Ndio nimekutana na title moja mtandaoni ikisema "hata Bakhresa hana Baunsa", possibly hapa wanapondwa kina Diamond wenye mabouncer.
Mimi nionavyo hii ishu ya mabaunsa ni sehemu ya Sanaa ya Msanii husika zaidi kuliko ulinzi, at least Watu mnapata cha kuwaongelea kutwa kucha.
Sasa cha ajabu Msanii anaye struggle na sanaa yake, na huenda benki ana sh 5,000,000, tena ni kwa kipindi hiki wanachokiita cha 'msimu' ili hali huyo anayepondwa kwa sanaa yake ya Mabaunsa ana zaidi ya bilioni moja...
Hivi Bakhresa na Diamond wana mfanano gani? shughuli wanazofanya haziwiani hata kwa nukta...hivi ni Watu wangapi wanamjua Bakhresa? Bakhresa jina lake ndio maarufu kuliko yeye mwenyewe, leo hii Bakhresa akikatiza viunga vya jiji la Arusha bila kutambulishwa na Mtu hakuna Mtu yeyote atakayeshtuka...vivyo hivyo akienda Iringa, Songea, Rukwa n.k.
Kila Msanii afanye sanaa yake, pale atakapofanikiwa na kuwa gumzo mjini basi ndio atoke mbele atuambie "hivi nifanyavyo mimi ndio sawa, nyie wengine acheni hayo nifuateni mimi mtafanikiwa".