Diamond kapoteza mvuto?

umemaliza
 
Hata jordan hana umiliki wa jordans 100%..

Mikataba anayoingia dimond ni mikataba inayoingiwa na wasanii wengi tuu duniani wanatangaza brand fulani kwa malipo au kupata asilimia kadhaa za umiliki.
 
Mpaka sahizi nyimbo ambazo zimeangaliwa zaidi youtube mwaka huu hapa Tz ni 2 kwangwaru pamoja na african beauty zimeangaliwa kwa pamoja mara milioni 40.

Zote diamond ameshiriki..

chuki chukieni... ila numbers dont lie@
 
Mimi nina uhakika mwandishi wa huu uzi inawezekana kakurupuka bila kufanya research kutokana na vijimaneno vya kwenye page za udaku au hamfahamu kabisa mond ila kackia tu mond n mtu fulan maarufu kaamua kumtungia uzi... mie naeza kusema kati ta miaka ambayo mondi kapiga hatua kubwa sana ni mwaka huu....
 
Mimi nikisikia tu "wasafi" huwa nachefuka maana wana tone moja wanayotumia katika nyimbo zote kama ya kulalamika hivi..oh sijui mama aliniambia..Vile visauti vya kumwiga diamond huwa vinaniboa sana.Hivi sasa hata nikitaka kusafiri naangalia gari lisilo na TV maana huwa nachefuka njia nzima akili inalazimishwa kupokea ujinga ujinga wa wasafi.
Nawapongeza wasanii wengine wa bongo fleva maana unaona kweli ni wabunifu.Sielewi kwa nini watu wanapenda nyimbo hata kama ni za hovyo za wasafi
 
Duzhel

Dushelele analitembeza kila sehemu, Hachagui wala habagui naona kasharogwa sana. Umalaya ukizidi akili hupungua
 
Nimeipenda last paragraph!
 
Diamond ni bland kubwa Tanzania,acheni kujifanya mnajua kufanya uchambuzi kwamba anafeli,ndio msanii pekee anayewekwa kwa sasa kwenye level moja na kina davido na wizikd,maana hata p square wameshapotea
 
Acha kutetea wanawake wenzio, waliyataka wenyewe, Diamond anawakilisha tabia ya mastaa duniani kote hawajahi kudumu katika ndoa au mahusiano, kama nikuzalilishwa walitaka wao wenyewe
Mimi siwatetei ila sipendagi wanaume wajinga wasiojielewa wanaozalilisha MTU anayemvulia chupi na kuzini wote huko ni kutokukua kiakili, kuna wanaume wako vzuri huwa hawazalilishi waliovuliana nguo, sasa huyu mtandale asiye na exposure ndo hufanya huo ujinga
 
hahah comment yako inachekesha..

Unaposema Dimond hana Expossure unamaanisha nini, ameshatembea nchi ngapi, kakutana na watu wangapi tangia ametoka mwaka 2009!

Labda utumie neno jingine ila ukisema Dimond hana exposurre unakosea si kidogo
 
Ndo maana nimekwambia hao unaosema wewe wanadhalilishwa wanapenda hivyo anavyowafanyia
 
Nahisi haumfahamu diamond vizuri labda nikueleweshe kidogo diamond ni nani?

HOJA YA UMILIKI KIBIASHARA
Hakuna mtu ambaye anaumiliki wa kila kitu kwa asilimia mia moja... inabid ukiri tyu kuwa kwenye biashara ww bado kabisaaaa.... hata haujui mfumo wa biashara unavoenda... tukianzia hapa bongo bakhresa ana umiliki wa 80% wa azamu... mo dewji ana umilik wa asilimia 65% wa kampuni yake.... dangote pia... njoo kwa bill gates tajiri wa dunia ana hisa nyingi microsoft... inamaana kuwa hana umiliki wa 100%. Mark zugerberg mwenyewe mitandao ya kijamii hana umilik wa asilimia zote.... so sio ajabu kwa diamond kuwa na umiliki wa hata nusu vya vile anavomiliki wengine wakashika kulikobak...

