Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mnajadili upumbavu diamond hafanyi mziki kwajili yako na mleta Uzi.unasema video chafu Ni chafu kipande kipi kwa mfano?Mimi mwenyewe nimekuwa discouraged na video ile. Atambue kuwa ana fan base kubwa. Yeye kama moja wa maicon kwenye muziki wetu hakutakiwa kuruhusu video chafu vile itoke achilia mbali kushiriki.
Asantevideo ni kweli huwezi kuangalia na watoto! Ila wakati mwingine analenga soko la mbele bwana unabaki bongo tu ndio yale fiesta ikipita unasubiri fiesta nyingine ndio upate show kubwa!
Kwani salome mbona inapigwa mpaka maharusini ,kwani wanajua kusimamia kama kangaroo maana yake nini? Ibane.
........
ale kokoro babiiiii.......nifinyie kwa ndani
ha haaa haaaa go chibu go
RightInakiki BBC extra radio,Trace huko,MTV,sound city,wewe mchimba chumvi unatuambia nini,akiimba ukimuona mnasema kaswida,DIAMOND WANYOOSHE MZEE.
Huu wimbo kwa ajili yako
Huu wimbo kwa ajili yako
hahahahaHuyu naye ni kichaa mwingine aliyekutana na studio
Nimeirudia upya kuaangalia sijaona sehemu chafu usiwe na shaka mkuuMnajadili upumbavu diamond hafanyi mziki kwajili yako na mleta Uzi.unasema video chafu Ni chafu kipande kipi kwa mfano?
Acha kuandika umbea ww matus gan unayoyasema na Ney wa mitego tutasemaje na huo mvideo wa Rosa Ree hpo chin kaimba nin[emoji116] [emoji116] punguza ushabiki mtoa mada km cjakosea ww n mojawapo ya tmu kibakul[emoji35] [emoji35]copied somewhere
NA HASSAN DAUDI
HUENDA ujumbe wangu huu kwa mwanamuziki anayeitesa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, ukawakera wengi na hata yeye mwenyewe.
Lakini, nimejiridhisha kuwa ninachotaka kukizungumzia hapa ni kwa masilahi yake, jamii inayomzunguka na soko la muziki kwa ujumla.
Kwa maana nyingine, kwa kuwa lengo langu si kubomoa bali ni kujenga, natamani kuona ‘message’ yangu hii ikiachwa huru kwa kutopewa tafsiri zitakazojenga chuki kati yangu na supastaa huyo.
Naamini Watanzania wa sasa wana uelewa wa kiwango cha juu kuliko miaka kadhaa iliyopita.
Kwa maana hiyo, sina shaka kuwa ujumbe huu utabaki kuwa sehemu ya mchango wangu kwenye soko la muziki na si vinginevyo.
Jina alilopewa na wazazi wake la Nasib Abdul si maarufu sana miongoni mwa mashabiki wa muziki hapa nchini.
Ni tofauti na utakapomwita Diamond ‘Paltinum’, ambapo hata mtoto mdogo atakwambia mambo mengi yanayomhusu staa huyo na kukuimbia moja ya ngoma zake.
Nikiri kuwa napenda anavyoishi kistaa na zaidi ni jinsi anavyojua mbinu za soko ikiwamo kutafuta ‘attention’ kutoka kwa mashabiki wake. Anaishi dunia ya kisasa zaidi.
Kwa hapa Bongo, unapotaja wakali wa Bongo Fleva, huwezi kuliweka kando jina lake hata kwa bahati mbaya.
Mbali na sauti nyororo, tungo na swaga zake, ubunifu ni miongoni mwa silaha zilizomwezesha Diamond kuteka hisia za mashabiki wa burudani.
Kwa sasa anatajwa kuwa mmoja kati ya wasaniii maarufu na wanaokubalika zaidi barani Afrika.
Wakati Nigeria ikijivunia Wizkid, Davido, D’banj, Flavour na wengineo kwenye tuzo mbalimbali, Diamond ameonekana kuwatosha kabisa akiwa peke yake. Ni wazi Tanzania inajivunia kuwa na staa huyo.
Kwa kipindi kifupi tangu alipotoka na ‘Kamwambie’, miaka isiyozidi 15, tayari nyota huyo ameliletea Taifa letu sifa kibao. Ameshinda tuzo nyingi zinazoandaliwa ndani hata zile za ng’ambo.
Haimaanishi nawapuuza wasanii wengine akiwamo mpinzani wake, Ali Kiba, la hasha! Ila hatuwezi kuukataa ukweli kuwa Diamond ameleta mapinduzi makubwa kwenye soko la muziki. Hakuna anayeweza kumnyima ujiko huo.
Hata hivyo, bado nina shaka kuwa Diamond hajatambua thamani yake kwa Watanzania.
Kinachonifanya niamini hivyo ni wimbo mpya uliotoka wiki chache zilizopita ambao ameshirikiana na swahiba wake, Rich Mavoko.
Binafsi niliposikia taarifa za ujio kibao hicho kinachokwenda kwa jina la ‘Kokoro’, nilitamani sana kupata bahati ya kuusikiliza na hata kuitazama video yake.
Shauku hiyo ilitokana na kutambua uwezo mkubwa walionao wanamuziki hao, hasa Diamond ambaye ndiye mwenye Bongo Fleva yake kwa sasa akisaidiana na Ali Kiba.
Nikiri wazi kuwa baada ya ngoma hiyo kutoka, nilijikuta nikivichukia vituo vya redio na televisheni ambavyo vilikuwa vikiupa ‘air-time’.
Hakuna ubishi kuwa wimbo huo umejaa lugha ya matusi, tena yasiyojificha, kiasi kwamba hata mtoto wa umri wa miaka 10 ataambulia uchafu unaozungumziwa.
Lakini pia, balaa zaidi ni video yake ambayo inahitaji akili za mwendawazimu kuitazama ukiwa ukumbini na familia yako.
Kwa zaidi ya asilimia 70 ya video hiyo, wanawake walikuwa uchi, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Kitanzania.
Kutokana na heshima kubwa aliyonayo Diamond kwa mashabiki wa muziki wa hapa nchini na Afrika kwa ujumla, sikutegemea kama angethubutu kushiriki kwenye vitendo hivyo vya uvunjifu wa maadili.
Nadhani Diamond alisahau au kujisahaulisha kuwa kazi zake zina mashabiki wa rika na jinsia tofauti.
Haoni kama amewadhalilisha mashabiki wake wa kike? Vipi kama watasusia kazi zake kwa kile alichowafanyia?
Lakini pia, hakuna ubishi kuwa amewaangusha mashabiki wake wenye umri mkubwa na wanaojiheshimu.
Unajua kwanini nimembebesha mzigo wa lawama Diamond kuliko Mavoko ambaye pia alishiriki kwenye uchafu huo? Jibu ni rahisi.
Ngoma ile ni mali ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo iko chini ya Diamond. Ikumbukwe kuwa kwa sasa Mavoko anasimamiwa na lebo hiyo, hivyo ni mfanyakazi wa msanii huyo.
Kwa maana nyingine, Diamond alikuwa na uwezo mkubwa wa kuizuia ngoma hiyo kutoka mpaka pale ambapo angejiridhisha kuwa imefikia viwango vya kimaadili.
Kwa maoni yangu, Diamond anatakiwa kujitathmini upya na kama itawezekana awaombe msamaha mashabiki wake kwa kushiriki vitendo vya uvunjifu wa maadili. Ni hayo tu.