Diamond amepiga marufuku nyimbo za Harmonize kupigwa Wasafi FM

Diamond amepiga marufuku nyimbo za Harmonize kupigwa Wasafi FM

Clouds ni watu wa Amani na upendo wasanii wengi wakiwemo Diamond ndio wamewakataza kucheza nyimbo zao....

Sent from my iPhone using Tapatalk
Umeusikia utetezi wa Salam na Babutale kuhusu wao kukataza nyimbo zao kupigwa lakini?

Wanasema wao mwanzoni hawakukataza nyimbo zao kupigwa Clouds ila wao Clouds ndo waliacha kupiga nyimbo zao, ikapita muda mrefu zaidi ya mwaka wakiwa hawapigi. Baadae ghafla wakaanza kupiga, wakaanza na wimbo wa Mbosso. Ndipo na wao wasafi wakareact kwa kuwaandikia barua Clouds kuwakataza wasipige nyimbo zao mpaka wajieleze kwanini hapo mwanzo walikua hawapigi nyimbo zao mpaka leo waamue kuzipiga tena.

Rejea interview ya Kusaga wasafi TV na interview aliyofanya Salam Dizzim online kujibu ile interview aliyofanya Kusaga Wasafi TV

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fundi
harmonizenews___B_Uisxhg7CM___.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyinyi si mnasema wasafi media Ni ya kusaga diamond yupo pale Kama kivuli sasa inakuaje unamlaumu diamond kutopeleka wasafi media pale kwenye uzinduzi wa Harmonize?
Ni kweli Mke wa Kusaga ana Hisa nyingi Wasafi Media ( Kwa mujibu wa Documents za TCRA ).

Ila kwa kawaida Venture Capitalists macho yao huwa kwanza yako kwenye Finacial Statements.

Wakiona pesa hziiingii na wako katika hatari ya kupoteza MTAJI wao ndio huwa wanakuja juu, ikiwemo hata kukutimua.

Ila kama Financial Terms ziko vizuri, as long as idea ni yako na kampuni inaenda, hawajali sana kuhusu wewe unaendeshaji kampuni.

Ndio maana watu walikua wanakosana na Ruge tu na ngoma zao zinakuwa hazipigwi Clouds na watu hao hao hawakuwa na Matatizo na Kusaga.

The same to East Africa Radio.

Wasanii ambao ngoma zao hazipigwi hapo haimaanishi walikuwa hawaelewani na Mengi.
 
Mbona ujajibu hoja ya msingi inakuaje unamlaumu diamond hajapeleka wasafi media kwenye uzinduzi wa album ya harmo?
 
Kama ni kweli anaizika radio muda sio mrefu clouds sasaivi wanapiga nyimbo mpaka za JD halafu diamond usharobaro radio changa anaanza mambo ya kipuuzi. itamfia
 
Ile sio TBS CCM, ni malia ya mtu binafisi akitaka ata afunge hamna atakae mpigia kelele, apige nyimbo za miaka 70 tutasikiliza tu tunao zielewa.
 
Hapana haiwepo hivyo. Kwann wasafi wafosi kwa kiba lakini wasifosi kwa harmonize. Hivi msanii km Drake analetaga nyimbo wasafi mbn anapiga nyimbo zake.. Diamond ameamuwa kuwa Ruge na yeye.
Ruttashobolwa na wanaokuunga mkono mnaongea mambo kirahisi sana... labda kutokana na ushabiki tu au kwa kushindwa kufahamu possible outcomes!

Kwanza mnatakiwa kufahamu yafuatayo!!

"Bifu" kati ya Kiba na Diamond ni ujinga ujinga na utoto tu, lakini "bifu" kati ya Harmonize na Wasafi ni la kibiashara!!

Kwa mujibu wa Harmonize mwenyewe, kavunja mkataba na Wasafi kwa kulipa 500M!!

Wakati hayo yanatokea, media za Bongo huwa hazilipi mrabaha kwa kupiga kazi za wasanii na wasanii wenyewe wanaridhika na hiyo hali kwa ajili ya kupata airtime, ingawaje pia system yenyewe ya ulipaji ni ya hovyo sana!!

Lakini wakati Wasanii wenyewe wanaridhika kutolipwa mrabaha in exchange for airtime, sheria inawapa haki ya kupata mrabaha.

Sasa unapochukua issue ya Harmonize na Wasafi ambao wao walim-charge 500M bila kumwangalia usoni, unatakiwa kuwa makini sana na ngoma zake kwa sababu ukifanya masihara anaweza kuwapeleka mahakamani na kufungua kesi ya kupiga nyimbo zake bila ruhusa na kutaka mumlipe mamilioni kama sio mabilioni ya pesa kama ambavyo na nyinyi mlimlipisha!!

And trust me, akienda mahakamani mtalipa tu kwa sababu haki itakuwa upande wake... rejea kesi ya Tigo na akina Mwana-FA!!

So, kabla hamjaanza kutangaza ubaya wa watu mnatakiwa kwanza kufahamu how the industry works!!

Kwa issue ya Harmonize, hata ningekuwa mimi kwenye management ya Wasafi KATU nisingepiga nyimbo zake unless awe ameji-commit kimkataba kwamba hatadai chochote kwa ngoma zake kupigwa kwenye media husika!

Kinyume na hapo, itakuwa ni kucheza na petrol jirani na wavuta sigara!!
 
Kama ni kweli anaizika radio muda sio mrefu clouds sasaivi wanapiga nyimbo mpaka za JD halafu diamond usharobaro radio changa anaanza mambo ya kipuuzi. itamfia
Hivi unajua hatari ya kupiga nyimbo za msanii ambae mlivunja nae mkataba kwa kumlipisha mamilioni ya pesa?!

Mkipiga bila kuwa na makubaliano nae kwamba hatadai mrabaha, unadhani akiwapeleka mahakamani hata kwa kuwakomoa kama ambavyo watu wanaamini Wasafi walimkomoa kumlipisha 500M, unadhani watatoka?

Haya mambo mnaongea kirahisi sana but trust me, hatari ya kupiga nyimbo zake bila kuwekana sawa ni kubwa kuliko mnavyodhani! Nani alitarajia Tigo wangelipishwa 2B na akina Mwana-FA?!
 
Back
Top Bottom