Diamond anafanya biashara gani?

Diamond anafanya biashara gani?

Mkuu hao Wanigeria wasiojua umiliki wa kiwanda cha Cement cha huyo Tajiri wa Africa labda wale wasiokuwa na mitandao ya kijamii.Especially wale waishio Kwa Mtogole ya Lagos. Ila sio wale wanaofuatilia latest news every time.
Usikariri Mkuu
Nakuuliza Swali Dogo tu kwa wewe unaeishi Mjini
a) Nitajie Waziri wa Tanzania ambae anamiliki Hotel kubwa Ya vyumba zaidi ya 100 hapa Zanzibar.
c)La pili,Waziri gani wa Mozambique ambae ana Hotel Hapa Zanzibar
d)Mtoto gani wa Raisi Maarufu EAT anaemiliki Hotel Zanzibar

Hapo inatosha,sasa kama umekariri nipe jibu hata la swali Moja tu wewe wa mjini?
 
Hivi mkuu Dangote unaweza ukamfananisha na huyo Waziri wa Tanzania. Huyu jamaa mali zake zote zinapatikana kwenye mitandao so huwa hamiliki mali kwa uficho kama huyo waziri mwenye hiyo hotel huko Zanzibar. Kwanza akijipambanua ataambiwa fisadi unadhani ni rahisi kihivyo kujua mali za Magufuli kuliko kujua mali za Bill Gates.
Kama unawajua hao viongozi wenye hizo hotel huenda umeyaona hayo majengo na umepata kujua hivyo kipindi cha ujenzi ulisikia tetesi tu kuwa hili ni jengo la mtu fulani ila hakuna media iliyotangaza kama ilivyotangazwa kiwanda cha cement cha Dangote ambacho Africa mashariki na kati wote wanajua kuwa kipi sisemei nchi za mbali ya hapa maana BBC waliripoti kuhusu hiki kiwanda.
 
Raia Mwema mmemtoa wapi huyo mwandishi mbona aibu hii..!
Hahaha,mkuu we acha,yaani aibu tupu
Hii ni taswira ya wandishi wetu wa Tanzania wanaoishi kwa mihemko
We si unakumbuka wale walioandika kwamba PEMBA wananchi wanakimbilia msitu wa Ngezi na wanalala huko kwa kukimbia Polisi.Cha kuchekesha waandishi kibao walioandika Pemba na Mazingira ya huko hawajui,walichofanya wlatafuta mwandishi kajanja akawa anawarushia habari za uongo.

Alichofanya Waziri,alichukua Ndege na kuwapakia waandishi wote kwenda huko,na wakakuta watu wapo makwao,na wakaambiwa kwamba Msitu wa Ngezi unalindwa na haishi mtu kule.Ikawa Aibu wakaka kimyaa.

Bado kuna tatizo sana kwa Wanataaluma wa Habari hapa kwetu.
Napenda Sana Citizen Kenya,yaani hawakurupuki
 
Ndiyo baadhi ya Watanzania walivyo Mkuu. Mambo yako yakikunyookea hawakawii kukuzushia kwamba unajishughulisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Hizi live shows anazofanya ndani na nje ya nchi zinamuingizia ngawira nyingi sana, pia baadhi ya makampuni nchini yanamtumia huyu kutangaza bidhaa zao mbali mbali.

Album hazilipi si kama zamani nilimsikia master Jay akihojiwa alisema kwa sasa soko la album halilipi, ila watu wanatoa kwa ajili ya kuipa hadhi na heshima mziki wake basi, zinazolipa sana ni tour na ndio maana msanii akitoa album faster tour zinaanza , ila soko album halilipi, labda hizo ring tone, ela inayotokana na airplay basi lkn TOUR ndio mpango mzima. Diamond platnumz mwaka huu amepiga show nyingi alikuwa na tour ulaya na sasa anatour ya Africa, tusiwe na mawazo kila anayefanikiwa ni muuza ngada au freemason kwani hayo ni mawazo ya kimasikini.
 
Hivi mkuu Dangote unaweza ukamfananisha na huyo Waziri wa Tanzania. Huyu jamaa mali zake zote zinapatikana kwenye mitandao so huwa hamiliki mali kwa uficho kama huyo waziri mwenye hiyo hotel huko Zanzibar. Kwanza akijipambanua ataambiwa fisadi unadhani ni rahisi kihivyo kujua mali za Magufuli kuliko kujua mali za Bill Gates.
Kama unawajua hao viongozi wenye hizo hotel huenda umeyaona hayo majengo na umepata kujua hivyo kipindi cha ujenzi ulisikia tetesi tu kuwa hili ni jengo la mtu fulani ila hakuna media iliyotangaza kama ilivyotangazwa kiwanda cha cement cha Dangote ambacho Africa mashariki na kati wote wanajua kuwa kipi sisemei nchi za mbali ya hapa maana BBC waliripoti kuhusu hiki kiwanda.
Majibu murua
 
Sisi tunachojua ni Mwanamuziki na muziki unalipa hasa kupitia shows

Mengine hatujui labda akamuulize yeye mwenyewe.
 
Watanzania tuna roho za kimaskini sana,huwa hatuwezi kuomba ushauri au kujifunza kwa waliofanikiwa badala yake tumekuwa tukiwaombea waliofanikiwa wafilisike wawe kama sisi,huu ujinga utatuisha lini? Tuacheni majungu ya kimaskini jamani LA sivyo tutaendelea kushona vilaka mpaka kiama
 
Si vibaya tukipata burudani kutoka studio,tukirudi tutaendelea na mjadala wetu kuhusu Icon wetu.

Kumbukeni na nyinyi kujitolea kwa kidogo mlichonacho.

Tokea haonyeshe hiki "kibanda" ndio yote haya yanakuja,lakini aliposema ana MALI ZINAZOFIKIA THAMANI YA $ 4M WATU WALIBEZA HAPA.

Angeonyesha na "kibanda" hiki alichonunua wiki moja na hiyo ya sauzi,basi wengi wangeshajinyonga humu.

Hakika hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
 
Huyu naye ni mwandishi? yani akili yake ameiaminisha msanii kupata hela hadi auze album, huyu ni mwandishi hewa.
Hiyo siyo habari, bali ni MAKALA (Writer's personal ideas). Mwandishi wa makala si lazima awe na taaluma ya Uandishi wa Habari.

Kambo la kujadili kutokana na makala hiyo ni sababu za kuficha jina la mwandishi (Na Mwandishi Wetu) na dhumuni la kuhoji maendeleo ya Diamond kulingama na hali ya soko la muziki kwa waimbaji wazawa!
 
Back
Top Bottom