Diamond Kununua Private Jet Ndani ya Mwaka Huu (2014)

Diamond Kununua Private Jet Ndani ya Mwaka Huu (2014)

na hivi 'baby' keshamnunulia wema vifaa vya ofisi yake? nimesubiri two weeks sijasikia habari?
nimepitwa eeenh?!?
 
attachment.php


Haya yote yamedhihirishwa wazi kwenye ukurasa waka wa IG yaani instagram kwa kuweka picha ya ndege na gari la kifahari na kuandika "Tuseme Inshaallah... #2014 #JusWaitAndSee #KwaniWaoWamewezaje #HadiWeUshindwe #WCB for life Darling....!" akimaanisha ya kwamba mafans wake wakae mkao wa kula na wajionee maajabu na kwamba ile gari ya pesa chafu landcruisser v8 aliyonunua si kitu akisingiziwa na haters eti kakodishwa na chief kiumbe,

OK so kiuffupi ni kwamba itabidi tumpe support kijana wetu wa tz aifanye hii ndoto iwe kweli maana ikitokea hivi sio siri atakua miongoni mwa wasanii waliojipatia mafanikio kuzidi tunavyofikiria

Toa comment kama una nyongeza..
Mbona atawakomba kila kinachokatiza yeye ni kuweka timetable tu wewe leo kesho wewe.
 
Sijui kama ndoto hii ina busara yoyote. Kwanza ndege si kama gari. Ina utaratibu tofauti kabisa wa umiliki na matunzo. Tuseme amemudu bei ya kununua hiyo Private jet (crazy idea in itself), kwanza inabidi ipaki kwenye viwanja vilivyosajiliwa kitaifa na kimataifa na kulipiwa kwa masaa (sio bei ya parking za magari mitaani DSM!). Halafu inabidi iwe na hati updated za usalama. Haitengenezwi ikiharibika; ina ratiba (kwa masaa) na viwango maalum vya service na matengezo (checks) - hapo ulizia bei ya kila check. Rubani wake naye leseni yake si kama ya daladala; ina gharama zake maalum.

Swali linabakia: katika mazingira ya kiuchumi ya ki-TZ, kuota kununua private jet kwa mtu wa aina ya Diamond (shughuli zake za uchumi) ni ndoto sahihi? Nacho ni moja ya vigezo vya mafanikio vya kujivunia kwa vijana wetu au ni aina nyingine ya ujinga wa kukosa shule ya maana? Tuwahamasishe vijana watafute maendeleo kwa ndoto zenye viwango muafaka sio hizo za kijinga. Nchi yenyewe hata viwanda vya kimataifa haina. Labda kama tunataka kuwaingiza kwenye uchumi wa Medellin!
 
Good for u Diamond wakimbize .....!!ipe roho ile kitu inapenda maisha yenyewe mafupi , wenye chuki roho mbaya na wivu watakuponda sana but keep it up
 
Back
Top Bottom