Mponjoli Njenga
Member
- Aug 16, 2016
- 43
- 56
Makala ya Raia Mwema lina habari ya kufikirisha kidogo:
Mwandishi anauliza " Diamond ana fedha, lakini anauza nini?"
Hata mimi nimejikuta nikiuliza swali hili mara nyingi tu bila majibu. Wengine wanasema anauza matangazo, wengine ana studio nk. Lakini vipi ile biashara yake ya msingi : Muziki?
soma mwenyewe hapa chini:
======
NASEEB ABDUL ‘Diamond Platnumz’ ananivutia sana miongoni mwa wasanii wa muziki wa nyumbani. Ananivutia kumsikiliza na kumtazama kwenye TV.
Akiwa ananengua jukwaani unaweza kujisemea kwanini asiwe ananengua na aachache na kuimba. Akianza kuimba bado utajisemea tena kwanini asiwe anaimba pekee na si kuchanganya vitu viwili kwa wakati mmoja?
Huyu ndiye Diamond ambaye anafanya vitu viwili kwa wakati mmoja na kuvutia wengi. Wapo wanaompenda kwa kuimba na wako wanaompenda kwa kucheza.
Amejivutia mashabiki wengi kwenye maeneo hayo mawili jukwaani. Kazi zake zimemfanya hivi sasa atajwe kama msanii anayetengeneza fedha nyingi zaidi hapa nchini.
Wingi wa fedha hizo zimefanya afungue kampuni ya WCB, inayofanya kazi za kusimamia wasanii mbalimbali.
Lakini mpaka unapoweka umakini wako kusoma andiko hili, fahamu Diamond amewahi kutoa albamu moja tu ya Nenda Kamwambie mwaka 2009.
Hii ni albamu yake ya kwanza na ya mwisho mpaka wakati huu 2016. Ni takribani miaka saba sasa imepita tangu atoe albamu hiyo ambayo haikuwa na idadi kamili ya nakala alizouza.
Inakuwaje Diamond, anayetajwa kuwa msanii mwenye fedha nyingi, awe ametoa albamu moja tu kwa zaidi ya miaka saba?
Ina maana Nenda Kamwambie ndio imemlipa kiasi hiki mpaka sasa aamue asitoe albamu nyingine?
Wanamuziki, bendi na vikundi duniani kote wanaonyesha na kutangaza utajiri wao kupitia mauzo ya kazi zao ambazo zinakuwa albamu.
Hata Ali Kiba, anayekinzana naye kimuziki aliwahi kusema albamu yake ya kwanza ya Cinderella ilivunja rekodi na kuuza ‘double platinum’ kwa kuuza nakala milioni mbili.
Mauzo ya nakala hiyo anadai yalimuingizia shilingi milioni 200. Kiba aliwahi kusema hata ukimya wake kwenye sanaa haukumfanya apumzika bure, bali alikuwa na ‘jembe’ lililofanya akae pembeni kidogo.
Kwenye dunia ya sasa, wasanii wa muziki wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao na ndiyo maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.
Hii ni sheria inayotumika kwa baadhi ya nchi duniani, japo nyumbani haijaanza kutumika. Inawezekana sheria hii ingekuwepo nyumbani Diamond, angeingiza fedha zaidi.
Swali kubwa ambalo nimekuwa nikijiuliza ni hili; Diamond na wasanii wetu wengine ambao hawajawahi kutoa albamu wanapata wapi fedha za kuendeshea maisha yao ya kifahari wakati mauzo ya albamu zao ni sifuri?
Biashara ya muziki ni sawa na nyingine yoyote iwe ya kuuza barafu, mikate, machungwa au magari. Mfanyabiashara wa magari, hesabu yake hutokana na idadi ya magari anayouza. Vivyo hivyo kwa biashara nyingine.
Hawa wasanii wetu ambao hawauzi muziki, wanapata wapi fedha za kuendeshea maisha yao? Muziki bila kutoa albamu ni biashara gani?
Nafahamu kuna maonyesho mbalimbali ambayo baadhi yao wanapata. Lakini, msanii ambaye kwa mwezi anapata maonyesho manne yenye thamani ya shilingi milioni sita hadi nane; anawezaje kutoa video ambazo tunaambiwa zina thamani ya milioni 30?
Hizi hela za kutengeneza video za milioni 30 wanapata wapi wakati hawana albamu hata moja? Wanauza nini?
Vanessa Mdee ‘Vee Money’ anapokea pesa nyingi nje ya nchi kutokana na nyimbo zake kuchezwa kwenye Radio na runinga za Afrika Kusini. Katika taifa hilo, vituo vya redio na luninga huwalipa wasanii kwa nyimbo wanazozipiga ingawa hilo si kwa wasanii wote.
Kwa mfano, wasanii wanaotoka nje ya nchi kuna vigezo vinatazamwa kukuwezesha kusajiliwa na mamlaka husika na baada ya hapo unakuwa kwenye mzunguko wa kulipwa kama wasanii wengine wa nchi hiyo wanavyolipwa.
Wasanii wote maarufu duniani kama vile Chris Brown, Rihanna, Eminem, Wiz Khalifa na wengine wote wanafahamika kwa kuuza albamu zao.
Hadi leo, Michael Jackson anafahamika kwa kuuza nakala milioni 100 za albamu yake ya Thriller iliyotoka kwenye miaka ya 1980.
Kwenye biashara ya muziki, hakuna msanii aliyetengeneza fedha kwa sababu ya Fiesta au matamasha ya Kili Tour. Msanii anapata fedha kwanza kupitia albamu anazotoa.
Tunafahamu mazingira yaliyosababisha wasanii wetu waachane na utaratibu wa kutengeneza albamu. Kinachotakiwa kufanyika ni kupambana kuhakikisha kuwa mazingira yanaboreshwa ili wasanii wapate wanachostahili kwenye mauzo ya albamu zao kwanza.
Vinginevyo swali langu hili halitaisha. Diamond anapata wapi fedha za kufanya anayoyafanya wakati albamu yake ya mwisho ilitoka miaka saba iliyopita?