Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,772
- 22,598
Akizungumzia kuhusu vijembe vingi ambavyo diamond amekuwa akitupiwa na mwanamama huyo hasa vya hapa karibuni alipokuwa kenya, Diamond alisema ; "hayo ya kenya bwana tuachane nayo, mimi nadhani yameshapita naomba tuendelee na haya yasasa itapendeza sana”
Hata hivyo, mwandishi hakuishia hapo ndipo alipoamua kumuuliza moja kwa moja kuhusu yeye kusafiri kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya kuomba radhi kwa zari huku akienda kwa siri mara kwa mara na Diamond alijjibu kuwa safari zake za Afrika ya Kusini hazihusiani na mambo hayo.
"N kweli ninaenda na so mara moja au mara mbili nimekuwa ninaenda,nakwenda kule sio kwa ajili ya kumuomba msamaha , hapana ila ninakwenda kule kwa ajili ya kuona wanangu tu,haiwezekani niwe ninatuma pesa za matumizi tu alafu ninafka mpaka Afrika ya Kusini na nisiende kuwaona wanangu.
"Hao wanaosema kuwa sijui nimekuwa nikimuangukia nadhani yatakuwa ni maoni yao tu wala sio yangu, ni maneno yasiyokuwa na msingi, zari ni mama wa watoto wangu na itabaki kuwa hivyo."
Mpekuzi