Nimejikuta nashindwa jizuia kuongea chochote..kuhusu Daimond na Baba yake Mzee Abdul..
Kwa maoni yangu kama. Diamond alikuja kugundua Mzee Abdul sio Baba yake ndo
Alipaswa kumheshimu zaidi Kwa Chochote Mzee Abdul alichompa hata kama ilikuwa ni malezi ya siku moja tu..
Diamond alipaswa sasa kumlaumu na kumchukia huyo Baba yake alietajiwa Kwa kutokuwepo wakati wa maisha yake..
Badala yake Diamond naona anajipendekeza Kwa huyo biological father hadi kujiweka karibu mno na huyo mdogo wake wakati maisha yake yote
Amekuwa anamlaumu Mzee Abdul Kwa kuwatelekeza....
Sasa kama unaesema alikutelekeza unagundua sio Baba yako si ndo unapaswa kushukuru hata Kwa madogo aliyoweza kukupa?Kuku sitiri usijione huna baba?Kukupa jina lake? Kumsitiri mama yako?..
Why Mzee Abdul awe kama 'adui'wakati
Alichofanya ni kwend na flow Tu kadri mama yake Diamond alivyotaka?..
Mtoto wa kiume akifika umri wa miaka 25 unatakiwa uwe kiongozi wa mama yako
Hasa kama Mama mwenyewe ana changamoto za malezi..tabia na elimu kama alivyo Mama yake Diamond....
Haya wanayonfanyia Mzee Abdul ni kumuonea mtu anaehitaji msaada Kwa makosa ambayo sio yake..
Kusaidia Hadi strangers huku mtu aliewahi kukupa matunzo hata kama ni ya siku moja anataabika ni kumjaribu Mungu..karma itawaadhibu..