Diamond jitathmini upya! ‘kokoro’ imekuvua nguo mshkaji wangu

Diamond jitathmini upya! ‘kokoro’ imekuvua nguo mshkaji wangu

Eti % 70 ya wimbo watu wako uchi unaujua uchi kweli ww kuna kipi kigeni mtu hajawahi kukiona kama ni matiti mbona watu wanayatoa hadharani kabisa kunyonyesha sio kwamba nakupinga ila sioni maana
 
Mimi mwenyewe nimekuwa discouraged na video ile. Atambue kuwa ana fan base kubwa. Yeye kama moja wa maicon kwenye muziki wetu hakutakiwa kuruhusu video chafu vile itoke achilia mbali kushiriki.
Mnajadili upumbavu diamond hafanyi mziki kwajili yako na mleta Uzi.unasema video chafu Ni chafu kipande kipi kwa mfano?
 
video ni kweli huwezi kuangalia na watoto! Ila wakati mwingine analenga soko la mbele bwana unabaki bongo tu ndio yale fiesta ikipita unasubiri fiesta nyingine ndio upate show kubwa!
Kwani salome mbona inapigwa mpaka maharusini ,kwani wanajua kusimamia kama kangaroo maana yake nini? Ibane.
........
ale kokoro babiiiii.......nifinyie kwa ndani

ha haaa haaaa go chibu go
Asante
 
Hivi muogo wa jang'ombe ushawahi kuusikia, au ule mkunaji na mkunwaji huona raha ni nani na hizi nyimbo za miaka hiyo za bi kidude na Shakira lkn kwenye zilipendwa tunazisikiliza, enzi hizo tena Kuna maadili ya kutosha au kwa sababu kafanya Diamond, ujue kama mtu HUMPENDI SEMA SIMPENDI, sio UNAZUNGUKA KAMA DAWA YA MBU YA KUCHOMA mara hoo namkubali mara hoo amenikela. Alafu hujui ule wimbo sio wa WCB ule wimbo ni mali ya mavoko diamond kashirikishwa, leo na kesho hata mavoko akiondoka WCB, wimbo unabaki kuwa mali yake.
 
Hivi KOKORO ni wimbo wa Nani kwani? Maana sielewi Elewi kinacho zungumzwa! Hivi Diamond ana wimbo unao itwa Kokoro? Tukijua hilo ndo tuendelee na Mjadala
 
Issue hapa ni soko lenye kukuingizia pesa nyingi lipo wapi, jamaa ametarget soko la nje na hakuna namna utatoboa kwenye soko la nje kama hujajitoa ufahamu,lazima uwe willing kufanya what you never thought you will do. Jamaa yupo sawa
 
Hakuna msanii bongo aliyekuwa akiimba matusi kwny nyimbo zake kama ngwair lakini cjawai kusikia mtu akilalamika kuhusu hizo nyimbo na humu utakuta wanazisifu tuacheni unafiki domo kila akifanya kitu lazima mtoe maneno ya shombo mmeshatuchosha shabikieni wanaoimba nyimbo za kuelimisha
 
Siku nyingine ukiwa unafanya Uandishi jaribu kuzingatia baadhi ya fact... yeah thread yako nimeipenda inaonekana unamfatilia sana chibu...

naomba niku jibu pasipo kuwa na Ushabiki nimependa sana jinsi ulivyo tiririka hapo juu kuhusu Chibu

But Nyimbo ya Kokoro sio ya Diamomd na mwenye Haki miliki ni rich mavoko. na wala sio diamond jaribu kutofautisha hilo.

Tatu tumekuwa tukisikia kitenge ambacho kinaitwa basata hawa watu wamekuwa wakifatilia vizuri sana

sheria na kanuni za kutokuvunjwa kwa maadil kwa kupitia wasani Unataka kuniambia huu wimbo hawajauiskia

Au hawamjui diamond... nakumbuka Chura ya snura Aikupita wiki... ikala block mpaka pale alipo badili video

Nay wa mitego Akumaliza hata mzunguko wa wiki yKe ya pili Akala block kuhusiana na Pale kati patamu.

shilole nae baada ya kufanya majanga kwenye nchi za watu. baada ya miez kazaa Alikula block

swali langu ni je!? wew una nafasi gani basata ili ulifanyie mchakato sasa hiv na kiukwel nitakuunga mkono.

Je basata ipo au haipo!!? kama ipo je Haimuoni Rich mavoko!?

KOKORO SIO NYIMBO YA DIAMOND
 
Umeandika insha ndeeeeefuuuu nasoma nikajua nitakutana na point walau moja ila mpaka nafika sentesi ya mwisho hakuna hata kijipoint kimoja..

Hata kukujibu nasikia uvivu kwasababu unaonekana hujui mziki, hujui industry ya mziki, hujui biashara ya muziki, hujui strategies za muziki na hujui hata lengo la hiyo nyimbo ni nini.!!

Jifunze hayo hapo juu kwanza ndio uanze kuandika hizi insha!
 
WCB na mashabiki wao wooote ni kipofu na mkongojo wake hawawezi kukubaki ukweli lakini hakuna anayethubutu kuangalia video hiyo na mzazi wake japo humu wanatetea puuuumbav
 
copied somewhere

NA HASSAN DAUDI

HUENDA ujumbe wangu huu kwa mwanamuziki anayeitesa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, ukawakera wengi na hata yeye mwenyewe.

Lakini, nimejiridhisha kuwa ninachotaka kukizungumzia hapa ni kwa masilahi yake, jamii inayomzunguka na soko la muziki kwa ujumla.

