Chuki itasaidia nini? asingekuwa maarufu angemtafuta huyo baba popote alipo. hiyo ndo balaa ya kuzaa na mswahili. huyo mama ni uchoyo tu unamsumbua anaona akiacha mtoto awasiliane na babake baba atashika kila kitu na yeye atakosa.
Ndio maana anaendelea kumjaza chuki mtoto.
Ishu ni kuwa kwanini hakumtunza Diamond kipindi anaitwa naseeb amemfata kumuomba ada ya shule matokeo yake Dogo anapotozewa hata hela ya pipi kijiti, hivi unahitaji kujazwa chuki kumchukia mtu kama huyu?
Kikubwa zaidi, diamond angekuwa mchinga unafikiri babayake angemtafuta? Kwasababu miaka yoote hiyo hakutambua makosa yake mpaka Naseeb amekuwa Diamond ndio akaanza kujisogeza, wakati kipindi hiko diamond mpiga picha na kuuza mitumba karume bado alikuwa hajatambua makosa yake
Ndio maana Diamond, akasema AMEMSAMEHE ila asitegemee treatment anayopata mama yake na yeye aipate..