Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Hongera domo
Mkuu ina maana unamzungumzia yule BABU WA KARIAKOO??Hapo ndipo anaowaachaga wale waudha mitumba wa kaliako na ule mkimbizi changudoa wa USA..
Huwa nawaambia watu kwamba huyu jamaa,anaona mbali sana,he is always one step ahead,lakini watu bado huwa wanataka kumringanisha na nani vile????,
Mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo kwa kutembelea hospitali ya Amana ambako amesababisha shughuli zisimame kwa muda.
Katika ziara yake hiyo aliyoifanya leo Jumatatu, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni.
Muda wote aliokuwa hospitalini hapo wagonjwa na waliokuwa wakiwahudumia walitoka kwa ajili ya kumuona msanii huyo.
Diamond ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya Hallelujah, amesema alifikia uamuzi wa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndiyo mahali alipozaliwa.
Amesema anajivunia kuwa na watu wazuri wa karibu ambao wanamshauri kurudisha kwenye jamii inayomzunguka.
"Najua hospitali kuna mahitaji mengi nikaona kwa uwezo wangu mdogo nami nishiriki kusaidia mahali nilipozaliwa siku ya leo ili nipate pia fursa ya kuwaona watoto waliozaliwa tarehe kama yangu,"
"Nafahamu kuna changamoto nyingi, niwasihi watu wengine waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia," amesema Diamond.
Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Shaany Mwaruka amempongeza Diamond kwa uamuzi huo na kutaka watu wengine waige mfano huo.
"Ungeweza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa kwa kufanya chochote kile, lakini ukakumbuka mahali ulipozaliwa."
Dk Mwaruka amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kutokana na idadi kubwa ya watu wanaowahudumia.
Kwenye ziara hiyo Diamond ameambatana na meneja wake, Said Fella.
Mwananchi
Chibuuuuu!!! Can't imagine how our mom feel proud of having u as her son congrats ila Nina kawivu ka maendeleo najtahid nifike n kutimiza ndoto nilzonazo