Tukija upande wa matangazo... diamond kasain mkataba na kampun ya vinywaji ya kifaransa Bellaire... kasain mkataba na gucci kampuni kubwa duniani la nguo ambao wanavalisha lebo na familia nzima... Bado pia dili na Safaricom ya kenya...

Kwa upande wa show...
Mwanzoni tu mwa mwaka huu alipiga show tano mfululizo Kenya... akaja akapiga show kubwa kabisa kenya hukohuko siku ya uzinduzi wa albam yake ya "a boy from tandale".... km hiyo haitoshi akafanya tour katika miji kumi huko marekani... hakukaa akaelekea mayotte ambako nako akafunika vya kutosha... hakupoa tena huyooo madagaskar ambako akaenda kujaza uwanja wa mpira... Hapo bado haitoshi ana show tatu kubwa huko Kanada... kuna One music fest dubai... kuna nyingine hv karibuni namibia.... Pia kuna wasafi festival inakuja hapo bado kuna mtu atasema kaporomoka

Katika kuwekeza kijana katia juhudi ya hali ya juu sana... ndio msanii pekee east africa kumiliki media zake... Afrika nzima wapo wawili tu na yule wa naija.... ana karanga ambazo ofa zake hata za miss tanzania hazikuona ndani... perfume inafanya poah sana huko uarabuni... ana lebo kubwa afrika yenye wasanii wa A-Class... anamiliki mtandao wa kuuzia nyimbo wasafi.com...

Kwenye nyimbo usipime... kila songi lake ni fireee... kila kolabo lake ni hatari... wabongo wanaita homa ya jiji.... icheki african beauty, iyena, kwangwaru, time to party na inayosumbua kwa sasa #Jibebe....

Vijana wengi kawainua mond... kuanzia watangazaji, madansa, wasanii, wapigapicha, walinzi, nakadharika....
Bado skendo za ajabuajabu ambazo zimewainua wengi akiwemo Hamisa na wengine wote waliowahi kuhusishwa naye...

Kiufupi mondi sio wa kispotispoti sidhan km ataweza poromoka leo au kesho....
 
Nenda wasafi.com ile yakuuza nyimbo zao hamisa mobetto kaweka wimbo wake humo wa madamhero halafu unakuja MTU unamtetea mwanamke,hivi kati ya hamisa na wewe nani anawadhalilisha wanawake na kama siyo wanawake wenyewe wanajidhalilisha.
 
Siamin km hao unaowaongelea wananyanyaswa au kudhalilishwa.... kukurupukia kila kinachozungumzwa mitandaoni nao ni ujinga usio na maana... kwan kuna aliyewah wathibitishia kuwa hapendi? Mambo mengine ni yao binafsi... we yakikuuma inabid upotezee tu maana hayakuhusu... we fatilia mziki wake potezea... kwan n wangapi ambao huwa wanapigwa na kufukuzwa kwao km mbwa mwiz mnawafumbia macho? Kawatetee kwanza hao ndo uje umtetee anayetoka na mond... kwanza naona ni bora sana anavofanya mond kuliko km angekuwa anawapiga na kuwafukuza kabisa... yaan wawe paka na panya
 
Umetoa povu la bure hao wanaopigwa hawajulikani lakini diamond yeye ndo huweka mambo yake hadharani ili atrend lazima tu apate mtazamo tofauti, ndo maana baada ya makiki za uzalilishaji wa wanawake watu wamemchoka hata hatishi ka before sasa anabaki kutumia kiki za uchawi za baby mamas
 
hahah comment yako inachekesha..

Unaposema Dimond hana Expossure unamaanisha nini, ameshatembea nchi ngapi, kakutana na watu wangapi tangia ametoka mwaka 2009!

Labda utumie neno jingine ila ukisema Dimond hana exposurre unakosea si kidogo
Kutembea nchi mbali mbali hakujamtoa tope la ujinga kichwani ka anashindwa heshimu wanawake kwangu ni useless hana exposure yoyote angekuwa nchi za nje kumemfundisha asingefanya huo ujinga tena angeshapotea kimuziki siku nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…