Kwa maana nyingine, kwa kuwa lengo langu si kubomoa bali ni kujenga, natamani kuona ‘message’ yangu hii ikiachwa huru kwa kutopewa tafsiri zitakazojenga chuki kati yangu na supastaa huyo.

Naamini Watanzania wa sasa wana uelewa wa kiwango cha juu kuliko miaka kadhaa iliyopita.

Kwa maana hiyo, sina shaka kuwa ujumbe huu utabaki kuwa sehemu ya mchango wangu kwenye soko la muziki na si vinginevyo.

Jina alilopewa na wazazi wake la Nasib Abdul si maarufu sana miongoni mwa mashabiki wa muziki hapa nchini.

Ni tofauti na utakapomwita Diamond ‘Paltinum’, ambapo hata mtoto mdogo atakwambia mambo mengi yanayomhusu staa huyo na kukuimbia moja ya ngoma zake.

Nikiri kuwa napenda anavyoishi kistaa na zaidi ni jinsi anavyojua mbinu za soko ikiwamo kutafuta ‘attention’ kutoka kwa mashabiki wake. Anaishi dunia ya kisasa zaidi.

Kwa hapa Bongo, unapotaja wakali wa Bongo Fleva, huwezi kuliweka kando jina lake hata kwa bahati mbaya.

Mbali na sauti nyororo, tungo na swaga zake, ubunifu ni miongoni mwa silaha zilizomwezesha Diamond kuteka hisia za mashabiki wa burudani.

Kwa sasa anatajwa kuwa mmoja kati ya wasaniii maarufu na wanaokubalika zaidi barani Afrika.

Wakati Nigeria ikijivunia Wizkid, Davido, D’banj, Flavour na wengineo kwenye tuzo mbalimbali, Diamond ameonekana kuwatosha kabisa akiwa peke yake. Ni wazi Tanzania inajivunia kuwa na staa huyo.

Kwa kipindi kifupi tangu alipotoka na ‘Kamwambie’, miaka isiyozidi 15, tayari nyota huyo ameliletea Taifa letu sifa kibao. Ameshinda tuzo nyingi zinazoandaliwa ndani hata zile za ng’ambo.

Haimaanishi nawapuuza wasanii wengine akiwamo mpinzani wake, Ali Kiba, la hasha! Ila hatuwezi kuukataa ukweli kuwa Diamond ameleta mapinduzi makubwa kwenye soko la muziki. Hakuna anayeweza kumnyima ujiko huo.

Hata hivyo, bado nina shaka kuwa Diamond hajatambua thamani yake kwa Watanzania.

Kinachonifanya niamini hivyo ni wimbo mpya uliotoka wiki chache zilizopita ambao ameshirikiana na swahiba wake, Rich Mavoko.

Binafsi niliposikia taarifa za ujio kibao hicho kinachokwenda kwa jina la ‘Kokoro’, nilitamani sana kupata bahati ya kuusikiliza na hata kuitazama video yake.

Shauku hiyo ilitokana na kutambua uwezo mkubwa walionao wanamuziki hao, hasa Diamond ambaye ndiye mwenye Bongo Fleva yake kwa sasa akisaidiana na Ali Kiba.

Nikiri wazi kuwa baada ya ngoma hiyo kutoka, nilijikuta nikivichukia vituo vya redio na televisheni ambavyo vilikuwa vikiupa ‘air-time’.

Hakuna ubishi kuwa wimbo huo umejaa lugha ya matusi, tena yasiyojificha, kiasi kwamba hata mtoto wa umri wa miaka 10 ataambulia uchafu unaozungumziwa.

Lakini pia, balaa zaidi ni video yake ambayo inahitaji akili za mwendawazimu kuitazama ukiwa ukumbini na familia yako.

Kwa zaidi ya asilimia 70 ya video hiyo, wanawake walikuwa uchi, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Kitanzania.

Kutokana na heshima kubwa aliyonayo Diamond kwa mashabiki wa muziki wa hapa nchini na Afrika kwa ujumla, sikutegemea kama angethubutu kushiriki kwenye vitendo hivyo vya uvunjifu wa maadili.

Nadhani Diamond alisahau au kujisahaulisha kuwa kazi zake zina mashabiki wa rika na jinsia tofauti.

Haoni kama amewadhalilisha mashabiki wake wa kike? Vipi kama watasusia kazi zake kwa kile alichowafanyia?

Lakini pia, hakuna ubishi kuwa amewaangusha mashabiki wake wenye umri mkubwa na wanaojiheshimu.

Unajua kwanini nimembebesha mzigo wa lawama Diamond kuliko Mavoko ambaye pia alishiriki kwenye uchafu huo? Jibu ni rahisi.

Ngoma ile ni mali ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo iko chini ya Diamond. Ikumbukwe kuwa kwa sasa Mavoko anasimamiwa na lebo hiyo, hivyo ni mfanyakazi wa msanii huyo.

Kwa maana nyingine, Diamond alikuwa na uwezo mkubwa wa kuizuia ngoma hiyo kutoka mpaka pale ambapo angejiridhisha kuwa imefikia viwango vya kimaadili.

Kwa maoni yangu, Diamond anatakiwa kujitathmini upya na kama itawezekana awaombe msamaha mashabiki wake kwa kushiriki vitendo vya uvunjifu wa maadili. Ni hayo tu.
Acha kuandika umbea ww matus gan unayoyasema na Ney wa mitego tutasemaje na huo mvideo wa Rosa Ree hpo chin kaimba nin[emoji116] [emoji116] punguza ushabiki mtoa mada km cjakosea ww n mojawapo ya tmu kibakul[emoji35] [emoji35]
 
Kwanza Mwasi Matata Unavosakata Kiuno taranta Jini makata Vonikamata Kichwa na Ngata Soka Samatta
 
Back
Top Bottom