Diamond hawa ndio wabongo, chukua ushauri wangu

matumbo

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
7,224
Reaction score
3,951
Kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusu Diamond haswa kipindi hiki akionyesha mafanikio makubwa kimuziki.

Wakati yeye akipambana kupiga hatua kuna wanaopambana kuakikisha hasogei na anarudi chini.

Mimi nimejitolea kumpa ushauri wa bureeee kabisa akiwa kama mdogo wangu.

Ukiangalia kelele zote na matukio ya hivi karibuni utagundua hakuna ishu ya maana sana ya kumchukia diamond ila ni roho mbaya zetu waswahili...Diamond kafanikiwa sana kuna watu linawauma ili jambo yani inawauma inawauma ata wangepata nafasi ya kumuwekea sumu wangemlisha ..Jamani hakuna mtu mbaya dunia hii kama mswahili ndio maana mimi uwa sipendi kuwa karibu na mtu mswahilimswahili,nchi haiendelei sababu ya roho mbaya za kiswahili.

Mswahili anaweza kukuchukia ata hakikosa sababu ya kukuchukia na yote hii sababu ya roho mbaya unakuta mtu ana roho mbaya mpaka akicheka kuna taswira inatokea kama analia vile.

Tukifanya leo tafiti lazima tutakuta asilimia 98 ya waswahili either ni wachawi au wana tabia zote za kichawi.mbongo yupo tayari kuchoma nauli hapa mpaka nachingwea ili akakuroge kisa umenunua gari mpya, ukimpa challenge anunue la kwake atakwambia ye hapendi makuu ila atakuchukia wewe ulieamua kupenda vya kwako

Mbongo atakuchukia ata kwa kumzidi kuvaa vizuri, awezi kujipanga nae atoke smart kukuzidi ila atataka muwe wote wachafu... We ukitaka kumpima mswahili imani mkute anakula alafu akukaribishe msosi na wewe ukaribie utaona uso unavyombadilika na roho yake mbaya.

Mtu anaibuka uko alipoibuka anakwambia dogo ana dharau siku hizi, lakini ukitafakari vizuri hapa tafsiri ya neno dharau ni mafanikio....yaani tatizo dogo ana mafanikio siku hizi.

Wabongo tuna roho za kwa nini ndio maana hatuendelei kamwe, sijui tulitoa wapi hizi roho ama ni ule ujamaa ulituaribu au vipi ! ila kama ni ujamaa wenzetu China mbona wanatumia ujamaa kumfanyia roho mbaya mtu anayerudisha nyuma maendeleo ndio maana ukilisha watu drugs wanakunyonga.....sisi wabongo ujamaa wetu tunatumia kuwafanyia roho mbaya wanaopiga hatua mbele. Yani kwetu mtu akipiga hatua anafanya makosa.

So dogo diamond mimi nakushauri utulie ufanye mambo yako kimpango wako wavumilie tu awa waswahili, ila ishi nao kiakili sana. Jiamini fanya kazi nzuri zaidi watachoka tu na watakubali matokeo.

Watu wanatengeneza maneno kisha wanayapenyeza kwenye media ili kukuharibia, leo mtu anakuja na maneno eti umedharau hotel za mbeya ukimuuliza hizi kauli ulizitoa wapi hana cha kusema, kama umelala hotel za Kigoma utadharau vipi hotel za Mbeya? majuzi hapa umepiga show Tunduma inamaana huko sio Mbeya?

Unakuta mpaka radio zinaingia kwenye ujinga huu unamuuliza mtu swali akitoa majibu, mnayarusha majibu bila swali kisha mnasema haya maneno Diamond kayasema kwa Kiba. Yote ni kufitinisha tu.

Imefikia kipindi watu wanachukia mpaka wanazomea, lakini sio ishu mtu ashushwi kwa kuzomewa ingekuwa ni hivyo Chege na Temba wangeshapotea zamani maana walishapigwa mpaka makopo stejini enzi za Wanaume family na Halisi..Leo halisi wako wapi? Ata AY anayeheshimika sana kwa sasa ameshazomewa na kupigwa makopo enzi za East coast vs Temeke.

Pia chukua tahadhari na Kiba, Kiba wa sasa anamtumia diamond kupata kurudi kimuziki kiukweli bila Diamond hakuna Kiba kwa sasa but kuna Diamond bila Kiba...Kiba kwa sasa hawezi kusimama kwa kazi zake ila kwa jina la Diamond tu.

Tangu Kiba arudi kazi yake ni kuzunguka kwenye media kueleza ubaya wa Diamond, media zote kuanzia radio mpaka Tv amezimaliza akionyesha wewe ni mbaya.

Mimi nakushauri achana na kiba wewe concentrate na muziki wako kwanza mfanye kama haexist vile.

Hakuna ataekuwa juu milele ila hatushushani kwa style ya kampeni, nature ndio uwa inaamua. Muda wa mtu ukiisha haitaitajika nguvu yoyote hatutaanza kumuona kwenye headlines, hatutaskia nyimbo nzuri n.k nature itaamua.

Siku zote ridhki anayegawa ni Mungu tu hakuna binadamu anayeweza kunyang'anya ridhki ya mtu. Mungu ndio anajua nani ampe nini ndio maana yule anapewa sauti nzuri wewe ukapewa nyota. nyota ikiwaka sio rahisi kuizima ndio maana yote yaliyotokea watu wanazungumzia Diamond tu sio nani kafunika wala nini habari bado ni wewe .

