Kama inavyofahamika kwamba hivi karibuni baraza la sanaa Tanzania (BASATA) liliufungia wimbo wa "Mwanza" ulioimbwa na mwanamuziki Diamond kutokana na maneno ya matusi aliyoyangiza makusudi kwenye wimbo huo..katika kuufungia wimbo huo BASATA walieleza wazi (kama inavyoonyesha barua ambatanishi) kuwa msanii Diamond hatakiwi kuutumia huo wimbo huo tena kwa vyovyote vile na vyombo vya habari pia vilionywa visiutumie kamwe lakini katika hali ya kushangaza jana usiku akiwa jukwaani nchini Kenya aliuimba huo wimbo...Swali je wapi Diamond anapata kiburi cha kutofuata masharti ya BASATA.. Natumai kwa dharau hizi alizoonyesha BASATA watamfungia si chini ya miezi sita kufanya shoo zake tena waanze kesho...