Diamond haji kuandika mashairi kama haya tena

Diamond haji kuandika mashairi kama haya tena

Kwa kweli lyrics ya ukimwona ni bora sijapata kuona hata nyimbo kwa ujumla haijawahi kunichosha masikio
Lyrics zingine kali zipo kwenye Wimbo wa nataka kulewa!
Diamond wa kipindi kile alikuwa Diamond kweli
Sasa naona kachanganya na Impurities za Platinumz lakni Jamaa ni mkali
 
yaani wasafi sijui huwa wanaimba upuuzi gani.harmonize katoa wimo mzuri ila nenda kwenye mashairi sasa upuuzi mtupu . africa tutabaki nyuma tu
Tatizo la mashairi ni la world wide cku izi wasanii wana base kwny melodi tu mziki umebadilika sio km zamani hata ukickiliza nyimbo za marekani za zamani na sasa utaona tofauti kuanzia RnB hadi Hip hop hamna kitu wamebaki wachache sana ambao bado wanatunga nyimbo za mashairi yakueleweka
 
Nimekuambia Diamond si mwanamuziki.....tofautisha kati ya mwanamuziki na msanii. Unaweza kulinganisha vipaji vya kina Barnaba Boy, Lady Jay Dee, Banana Zorro na Diamond? Hao niliokutajia ni wanamuziki pure lakini si Diamond japo ana jina kubwa pengine shinda ya hao niliokutajia. Kuwa mwanamuziki si lele Mama, kile ni kipaji na kazi ya watu sema tu kuna wengine wanaiga na kufika mbali Zaidi ya wahusika.
Umeona sasa....

Nilikwambia we mbishi ila ujui unabisha nini alafu ukabisha.
 
Huu wimbo ni kati ya nyimbo nisizo zichoka kila nikusikiliza naona mzuri na uwa haukosi kwenye list yangu.
Manecky alimsaidia diamond kuupendezesha zaidi wimbo kwa beat kali maana ina hisia flani kitu ambacho mpaka leo namlaumu diamond ni kugombana na manecky akaacha fanya naye kazi maana kwa nyimbo za hisia manecky ndiko mahara pake.
Pia ile kutoumalizia akaacha chorus ina hang kuliupendezesha zaidi yani it was a blessing in disguise.


Mkuu Diamond alitamka mwenyewe kuwa wameshamaliza tofauti zao na manecky. Pia alikiri kuwa manecky huwa anampatia sana kwenye nyimbo za kubembeleza na kuna vibao tayari ameshaandaa na manecky atavitoa hivi karibuni...
 
mmmmhhhh
Mungu aliumba dunia mapenzi tangu na tangu
yashanipiga sasa sinabudi nielewe
siwezi kung'ang'ania maana sio fungu langu
japo ni shida ila, nitabaki mwenyewe
ohh ila, mpe shukrani kwa kuniumiza suraya
mwambie mi bado mahututi nauguza kidonda changu
na asisikie asilani, mwambie mapenzi mabaya
hata angali hai Kairuki asingetibu gonjwa langu
kutwa nzima moyo unanidunda dunda (dunda)
sina amani nasaga rumba (rumba)
ohh unani dunda
sema chine tembee moyoo
unanidunda dunda (mamii moyooo)
sina amani nasaka rumba (oohh mimii)
ohh unani dunda
eeeeeeehhhhhhhhhh ukimuona
ukimuona ukimuona
ukimuona ukimuona ukimuona
we nenda mwambie marafiki, marafiki wabaya
tena wengi waongo, wala wasimdanganye
oya ni mashoga rafiki, oohh marafiki wabaya
oooohhhh oooohhh mmmmmhhh
tatizo mi bado, nilipoteleza nkakosa sipajui
mpaka akafunga virago, na akaamua kuondoka sitambui
ubaya, kinacho niumiza, maneno neno maneno
mara kwa ndugu rafiki, kwanini anawapa misemo
najaribu papasa, mbona kwa macho ataona chochote
ila ndo kutwa mikasa, na nazidi kuanguka, niokote
kutwa nzima moyo unanidunda dunda (dunda)
sina amani nasaga rumba (rumba)
ohh unani dunda
sema chine tembee moyoo
unanidunda dunda (mamii moyoo)
sina amani nasaga rumba (ooohh mimii)
ohh unani dunda
eeeeeeehhhhhhhhhh ukimuona
ukimuona, ukimuona
ukimuona, ukimuona
ukimuona

Read more: Diamond - Ukimwona Lyrics | MetroLyrics
Kiufupi mimi sio shabiki wa diamond ila kwenye huu wimbo.... Diamond amesimama vilivyo... Yaani hakuna gepu la kufikiria kama diamond wa juzi amesimama na mtumzima.... Heshima kwako Diamond unajua
 
Back
Top Bottom