Diamond hivi huyu Mzee ni baba yako kweli? Mama anasemaje?

Halafu ujue yule Mzee hajalalamika.
Kuna watu tunaamini kulipa kisasi ni alama ya udhaifu.Na hasa kama unalipa kwa mtu asiyeweza kujitetea.

Siamini kama Diamond anaona furaha sana akisikia mzazi wake anasaidiwa na watu baki wasio na uwezo.Ninadhani ili furaha yake iwe ya kweli,amsaidie baba yake hata kama hajamsamehe.

Hiyo spirit haitoi funzo kwa mtu yeyote!Mimi nilinyimwa pia pesa ya shule.Ila mzazi wangu nilimsamehe kitambo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa upande mmoja ni funzo kwa wanaotelekeza watoto kwa upande wa pili, Queen Darlin mtoto wa huyo baba dada yae diamond, alisema baba yao wanamjua na ela si kwamba hapewi anapewa ila inaelekea mzee anataka awe level moja ana mama yake diamond ni kitu ambacho hakiwezekani, they have no chemistry alidhike na anachopewa tu
 
Ngoma ya mzee ya dudu la yuyu ilipata viewers wangapi?
 
Misukule ya Diamond hamkosekani kutetea kila kitu hata kama ni cha kipumbavu


Sio hivyo mkuu, niko na mchizi wangu damdam lakini akikusimulia historia ya maisha yake inasikitisha sana. Jamaaa alitelekezwa na wazazi wote wawili, akakua maisha ya kuungaunga ya kichokoraa. Sasa hivi yuko njema vibaya vibaya, watu walewale waliomtelekeza wanamletea gozigozi.
Mwenyewe anasema hajisikii kitu chochote kuhusu hao jamaa. Ile feeling ya mzazi haipo kabisa, anawaona watu tu. Haya mambo myasikie tu
 
Kama anauwezo awasaidie kama watu tu wakawaida..
 
Pesa Ni zake jamani ,na nyie tafuteni zenu
Ushauri wa Nini, kwani unadhani yeye haoni hayo maisha anayopitia baba yake
 
Amehojiwa na TV ya Carry Mastory? Inabidi atulie dawa imuingie, mnavyotelekeza watoto malipo ni hapa hapa, nyau nyie. Mpo wengi tu, hata humu JF.
Usiwe mpuuzi,jambo limeshatokea uwezi rudisha siku nyuma,samehe sahau wacha maisha yaendelee,kumsamehe mzee wako ni thawabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mondi akumbuke kuwa hata kitendo cha Mzee kumchagua Mama yake na akazaliwa yeye ni juhudi tosha na anahitaji tuzo.

Huwezi jua Mzee alimsotea Mama kiasi gani, labda alikuwa anatembea kwa miguu zaidi ya kilomita 15, au alishindia muhogo na maji ili Mama (enzi hizo totos) apate pesa aliyoomba ya kusuka n.k.

Mzee asingefanikisha Mondi asingekuwepo, Mama angekutana na Mwingine na kuzaa wengine, na vivyo hivyo Dingi naye angekutana na 'bebii' mwingine na kuzaa wengine.
 
mmmh hzo billion walizopewa na tgo walifanya nn..?
 
Wanae pia wanalelewa na mama zao.
Huwezi jua nafasi anayopewa baba katika malezi ipoje.

Pengine; ndio aina ya maisha aliyochagua.
Ni vema kumuunga mkono katika kazi zake, kumsamehe baba yake ni uamuzi wake.

Tuache kutelekeza watoto (au abortion), maana huwezi jua kesho yake.
Satan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…