Diamond hana washauri?


You're very right... Aisee it's hard ukijiweka kwenye position kama hii.. Imagine mwanamke amehangaika toka akiwa mjamzito peke yake leo eti mtoto ame fanikiwa ndio awe wa maana!!!
 

What if the child died? Mimi huwa naona kuwa muda mtu anapohitaji baba kuliko kipindi chochote kile ni wakati wa utoto.. Sasa kama hakumfaa utotoni Sasa kuna mantiki gani ya kuwa na baba?
 
mimi namchukulia huyu mondi kam wapenda sifa wengine waliopita...siku zote mzazi akosei...mondi kalewa misifa anayoipata kwenye mitandao ila akae akumbuke kuwa huwezi kuwa bingwa milele siku moja utashuka ili apande mwingine...mafanikio ni kama gari la abiria...kila mtu atapanda...wako wapi wakina mr.nice (mzee wa kuku kapanda basikel) yuko wapi tid (mzee wa zeze) wote walipanda gari la mafanikio wakalewa umaarufu wakafanya mambo ya kijinga mwisho waka zima kama taa...joks maana ya mond hayanihusu
 
What if the child died? Mimi huwa naona kuwa muda mtu anapohitaji baba kuliko kipindi chochote kile ni wakati wa utoto.. Sasa kama hakumfaa utotoni Sasa kuna mantiki gani ya kuwa na baba?
Wababa wa hivi wanatia hasira yeye anavomuhitaji diamond sahivi Ndivo hivo diamond alimuhitaji kipindi hicho hayupo.... Mzee atulie tu ndo kishalamba garasa
 
Je alizaliwa ndani ya ndoa au nje ya ndoa....!?? Alimuhudumia kipindi cha malezi....???
 
Kila mwanaume anatakiwa ajifunze ujifunze kupitia baba Diamond kuwa kutelekeza watoto hailipi hata siku moja. Wapendeni watoto wenu hata ama umeachana na mama yake but hakikisha kuwa unaelea watoto wako. Iko neno la Mungu linasema kuwa Jiwe walilolikataa Waashi litakuwa jiwe kuu la pembeni siku moja. Kwa misingi hii unamkataa mtoto halafu mama anateseka naye anakuwa na say kusoma au kufanikiwa katika maisha halafu unajitokeza. Kafie mbali kabisa.
 
Vipi Quran inasemaje kuhusu kumtelekeza mtoto?
 
Mm huwa najiuliza hivi bahati mbaya huyu baba yake anafariki (Mungu aepushie mbali) HIVI HUYU KIJANA DIAMOND ATAKWENDA MSIBANI???? Hivi huwa hajiulizi? ?? Atakua lini???
NA ASIPOKWENDA ATAJENGA LEGACY GANI KWA KAZI ZAKE???? Yani ndo maana watu husema pesa ni kama mvua inayo nyesha popote hata kwny kinyesi....huyu KIJANA kutembea kwake na pesa alizonazo hazijamsaidia lolote kukua kiakili...na kama mama yake ndo anamsonga hivyo achunguze sana huo msimamo...napita tu
 
Ivi huyo Mzee ana Mtoto Mmoja tu? Kwanini anae pewa lawama ni 'Dimond' tu?
Kabla ya kupost jiulize kwanza kisha upost, usikurupuke hao ndugu zake umewahi kuwasikia?na je hali zao kimaisha zikoje? Usiteteee ujinga hivi anwezaje kutoa m3 kwenye birthday ya rafiki akashindwa kutoa laki mbili Kwa ajili ya matibabu ya baba take ambaye alikatika mpaka akatokea yeye?
" Baba na mama ni Mungu wako wa hapana duniani"
 
Nipe tano
 
mtoa mada mbona ameandika wajibu wa mtoto kwa baba pekee yake, alitakiwa aandike pia wajibu wa mzazi kwa mtoto ili kubalance story, na kukote vifungu vya aya

Umenena sawa kabisa, vifungu vyote alivyoandika ni vya wajibu wa mtoto kwa wazazi lakini hakuna kifungu cha wajibu wa wazazi kwa mtoto.

Kwa asilimia kubwa ikiwa wazazi watakushughulikia ipasavyo na wewe mtoto unapata upendo wa kuwashughulia vyema uzeeni kwao.

Mibaba mingine ikishazalisha haijui hata kumsalimia mtoto na unakuta ni mama ndiyo anahangaika peke yake, lakini mtoto akishapata kazi nzuri ndiyo bingwa wa kulaumu hashughulikiwi.
 
Wababa wa hivi wanatia hasira yeye anavomuhitaji diamond sahivi Ndivo hivo diamond alimuhitaji kipindi hicho hayupo.... Mzee atulie tu ndo kishalamba garasa
Atulie dawa imuingiee....kumbe aliuza nyumba kariakoo hela akakatia viuno leo anataka msaada kupitia waandishi makanjanja......aende kwa aliokula nao maisha wamsitiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…