Diamond kainuliwa na Mungu mwenyewe. Binadamu hawezi kumshusha

Diamond kainuliwa na Mungu mwenyewe. Binadamu hawezi kumshusha

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Achana na mapungufu yake, haya tumeumbiwa wote chini ya jua.. Kwakuwa sisi wa mwili wa damu na nyama si wakamilifu..

Mungu huwainua wachache kati ya kwa kila taifa, ukoo hata familia.. Huwainua kwa vipawa na vipaji mbalimbali... Na wengine baada ya kujitenga na dunia hutunukiwa karama mbalimbali za kiroho

Diamond Mungu kamtunuku kipaji cha uimbaji wa nyimbo za kidunia na kipawa cha kuweza kufanya mambo makubwa ambayo kuna mamilioni ya wasomi wameshindwa kufanya

Usimwangalie Diamond wa sasa bali mwangalie pale alipoanza kuonekana kwenye mwanzo wa msingi wa mafanikio kupitia wimbo wake wa Mbagala..Na baada ya hapo kuzindua brand yake ya WASAFI iliyoanza kama utani

Mtoto wa fukara aliyelelewa na mzazi mmoja, aliyeshindwa kusoma shule bora na pengine kushindwa kumaliza masomo yake kutokana na changamoto za karo sare nk... Mungu hujidhihiri kupitia watu kama hawa
Kumbuka ni mzazi gani ambaye hapendi mwanawe awe kama Diamond? Na ndio maana kila mzazi mwenye uwezo anajitahidi kumpatia mwanawe elimu bora ili aje kuwa fulani katika maisha...

Njia aliyopita Diamond ni ngumu, nyembamba na iliyojaa taabu na misukosuko mingi, lakini kuna sauti na nguvu ya kiroho iliyokuwa inampa hamasa kwa kila hatua aliyopitia.. Ni wengi wamepita na wanapita aliyoptia Diamond.. Wanapambana kufa na kupona, lakini kwa Mungu kila mmoja ana kipimo chake

Diamond sio wa level ya wasanii wengi kwa sasa kitaifa kikanda na hata kidunia.. Usiangalie followers wake tuu mitandaoni, na mali anazomiliki. Bali mwangalie jinsi alivyoweza kutengeneza legacy yake kwa kuwatengeneza wasanii wengine kupitia yeye mpaka wakajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania.. Ana hiki kipawa cha kumbrand mtu.

Tuna wasanii wengi na wazuri sana lakini bado hakuna mpaka sasa aliyeweza kufanya aliyofanya Mond..hata kama baadhi wameweza kujisimamia lakini kusimamia wengine wakawa kama wao wameshindwa kabisa.. Kwasasa WASAFI ni BRAND tishio kwenye hilo...!

Nitarejea[emoji1541]
[emoji1541]
Naendelea
Dunia ina wasanii wakubwa wengi, maarufu na matajiri sana waliofikia mafanikio yao kwa njia mbalimbali haramu na halali lakini Mungu akamuinua mmoja tu kati yao naye si mwingine bali ni mfalme wa pop duniani Mwendazake Michael Jackson mwafrika kwa jina la mmarekani mweusi... Ukimwengu utapita vizazi vingi kabla ya kumpata MJ mwingine

Diamond is almost there.. Japo hajafika lakini aliyoyafanya mpaka sasa anastahili kupewa heshima yake kitaifa.. Huyu ni mmojawapo ya tunu za taifa kupitia sanaa ya mziki wa kisasa.. Ni mbunifu, ni mtunzi ni muibua vipaji na mwendeleza vipaji, ni mjasiriamali na yuko very smart kwenye kazi zake..!

Action speak louder than words.. Si muongeaji sana lakini matokeo ya kazi zake yanaonekana.. Ufahari wa kununua vitu vya gharama kubwa ni kiu ya binadamu yoyote yule, lakini vilevile ni kuudhihirishia umma kwamba yeye ni above next level ...!

Ndege yake inakuja iko njiani.. Gharama za kumiliki hiki chombo si mchezo hata kama hataitumia sana Lakini tayari ameshatengeneza historia nyingine ya msanii wa kwanza Tanzania na wachache ulimwenguni kumiliki chombo Kama hicho..

Waswaheli wanasema usimwingilie aliyepewa kapewa! Mond kapewa kama wewe hujapewa mwombe sana Mungu katika ukoo wenu kama si familia basi amuinue mmoja kati yenu atengeneze legacy ya familia na ukoo... ! Chuki dhidi yake ni roho ya washindwa na kijicho..

LA Mwisho wainuliwa wengi huwa hawana maisha mengi.. Lakini kwa Mond tunaweza kumfanyia ibada mwenyezi Mungu amjaalie maisha mengi mengi[emoji1545][emoji818]
 
Ameeen, ukimwangalia harmonize aliyekua anakataliwa na kila mtu!

Ukamtazama harmonize aliyebrandiwa na mond!

Then ukamchungulia harmonize anayemvimbia mond now, unaweza usisaidie mtu maishani!

Ila mond hachoki kusaidia, maana ndio kipawa chake!

Huyu mtu kwa nchi zenye watu wanaojielewa sio wa kumvunja moyo.
 
Kuinulia ni kuinuiliwa ni kuinuliwa u bila kujali ni falme gani imekuinua.. anaweza kuwa ameinuliwa kiMungu au na kuzimu yote ni kuinuliwa na kufanikiwa......

Kitu pekee ninachokijua hata kama umeinuika namna gani au ni upande gani ndio unakuinua ila ukianza kutumia nafasi yako kugusa taasisi za za kiMungu vibaya hapo unakosea.

Mfano kuna nyimbo mbili ambazao diamond ameligusa kanisa. na kanisa ni taasisi ya kiroho ambayo inataratibu zake na usafi wake na sherehe zake.. sasa unapotumia nyimbo za kidunia kwenye taasisi ya kiMungu tegemea matokeo baada ya mda fulani hata kama hayataonekana sasa ila lazima yatatokea...
tofauti na hapo diamond anajitahidi sana na anajituma
 
Zaburi 10:3-7

3. Mwovu hujisifia tamaa zake mbaya, mtu wa tamaa hulaani na kumkataa Mwenyezi-Mungu.
4. Katika majivuno yake husema: “Mungu hatagundua.” Mawazo yake yote ni: “Hakuna Mungu.”
5. Njia za mwovu hufanikiwa daima; kwake hukumu zako ziko mbali na mawazo yake, na huwadharau maadui zake wote.
6. Huwaza moyoni: “Sitakuwa na wasiwasi; sitapatwa na dhiki maishani.”
7. Kinywa chake kimejaa laana, udanganyifu na dhuluma; mwepesi kusema maneno ya kuchukiza na maovu. (rejea maudhui ya nyimbo zake)


Mengine tumuachie mwenyewe Maulana
 
We mlozi umeamua kumtetea mlozi mwenzako pathetic

Huyo domo uccm upuuz kibao kichwan pesa sio kila kitu man
Achana na mapungufu yake, haya tumeumbiwa wote chini ya jua.. Kwakuwa sisi wa mwili wa damu na nyama si wakamilifu
 
Back
Top Bottom