Diamond azindua Pafyum yake ya Chibu, bei yake ni balaa

Diamond azindua Pafyum yake ya Chibu, bei yake ni balaa

Sio kila bidhaa ni ya kila mtu. Tatizo ni Diamond au bei? Mbona watu tunanunua cologne za 150,000 hadi 200,000 bila shida? Tena sio moja. Wapo watakaonunua.
Shida ni diamond na wala sio bei. Kama mtu hawezi iyo bei si aache. Mbona zinanunulika

Uyu dogo atazidi kuumiza watu roho kwakweli.
 
Naiyona kule lipstick za Kiss zilipo
Elimu Elimu Elimu
Mh Lowassa aliona ombwe kubwa sana katikati ya vichwa vya watanzania

Nina mashaka na haya
-Hakuna market survey and research
-Needs and wants assesment
-Marketing test na consumerizatiom
-Standards grade and brand (Hapa kachemka yeye kiumaarufu anaitwa Diamond plutnumz perfume inaitwa chibu hapo ni ugali na mgonjwa haiwezi kufanya vizuri sokoni na ni ndoto )
-Varieties hapa pia kachemka( kila mtumiaji na preference zake sio wote wanahitaji kitu kimoja(uniformity) kwa wakati mmoja wanawake wanapenda harufu flani wanaume pia kila mteja na kada yake, vijana, watu wa umri wa kati, wafanyakazi wa maofisini n.k
Swali wateja wote watanukia harufu sawa??? )
-accessibility ([emoji38] kaziweka GSM Mall pole kaka Nasibu Watu wote wataenda Gsm Mall kuifuata perfume tu kazi kweli kweli)
-Price sio rafiki kwa watu wote(Japokuwa kuna wateja wa perfume za bei ghali kwa sababu wanaafford au for presitige)

I stand to be corrected
Hivi unamfananisha wema sepetu na nassib Abdul? Wema sepetu fans wake ni matusi.com hawako serious kwenye vitu vyake vya maendeleo. Iyo iko wazi na ni tofauti na mashabiki wa Nassib.
Halafu kingine kuhusu kunukia sawa hiyo ni kawaida, mimi nmeshasimamishwa mara kibao kuulizwa natumia perfume gani mtu akanunue. Ingekua kunukia sawa perfume ingekua inatoka moja tu per brand.

Kuhusu elimu, bakhresa ana elimu gani na yuko wapi? Hao wenye maelimu wako wapi?
 
Siyo kwa mtindo huu wa laki moja. Kuna line kubwa kama Dune, Chanel, KC na wengine huwa wanatoa kulingana na uwezo wa mtu wanaanzia hata dollar 10. Wewe unaanza na dollar 50 kwa nchi yetu ya bongo??? Haya yetu macho labda mapushers na ma Godfathers wataweza plus cocochanel siyo sisi makapuku family ingawa tunapenda kumsapoti kijana wetu.
Kitabu kama hukielewi hujaandikiwa wewe.
 
Hivi unamfananisha wema sepetu na nassib Abdul? Wema sepetu fans wake ni matusi.com hawako serious kwenye vitu vyake vya maendeleo. Iyo iko wazi na ni tofauti na mashabiki wa Nassib.
Halafu kingine kuhusu kunukia sawa hiyo ni kawaida, mimi nmeshasimamishwa mara kibao kuulizwa natumia perfume gani mtu akanunue. Ingekua kunukia sawa perfume ingekua inatoka moja tu per brand.

Kuhusu elimu, bakhresa ana elimu gani na yuko wapi? Hao wenye maelimu wako wapi?
Kuna thread ya perfume humu, watu wengi wanatumia issey miyake, creed etc mbona hawasemi watanukia sawa...shida ya wengi humu ni chuki dhidi ya Diamond.
 
Hivi hawa GSM ndio wanamkweza diamond au daimond anawakweza GSM!? Jibu sahihi hapa litatufanya tujue kuwa huyu msanii naye anaangukia kwenye 'bubble popularity'.
Kuwatageti 'wapanda ndege' na wenye uwezo wa kulipia 11k kwa ajili ya perfume ina maana unatergerti watu wenye uelewa na mtu yeyote mwenye uelewa sidhani kama anaweza kuwa sehemu ya 'utanzania' huu!
 
Duh! Angezileta kipindi cha Mkapa au Kakaya, watumiaji wangekuwa wengi.
Hata hivyo wabongo kwa kuchakachua, kesho kutwa utaikuta dukani kwa Mangi Chibu perfume 7000/=
Ngoja nisubirie ya kaka Harmorapa labda nitaimudu.
 
Huyo katumiwa tu coz ni celebrity basi watu wanapiga hela kupitia yeye,,,,japo ni njia nzuri ya kufany promotion lakin kwa bei hiyo apana axeeee,,,ming mnooo
 
6dd87da99c2921b89aa79e2f2b2bc990.jpg

Hivi huyo jamaa mwenye sura kama huyo kinyago cha kimakonde si ni yule anaye angamiza wasanii kwa kuwapa mizigo ya kwenda nayo South? Huyu mtuhumiwa anatumia cologne kweli, maana anaonekana ni mtu wa kunuka makwapa na sehemu nyeti mwilini.
 
