Hapana haiwepo hivyo. Kwann wasafi wafosi kwa kiba lakini wasifosi kwa harmonize. Hivi msanii km Drake analetaga nyimbo wasafi mbn anapiga nyimbo zake.. Diamond ameamuwa kuwa Ruge na yeye.
Ruttashobolwa na wanaokuunga mkono mnaongea mambo kirahisi sana... labda kutokana na ushabiki tu au kwa kushindwa kufahamu possible outcomes!
Kwanza mnatakiwa kufahamu yafuatayo!!
"Bifu" kati ya Kiba na Diamond ni ujinga ujinga na utoto tu, lakini "bifu" kati ya Harmonize na Wasafi ni la kibiashara!!
Kwa mujibu wa Harmonize mwenyewe, kavunja mkataba na Wasafi kwa kulipa 500M!!
Wakati hayo yanatokea, media za Bongo huwa hazilipi mrabaha kwa kupiga kazi za wasanii na wasanii wenyewe wanaridhika na hiyo hali kwa ajili ya kupata airtime, ingawaje pia system yenyewe ya ulipaji ni ya hovyo sana!!
Lakini wakati Wasanii wenyewe wanaridhika kutolipwa mrabaha in exchange for airtime, sheria inawapa haki ya kupata mrabaha.
Sasa unapochukua issue ya Harmonize na Wasafi ambao wao walim-charge 500M bila kumwangalia usoni, unatakiwa kuwa makini sana na ngoma zake kwa sababu ukifanya masihara anaweza kuwapeleka mahakamani na kufungua kesi ya kupiga nyimbo zake bila ruhusa na kutaka mumlipe mamilioni kama sio mabilioni ya pesa kama ambavyo na nyinyi mlimlipisha!!
And trust me, akienda mahakamani mtalipa tu kwa sababu haki itakuwa upande wake... rejea kesi ya Tigo na akina Mwana-FA!!
So, kabla hamjaanza kutangaza ubaya wa watu mnatakiwa kwanza kufahamu how the industry works!!
Kwa issue ya Harmonize, hata ningekuwa mimi kwenye management ya Wasafi KATU nisingepiga nyimbo zake unless awe ameji-commit kimkataba kwamba hatadai chochote kwa ngoma zake kupigwa kwenye media husika!
Kinyume na hapo, itakuwa ni kucheza na petrol jirani na wavuta sigara!!