BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,327
Moja ya ndoto nyingi za mastaa kibao wa muziki ni kupata nafasi Billboard. Diamod amepata bahati hio baada ya kuandikwa kwenye makala ya mtandao huo wa BILLBOARD.
Katika picha ambayo imewekwa kwenye makala hiyo, Diamond amewekwa pamoja na wasanii wengine wanne kutoka Afrika Magaribi akiwemo Wizkid, Davido na Tiwa Savage.
Kwenye makala hiyo ambayo imewaonyesha wasanii hao inazungumzia juu ya lebo kubwa za muziki duniani zinavyoangazia Afrika kumpata staa ajaye wa Pop duniani.
Hilo limekuja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kampuni ya Universal Music Group ambayo pia inasimamia kazi za Diamond, kupitia tawi lake la nchini Uholanzi ilitangaza kununua hisa asilimia 70 za lebo ya AI Records ya nchini Kenya.
UMG watakuwa wanafanya kazi za kusambaza kazi za wasanii wa Al Records duniani kote ikiwemo kwenye mitandao mikubwa tofauti tofauti ya muziki.
We wish you all haters to have nice day !!