Diamond hana washauri?

Diamond hana washauri?

Kwa hili diamond hapana jaribu kuwa na utu.. Huyo baba yako akifa ndio utamkumbuka?

Una uhakika huyo ni baba yake kweli? Diamond ni mtu anaejitambua, anaelewa Diamond kaambiwa nini na mama yake kuhusu huyo mzee?
 
Mama kashamwambia Diamond huyo sio baba yake mzazi. Huu ndio ukweli .
 
mkuu umeenda nje sana ya mada,mzazi hakosei? kuna wazazi wanawabaka binti zao,je na wao hawakosei? sema mkuu umeongea mengi ya moyoni ambayo ni OP ndo tatzo.
mzazi hakosei...unamaanisha mzazi akupigie magoti akuombe msamaha..? angeamua kuwithdrow je...
 
Je alizaliwa ndani ya ndoa au nje ya ndoa....!?? Alimuhudumia kipindi cha malezi....???
Alizalia nje ya ndoa na mzazi wake wa kiume hajamhudumia kwa lolote alijua kumpa mimba huyo mama ndio akazaliwa Nasseb baada ya hapi hakuwa na msaada kwa lolote
 
Alizalia nje ya ndoa na mzazi wake wa kiume hajamhudumia kwa lolote alijua kumpa mimba huyo mama ndio akazaliwa Nasseb baada ya hapi hakuwa na msaada kwa lolote
Duh..! Umeongea kama Mama Nasseb kabisa.
 
Una uhakika huyo ni baba yake kweli? Diamond ni mtu anaejitambua, anaelewa Diamond kaambiwa nini na mama yake kuhusu huyo mzee?
Ni baba yake mbona wamefanana? Hata jina analotumia ni la huyo mzee
 
Katika hili la mzazi wake wa kiume mimi binafsi limenigusa hasa kwa imani yangu ya dini. Siwezi kuhukumu moja kwa moja kwa maana sijui chanzo cha ugomvi wao wala status yao kwa sasa na pia MIMI SI HAKIMU, lakini nina haki ya kutoa maoni yangu hasa kumsaidia pia diamond ajitambue.

Katika hali ya kawaidia inatakiwa ingekuwa rahisi kama mzazi wako anapata msaada wako by then kila siku awe analalamika au tunamuona kwenye mitandao huo tayar ni udhaifu wako wewe mtoto kwa kuruhusu mzazi wako awe anakutia aibu wewe au familia yenu kwa ujumla. Kwa namna yoyote ni lazima suala la wazazi wako ukalipa umuhimu mkubwa sana katika maisha yako.

Katika mafundisho ya dini yanatufunza nini kuhusu wazazi?

Hakika ametakasika yule ambaye amewajibisha na kuamrisha wema na kutimiza haqqi na kuiegemeza kwa kila anaestahiki na akawajibisha haki kwa wazazi wawili, na ikawa ni amri iliyoenea kwa walimwengu wote. Hakika ameamrisha ALLAH tabaaraka wata’la katika aya nyingi kuwafanyia wema na ihsani wazazi wawili.
Mfano wa kauli yake aliposema:

{وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلاَهُمَا فَلاَ تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلاَ تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلاً كَرِيماً* وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيراً}
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.


Akaamrisha ALLAH tabaaraka wata’la ihsani kwa wazazi wawili katika namna zote za wema, nao ni katika kauli [unapozungumza nao] pale aliposema [basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima]. Vivyo hivyo kuwafanyia wema katika matendo; kimwili na kimali kwa kauli yake aliposema: (Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma).
Na akanyanyua ubora wanapofika katika hali ya uzee, kisha akakataza kuwavunjia adabu na kuwatusi, achilia mbali kuwaacha wakiteseka.

UWAJIBU WA KUWAFANYIA WEMA WAZAZI WAWILI:

Hakika ameamrisha Allah tabaaraka wata’la, na akawajibisha kwa njia ya wasia kuwafanyia wema wazazi wawili katika aya nyingi za qur’an. Pale ilipokuja amri ya wazi juu ya kuwatii, aliposema:
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَاناً
Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake wawili[1]


Ikaonesha wazi kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ni jambo la wajibu kwa kuwa ni wasia wa Allah kwetu. Bali akaliambatanisha jambo hilo la kuwafanyia wema wazazi wawili na twaa’ yake Allah tabaaraka wata’la pale aliposema:

وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mola wako mlezi ameamrisha kuwa msimuabudie yeyote isipokuwa yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema.[2]


Na kauli yake aliposema:
وَاعْبُدُواْ اللّهَ وَلاَ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئاً وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mwabudieni Allah wala msimshirikishe na chochote, na muwafanyie wema wazazi wawili.[3]


Zikakusanya aya mbili hizi kuwa kufanyiwa wema wazazi wawili ni haqqi yao, bali akaifafanya haki hiyo kuwa ni ya pili baada ya tawheed yake Allah tabaaraka wata’la akionesha ukubwa wa jambo hilo [la kuwafanyia wema].

Amesema Al qurtwubiy [Allah amrehemu], kauli ya Allah “Na wazazi wawili kuwafanyia wema [ihsani]” maana yake ni:
برهما وحفظهما وصيانتهما وامتثال أوامرهما

Kuwafanyia wema na kuwahifadhi, kuwatunza na kutekeleza amri zao.


Katika kulisisitiza hilo, mpaka ikawa [wema kwa wazazi wawili] ni wenye kutangulizwa mbele hata kabla ya Sunnah za kujitolea kama vile Sunnah za kabla ya swala nk. Na kwa hili akaweka imamu muslim [Allah amrehemu] mlango katika swahih yake akiuita:
باب تقديم بر الوالدين على التطوع بالصلاة وغيرها

By the way mimi nimekubusha tu. Kama ni kweli mzazi hapati msaada basi ajitahidi kumsamehe, kama anapata msaada ila ndio umaarufu basi Diamond anisemehe maana binadamu tumeumbwa kukOsea. Na huu ni mwezi wa toba hakika atakuwa amenisamehe.

Asante.
Umetoa Aya nyingi ili kuhalalisha Maelezo yko Je Umefatilia kujua Huyo mzee Diamond ni mtt wa ndoa au Alizini?
Kama ni mtt wa zinaa anahusikaje na Aya za mola?.. Mtt wa nje ya ndoa c ni mali ya Mama?
 
Mtu anaenda kwa daktari na mikamera!

Anaumwa kweli huyo?

Mtu anaenda kwa daktari na mikamera!

Anaumwa kweli huyo?



ahahahaha, haumwi huyo..halafu alijua diamond atakua hakui dizaini aliona huyu ni mtoto tu hata nikiwa nae karibu atanisaidiai nini...wazazi jamani hii iwe fundisho hasa wakina baba mnaotelekeza watoto sijui kwa nini mungu uwa nawabariki kwa kiasi kikubwa saa watoto waliotelekezwa na baba zao
 
Back
Top Bottom