Selwa
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 583
- 590
Jamani eeeeh...kelele.nyingi za Diamond na watu mtandaoni zimenifanya niweke hiii wazi. Nilikuepo eneo la tukio nikitoka mwanza kwenda dar. Huku nikiwa nimebook fastjet..ndege haikufika. Diamond alichelewa sana kufika airport. Dirisha la ndege linafunga 40 mins before departure tuliondoka na dakika 45.kafika kama sio saa mbili kamili na dakika 10.... kwa kawaida kwa warukaji wa ndege za tanzania hujua kuwa wanasaidiana. Kama fastjet imechelewa au haiji na kuna wateja wameshacheck in wa fastjet departure room na ndege haipo air tanzania inakubeba kama nafasi imebaki kama tu upo departure room... na kama air tanzania imechelewa au haipo na fastjet imefika uwanjani na wateja wa air tanzania wapo departure.room,Wateja wa fastjet wataingia wote alafu rubani atawaruhusu wateja wachache wa air tanzania wapande (tena bure) kama kuna nafasi.. mimi nilikuwa fastjet ila nilipanda air tanzania kwasababu kulikuwa na no show ya fastjet. Tena rubani anatangaza kabisa kwa abiria wake tunabeba wenzetu wa ndege flani kwani ndege yao haipo na abiria muwe wavumilivu. Hii imenitokeaara mbili...mara moja fastjet ilinibeba air tanzania ilikuwa haipo tena no charge nilikuwa naenda mbeya na juzi air tanzania imenibeba fastjet ilikuwa haipo..sidhani kama ni problem na ni wachache sana wanabahatika maana mnaweza pewa watu 10 tu au 5 kutokana na nafasi ya ndege. Hivo mpaka rubani agawe siti yako ni kwamba haujacheck in..angekuwa amefika angekuwa ndani kule kwenye departure room sio nje. Na siku hiyo wateja wa fastjet walikuwa wengii mnooo.