Niliposoma swali kwenye title yako, nilifikiri unamaanisha mtu nyuma ya bifu yao, Mara nyingi issue kama hizi huwa zinatengenezwa kwa manufaa ya kibiashara zaidi, panaweza kuwa hakuna tatizo wala uhusiano mbaya kati ya watu hawa wawili, lakini panatengenezwa issue kuwa hawaelewani ili kuweka majina yao katika midomo ya watu na kutengeneza team za kiuhasama kwa lengo la kibiashara.
Mara nyingi washabiki na wana team wanakuwa hawajui lolote nyuma ya pazia, mtu anaweza mpenda mmoja wao sababu tu eti yule mwingine ana maringo, wengine utasikia mimi napenda tu mziki wa fulani bila kujali ubora wala umahiri katika kazi, Nilisikia mwingine akisema " Mimi nampenda fulani kwasababu tu ni mpiganaji na mbunifu katika maisha". Mwingine anampenda fulani kwa uvaaji wake tu, Mwingine kwa muonekano wa mwili wake tu.
Siku bahati mbaya ikatokea watu hawa wawili wakakutwa pamoja wakicheka na kufurahi pamoja au wakaamua kufanya kazi pamoja, huu ndo utakuwa mwisho wa kambi zao mbili na mwisho wao hao wawili utakuja haraka sana. Kazi ya mtu wa tatu( invisible person) ni kuhakikisha hali inabaki kama ilivyo kwa gharama yoyote, wana habari wamekuwa wakitumika bila kujua katika kufanikisha haya.