Huo utamaduni wa hawa wasanii kukimbilia makanisani kufanyia maigizo yao uliletwa na nani?
Kanisa ni nyumba ya ibada, inaheshimiwa na wanaoabudu mahali husika, unapokwenda kufanyia maigizo yako pale kisa kuna fulani aliwahi kufanyia huko haiwezi kuwa defence.
Huyo director wake alikosa sehemu nyingine yoyote ya kufanyia hilo igizo lao? au walichagua kanisani kwasababu wanaamini Kanisani ndio delicate place itawavutia watu kutazama?
Hao watu watakaovutiwa kuona nyumba yao wanayoiheshimu kwa ajili ya ibada zao inafanyiwa maigizo ni watu wa aina gani? wajifunze kuheshimu vitu vya watu, waache kufanya mambo kwa mazoea.
Naamini huu uamuzi wa Basata utakuwa fundisho kwa wajinga wengine waliokuwa na mipango ya aina hiyo. Diamond kama anaona ameonewa na Basata next time akaombe kufanyia maigizo yake msikitini.