Zidane alikuwa bonge la mchezaji lakini matangazo mengi na project za hela alizibeba Beckam ndio ridhki iyo kila mtu na yake.

Nakushauri fanya kazi kwa juhudi zote wataelewa tu, tena kwa sasa ndio uzidishe mara mia hasikuvunje mtu moyo bongo fleva bado inakuhitaji mno. na mashabiki wako wamezidi kukupenda amini usiamini.

Kuna wataokupenda ukifa kama Kanumba na Amina chifupa
 
Uswahili hauwezi ishaaaa,watu wanaongeaa weeeee utadhani wanalipwa mshahara,Tanzania bila Uswahili haiendiii wengine wanajiita wasomi lakini waswahili, wanafiki,wachawiii,lakini mwisho wa siku wataongeaaa weee na watalalaaa
Wivu unatusumbua wabongo sanaaa yaan hata kwa kitu kidogo mtu anaumiaaa ndio ilivyo kwa Diamond, Ally kiba kapata kiki baada ya bifu na diamond na hiyo kuzomewaaa mbona kina Fetty waliandaa mazingira muda ule wanamsifia kiba na kusema team kiba mpooooo huo ni uchonganishiiii ,kiba alikuwepo toka zamanii kuzubaa kwake ndio kumemfanya hivyooo,Akichangamka atafika alipofika Diamond kama kuitwa kushindania tuzo, Diamond hawez kukata tamaaa,mi ningemshaurii asihudhurie hayo mafiesta yao kabisaaa afanye kama Lady jide alivyofanya basiii
(Nimeandika navyojisikia staki kubishana na mtu,toa maoni yako bila kubishana na kila mtu aandike anachojisikiaaa sio)
 
Nakushauri, ukishakula na ukiwa hauna stress za maisha njoo usome tena utaelewa tu.
matumbo katika wadau wa jf ambao wako juu kwa amsha amsha, wewe ni nambari wani yaani ayena ayena. Sasa nikuulize swali moja tu, hivi kuna msanii hapa Tanzania ambaye amewahi au anaenda nchi za nje mara kwa mara kufanya show bila unga wa ... kupakiwa katika safari zake za huko nje ya Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
hujajibu swali, masanja anayo hela zaidi yao mbona hachukiwi????????/ na kipindi diamond alikuwa anashangaliwa alikuwa na maisha mabovu?

Jibu lake unaloo hebu Masanja aanze kushindanishwa na mtu yeyote maarufu lazima yamkute hayo ya kuchukiwa na kuzomewaaa,kwanza huwezi kupendwa na watu wote hiyo haipooo
 
ulikua kwenye akili yangu matumbo
wabongo ndo tulivyo mi binafsi diamond sijaanza kumkataa leo toka nenda kamwambie home kote walikua wanampenda kasoro mie
napenda nyimbo zake mbili tu"nataka kulewa" na ntarejea baas
mi simkubali hata aimbe na marc anthony kwangu mi wa kawaida sanaaaaaaaa
sio nyota yangu binafsi ila nampongeza kwa juhudi zake kimuziki
ananikera show off zake na uongo uongo kuna kipindi 2yrs back nlikua nataka niingie kwenye boti yake si akaanza tena maisha ya location baas ndo nshamdiss
binafs mi sio mshabiki wake ila kila la heri ktk mziki wake
na juzi kankera alivyosema eti anaweza msaidia kiba
si kauli nzuri kiukweli
na hizo kazi mashabiki ndo wanaamua iwe nbaya au nzuri cha msingi awe yule wa mwanzo
wabongo hatupendi maisha ya "location"
 
Jibu lake unaloo hebu Masanja aanze kushindanishwa na mtu yeyote maarufu lazima yamkute hayo ya kuchukiwa na kuzomewaaa,kwanza huwezi kupendwa na watu wote hiyo haipooo

Mbona Jide hajashushwa? Ana hela kuliko Nassib, ana tuzo nyingi kuliko Nassib.
Ana gari la thamani kuliko Nassib. Ukweli ni kwamba hakuna msanii atakuwa juu miaka yote.
Mwambieni ukweli Nassib kuwa wakati huu anapaswa kujaribu kubadilika kimuziki ili kubaki juu, kwani mashabiki wake mmebaki wachache na ndio maana kelele zenu hazikutosha kwenye Fiesta.
Mficha maradhi mauti humfichua. Mwambieni ukweli.
Ova
 
matumbo! iv mbeya ni hakuna hotel yeny hadh ambayo diamond anaweza kulala? sas kwa dharau km izo ndo wa2 wanaanza kumchukia.
 
Miluzi mingi lazima mbwa apotee naona umu ndani tu kutakua na thread kibao za ushauri plus comments,ila nadhani dogo ana matatizo yake haiwezekeni over blue colour aanze kuzomewa kwa kigezo cha mafanikio yake maana utadhani kipato chake kimepanda juzi.
Ivi uyu watu wake si waliandamana kumpokea air -port hapa juzi akiwa na mafanikio iweje leo wamgeuke lazima kuna button dogo kaibonyeza ambayo sio sahihi na akileta utani atakua historia.
 
Bahadhi ya wabongo,sijui hizi roho za kishetani wanatoa wap?full ujuma,usuuda,uongo na umbeya ukifanikiwa tuuuh.
 

Kila mwaka hua wanasema domo huu mwake wa kushuka lakini dogo anapanda tu,kwan kuzomewa kaanza yeyee kwan hadi Chriss Brown huzomewa seuse Dai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…