"Nafahamu kuna changamoto nyingi, niwasihi watu wengine waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia," amesema Diamond.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Shaany Mwaruka amempongeza Diamond kwa uamuzi huo na kutaka watu wengine waige mfano huo.

"Ungeweza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa kwa kufanya chochote kile, lakini ukakumbuka mahali ulipozaliwa."

Dk Mwaruka amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kutokana na idadi kubwa ya watu wanaowahudumia.

Kwenye ziara hiyo Diamond ameambatana na meneja wake, Said Fella.

Mwananchi
Chibuuuuu!!! Can't imagine how our mom feel proud of having u as her son congrats ila Nina kawivu ka maendeleo najtahid nifike n kutimiza ndoto nilzonazo
 
kuwa na washauri wazuri nakukubali kushaurika jambo nzuri sana ila yule jamaa yetu kule posta sijui nikwanini asee
 
Mi napenda kumwangalia Diamond zaidi sababu najifunza vitu vingi kupitia kwake huku naburudika na Mziki wake.
Yule mwingine napata Mziki tu. Hana cha zaidi.

Hongera Diamond, we ni zaidi ya Mwanamziki. Nakumbuka kuna Mwanamziki wa zamani alikuwa anaumwa ukampa gari la kutembelea. Kitu kama Tx William. Unamoyo wa kutoa toka zamani.
 
Back
Top Bottom