Diamond anapata wapi kiburi cha kuidharau BASATA na kuimba wimbo uliopigwa marufuku?

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
Kama inavyofahamika kwamba hivi karibuni baraza la sanaa Tanzania (BASATA) liliufungia wimbo wa "Mwanza" ulioimbwa na mwanamuziki Diamond kutokana na maneno ya matusi aliyoyangiza makusudi kwenye wimbo huo..katika kuufungia wimbo huo BASATA walieleza wazi (kama inavyoonyesha barua ambatanishi) kuwa msanii Diamond hatakiwi kuutumia huo wimbo huo tena kwa vyovyote vile na vyombo vya habari pia vilionywa visiutumie kamwe lakini katika hali ya kushangaza jana usiku akiwa jukwaani nchini Kenya aliuimba huo wimbo...Swali je wapi Diamond anapata kiburi cha kutofuata masharti ya BASATA.. Natumai kwa dharau hizi alizoonyesha BASATA watamfungia si chini ya miezi sita kufanya shoo zake tena waanze kesho...
 
Attachments

  • Video_320182856.mp4
    Video_320182856.mp4
    7.3 MB · Views: 59
  • 20181202_211050.jpg
    20181202_211050.jpg
    59.3 KB · Views: 90
  • 20181202_211025.jpg
    20181202_211025.jpg
    76.2 KB · Views: 77
Kwanza huna taarifa sahihi hakuwa nairobi ila thika, alafu huko sio Tanzania ni kenya.
.
Yani anaweza kuimba hiyo nyimbo OPBS ya namanga kenya ambayo ipo mita mia tatu toka OPBS ya Tanzania na asifanywe lolote kwa sababu mamlaka ya basata yapo ndani ya tanzania tu.
.
Hata shilole alivyocheza uchi ulaya hakufanywa lolote zaidi ya mkwara wa kumtishia kinyago mtoto
 
BASATA Na Diamond Nani alikuwa Na Mchango Mkubwa kwenye harakati Za kumpigania Mzalendo wetu namba Moja 2015?

Mwakyembe Mwenyewe alim tuliza Yule Naibu wake alietaka kupimana mbavu Na Naseeb
 
Kwanza huna taarifa sahihi hakuwa nairobi ila thika, alafu huko sio Tanzania ni kenya.
.
Yani anaweza kuimba hiyo nyimbo OPBS ya namanga kenya ambayo ipo mita mia tatu toka OPBS ya Tanzania na asifanywe lolote kwa sababu mamlaka ya basata yapo ndani ya tanzania tu.
.
Hata shilole alivyocheza uchi ulaya hakufanywa lolote zaidi ya mkwara wa kumtishia kinyago mtoto
Siku nyingine usikurupuke kujibu tu thread bila kusoma kwa undani barua ya BASATA haikuwa na mipaka alipigwa marufuku kuutumia popote...hata yeye aliomba msamaha kwa kukili kuwa wimbo una matusi wala hawezi imba mbele ya wazazi wake..hilo linatosha kumchukulia adhabu
 
Mkuu nasikia Leo wabunge wakiongozwa na naibu spika walikuwa wakicheza hiyo nyimbo.
Sasa washitaki na hao wabunge kwa basata.
Fanya ya kwako roho mbaya haisaidii
Issue yao ni tofauti hii ilikuwa ni burundi..aliopiga huo wimbo ndio afanyiwe uchunguzi nani kamsambazia kama ni diamond basi sheria ichukue mkondo wake...
 
Mkuu nashindwa kuiapload hiyo video uwaone wabunge wakiongozwa na naibu spika wanavyocheza hiyo nyimbo
 
Kwanza huna taarifa sahihi hakuwa nairobi ila thika, alafu huko sio Tanzania ni kenya.
.
Yani anaweza kuimba hiyo nyimbo OPBS ya namanga kenya ambayo ipo mita mia tatu toka OPBS ya Tanzania na asifanywe lolote kwa sababu mamlaka ya basata yapo ndani ya tanzania tu.
.
Hata shilole alivyocheza uchi ulaya hakufanywa lolote zaidi ya mkwara wa kumtishia kinyago mtoto
umenikumbisha safar moja nimeenda boda ya tarakea,kuna wahuni wamening'iniza mirungu upande wa Kenya halaf wanaishi bongo yani mtu akitaka wanavuka wanamuuzia anasaga huko huko halaf anaingia bongo yuko safi askari hawana cha kufanya,halikadhalika na pombe hivyo hivyo wamekataza kuuza mchana but mida wote watu wako njwiii kumbe wanaenda kulewea kenya wanarudi ardhi ya TZ washapendeza na askar wanakodoa tu hahahahah
 
😂😂😂😂 hao madingilai hawafai
 
Kwanza huna taarifa sahihi hakuwa nairobi ila thika, alafu huko sio Tanzania ni kenya.
.
Yani anaweza kuimba hiyo nyimbo OPBS ya namanga kenya ambayo ipo mita mia tatu toka OPBS ya Tanzania na asifanywe lolote kwa sababu mamlaka ya basata yapo ndani ya tanzania tu.
.
Hata shilole alivyocheza uchi ulaya hakufanywa lolote zaidi ya mkwara wa kumtishia kinyago mtoto
Ila yale matiti ndala ya shilole umenikumbusha mbali Mkuu...
 
Siku nyingine usikurupuke kujibu tu thread bila kusoma kwa undani barua ya BASATA haikuwa na mipaka alipigwa marufuku kuutumia popote...hata yeye aliomba msamaha kwa kukili kuwa wimbo una matusi wala hawezi imba mbele ya wazazi wake..hilo linatosha kumchukulia adhabu
Tatizo haukubali kueleweshwa kile ulichokiandika chenye mapungufu Makubwa bado unakisimamia.
.
Unajua kwanini baada ya kufungiwa ilifungiwa kuonekana na viewers wa bongo ila kenya na dunia nzima wakaendelea kuitazama?
 
🤣🤣🤣🤣
BASATA HAWANA NGUVU..
LABDA NYUMA YA PAZIA WALIWAAMBIA WAENDELEE BILA KURUSHA TENA BARUA YA HAYO

MIE 🙆‍🙆‍🙆‍
Matusi ni tz tu
Hata nyimbo za nje baadhi zikitafsiriwa kwa kiswahili tutaona Ni matusi
Kijana nje atazipiga Kama kawaida
 
Tatizo haukubali kueleweshwa kile ulichokiandika chenye mapungufu Makubwa bado unakisimamia.
.
Unajua kwanini baada ya kufungiwa ilifungiwa kuonekana na viewers wa bongo ila kenya na dunia nzima wakaendelea kuitazama?
Mkuu huyo anachuki zake binafsi
Hata ukimuelewesha hawezi kukubali
 
Back
Top Bottom