Hivi kwann watanzania hatuna utamaduni WA kuacha tusivyovimudu Kwa wenye uwezo nazo Bila malalamiko na majungu?ukiona bei kubwa ujue haikutengenezwa Kwa ajiri yako we piga kimya nunua ya bei unayoimudu maisha yaendelee,kila mfanyabiashara huwa analenga tabaka fulani kulingana na thamani ya bidhaa yake na malengo yake,ye kaipa thamani hiyo bidhaa yake tumuache afanye biashara tusilete uteam Kiba hapa na kumuombea njaa kijana mwenye uthubutu.
 
Hivi ile clothing line yake aliyoanzisha ya WCB inafanyaje sokoni?

Kama ile ameshindwa hivi kweli perfume nani atanunua kwa hiyo bei? Exposure yote aliyonayo pamoja na kwenda ulaya kila siku bado hajui apart from mziki nini kitampatia pesa matokeo yake yeye kila siku kujaribu jaribu tu mambo.. Mara App sijui ya kuuza mziki, huko hajafanikiwa karukia perfume..

Diamond una jina kubwa sana, clothing line sijui maperfume havijawahi kumtoa msanii yeyote mkubwa hata huko duniani. Tafuta biashara ambayo inagusa matumizi ya watu ya siku kwa siku.. Angalia biashara wanazofanya akina Mo na Bakhressa.. Ushauri tu ebu jaribu hata kutengeneza kinywaji chako, iwe Juice au Soda kama za Azam au Mo hapo utatoboa mara moja maana mashabiki wako wengi ni wanafunzi na watoto wa uswazi ambao hawana kipato kikubwa ukilinganisha na hizo bei unazoweka kwenye bidhaa zako.. Na hata biashara ya Juice mteja mmoja anaweza akawa anakunywa Juice yako angalau mara tatu kwa wiki lakini hizo Perfume na nguo anaweza purchase once in a lifetime.. Akina Pdidy na 50 Cent wao wanatajirikia kwenye liquor sasa wewe si mnywaji basi fanya hata Juice hizo au hata Non-Alcoholic drinks..

Demu wako Wema alikuja na biashara gani sijui lakini pamoja na mvuto wake kwa mashabiki wake alifeli, kuwa tofauti usifate mkumbo na usifanye biashara za sifa (kwamba perfume yangu inauzwa ghali).. Hujafikia level za kutengeneza prestigious products maana mashabiki wako ni watu wa hali ya chini..
Loser mind...nahisi hapo ht 10000 mfukoni huna
 
Zari ana akili sana;
amshukuru, angebaki na hawa wabongo angeshangaa.
 
Hivi huyo jamaa mwenye sura kama huyo kinyago cha kimakonde si ni yule anaye angamiza wasanii kwa kuwapa mizigo ya kwenda nayo South? Huyu mtuhumiwa anatumia cologne kweli, maana anaonekana ni mtu wa kunuka makwapa na sehemu nyeti mwilini.
we jamaa umasikini wako unasababisha uwe na chuki
 
Hivi huyo jamaa mwenye sura kama huyo kinyago cha kimakonde si ni yule anaye angamiza wasanii kwa kuwapa mizigo ya kwenda nayo South? Huyu mtuhumiwa anatumia cologne kweli, maana anaonekana ni mtu wa kunuka makwapa na sehemu nyeti mwilini.
Huyo jamaa anaitwa Ruge. Labda na wewe jitaje hapo ili tuwafananishe tuone nani anaweza kuwa mnuka kwapa.
 
Shida ni diamond na wala sio bei. Kama mtu hawezi iyo bei si aache. Mbona zinanunulika

Uyu dogo atazidi kuumiza watu roho kwakweli.
Hivi mtu akiku criticize au akiwa na mtizamo tofauti na wewe/mtu fulani ni kwamba hakupendi/hampendi au anakuchukia/anamchukia huyo mtu??

Ni dhambi kuwa na mawazo mbadala ya jambo/kitu fulani kilichofanywa/kinachofanywa na mtu/watu fulani? Wewe yawezekana hujalalamika sababu hiyo perfume unaweza kuafford lakini hivi angeuza tuseme million 1 au hata 2 na wewe usingetoa povu kama tunavyotoa sie maskini tunaoshindwa hiyo 105,000/-?

And why is it everyone that disagree na huyo bwana Diamond is a hater?
 
Hater ndiye huona kila jambo atakalofanya mtu ni baya. Ata km likiwa jema bado ni baya. Kutoweza ku "afford" kitu haimaanishi ndio ukiponde.

Kama uwezo wako ni tv ya chogo 12' sio kwamba ndio uiponde LG 32' kisa huwezi inunua. Nunua unachoweza sio umlazimishe mtu auze kwa price unayoitaka wewe
 
Una hakika kila aliyelalamika bei hapa ni hater wa huyo Diamond?

Sijui una uelewa gani, lakini kwani kulalamikia bei ni sawa na kuponda bidhaa ya huyo Diamond.. Apart from Mziki, wengine tulihoji ile clothing line yake inafanyaje sokoni? Mbona huku mtaani hatuoni watu wakivaa hizo brand za WCB.
 
Back
Top Bottom