Diamond ajisalimisha Polisi baada ya kuvunja sheria za Barabarani

Nifah

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2014
Posts
34,020
Reaction score
79,098
Baada ya fununu na malalamiko mengi hatimaye Diamond nae kaitwa kutoa maelezo polisi.

Hata hivyo,bado haijafahamika kaitwa kwa tuhuma gani.
Tetesi ni kwa kosa la kuendesha gari huku akicheza wimbo wa Marry you na kuachia usukani akiwa na familia yake kwenye gari,au tuhuma za madawa ya kulevya zinazomuandama.

Iliwahi kujadiliwa humu na watu kusikitishwa kwa kitendo hicho, zaidi soma Diamond Platnumz akamatwe kwa kuvunja Sheria Barabarani

Swali ni je,Diamond nae atalala kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani kama wenzie?


My take; kama ni suala la madawa ya kulevya basi WCB wengi wana tuhuma za madawa ya kulevya.
Wakiwemo Dansa Mose Iyobo,Queen Darling na Shetta.

Haki itendeke na sio janjajanja za kuitwa polisi na kuachiwa ili kutufunga midomo tuliokuwa tunapiga kelele.

Nifah

=======

UPDATES;

=======



Si kweli kwamba Diamond aliitwa kuhojiwa sababu ya kujihusisha na Madawa ya Kulevya, Bali aliripoti Polis baada ya Video yake kusambaa ikimuonesha akivunja sheria za barabarani.

Haya ndio Maneno aliyoyaandika Diamond...


Leo nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na Vidoe Clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na pia kuachia usukani na kucheza.... Nikapewa Onyo na Kulipa faini kulingana ya Mujibu wa sheria... Tafadhali watanzania na Vijana wenzangu...

Tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe pia..
 
hakika kakuna jiwe juu ya jiwe litakalo salia
 
Tuhuma yake ni kuendesha gar akiwa anaimba na kucheza huku gar ikiwa inatembea... I will mary u...!!
 
Acha uongo wewe
Tangy link kamanda Mpinga akahusika na madawa ya kulevya?
Hiyo ni kuhusu ishu ya kuendesha gari akiwa hajafunga mkanda uku akiimba mziki na familia yake
 
Wampeleke kwa mkemia mkuu apimwe mkojo na damu kwanza halafu waende nyumbani kwake wampekue chumba hadi chumba.
 
Acha uongo wewe
Tangy link kamanda Mpinga akahusika na madawa ya kulevya?
Hiyo ni kuhusu ishu ya kuendesha gari akiwa hajafunga mkanda uku akiimba mziki na familia yake
Ha ha ha ha ha safi sana umempatia huyo anataka kuudanganya uma
 
Mie naipendea TZ na mamlaka zake kwa kutoa haki stahiki... hakunaga raia aina mbili waka sheria aina kadhaa... wote amri moja !!!!

Mungu ibariki
 
Peleka na ushahidi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…