mamaudaku
JF-Expert Member
- Nov 24, 2016
- 706
- 467
Hivi ile clothing line yake aliyoanzisha ya WCB inafanyaje sokoni?
Kama ile ameshindwa hivi kweli perfume nani atanunua kwa hiyo bei? Exposure yote aliyonayo pamoja na kwenda ulaya kila siku bado hajui apart from mziki nini kitampatia pesa matokeo yake yeye kila siku kujaribu jaribu tu mambo.. Mara App sijui ya kuuza mziki, huko hajafanikiwa karukia perfume..
Diamond una jina kubwa sana, clothing line sijui maperfume havijawahi kumtoa msanii yeyote mkubwa hata huko duniani. Tafuta biashara ambayo inagusa matumizi ya watu ya siku kwa siku.. Angalia biashara wanazofanya akina Mo na Bakhressa.. Ushauri tu ebu jaribu hata kutengeneza kinywaji chako, iwe Juice au Soda kama za Azam au Mo hapo utatoboa mara moja maana mashabiki wako wengi ni wanafunzi na watoto wa uswazi ambao hawana kipato kikubwa ukilinganisha na hizo bei unazoweka kwenye bidhaa zako.. Na hata biashara ya Juice mteja mmoja anaweza akawa anakunywa Juice yako angalau mara tatu kwa wiki lakini hizo Perfume na nguo anaweza purchase once in a lifetime.. Akina Pdidy na 50 Cent wao wanatajirikia kwenye liquor sasa wewe si mnywaji basi fanya hata Juice hizo au hata Non-Alcoholic drinks..
Demu wako Wema alikuja na biashara gani sijui lakini pamoja na mvuto wake kwa mashabiki wake alifeli, kuwa tofauti usifate mkumbo na usifanye biashara za sifa (kwamba perfume yangu inauzwa ghali).. Hujafikia level za kutengeneza prestigious products maana mashabiki wako ni watu wa hali ya chini..
Subiri wachafu waje na mapovu umempa ushauri mzuri sana halafu market yake siielewe wewe unataka kuanzisha biashara unatoa wimbo wa kuwatukana watz kweli unaakili halafu week hiyo unatoa biashara tatizo kila kitu wanafikiria ni kiki tu