Diamond aibuka na kupinga wimbo wake kufungiwa, asema nchi ina wenyewe

Diamond aibuka na kupinga wimbo wake kufungiwa, asema nchi ina wenyewe

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Diamond platinumz ameibuka na kupinga wimbo wake na Zuchu kufungiwa akihoji ni sababu zipi hasa zilizopelekea wimbo wake kufungiwa.

20220508_173437.jpg
 
Basata wamempa mswahili cha kuongea, nyimbo sijaiona lakini kusema kashoot kanisani ndio afungiwe haiingi akilini.

Nakumbuka banana video ya ZOBA kama sikosei ilikuwa na scene ya kanisani, sikumbuki kama ilifungiwa.
 
Wakati mwingine wakafanyie hayo maigizo yao kwenye misikiti! Kwa nini kanisani kila siku? Yeye na huyo mwezi wake, wote ni waislam! Iweje wasiende kufanyia hiyo shooting msikitini, au kwenye Madrasa?

Hongereni sana BASATA. Angekuwa ni Mkristo akaenda kufanya hayo maigizo msikitini, muda huu zingekuwa kelele nchi nzima.
 
Mbona hakutumia msikiti. Nyumbu mkubwa Sana huyo Mondi a k.a mtembeza mkongojo kwa Wanawake.
Unampangia atumie jengo gani ? Ulimtungia nyimbo au ulikuwa Director wa hio Scene ?

Tutakapoanza kupangiana cha kufanya na wapi tukifanye basi dunia hii itakuwa a very Boring Place..., Yaani Magereza ya Nje
 
Unaweza kutuambia umuhimu wa ile scene ya kanisani kuwepo pale ni nini? Na kwanini huo umuhimu usiwe msikitini ilihali zote nyumba za ibada?

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom