Diamond Kununua Private Jet Ndani ya Mwaka Huu (2014)

na hivi 'baby' keshamnunulia wema vifaa vya ofisi yake? nimesubiri two weeks sijasikia habari?
nimepitwa eeenh?!?
 
Mbona atawakomba kila kinachokatiza yeye ni kuweka timetable tu wewe leo kesho wewe.
 
Sijui kama ndoto hii ina busara yoyote. Kwanza ndege si kama gari. Ina utaratibu tofauti kabisa wa umiliki na matunzo. Tuseme amemudu bei ya kununua hiyo Private jet (crazy idea in itself), kwanza inabidi ipaki kwenye viwanja vilivyosajiliwa kitaifa na kimataifa na kulipiwa kwa masaa (sio bei ya parking za magari mitaani DSM!). Halafu inabidi iwe na hati updated za usalama. Haitengenezwi ikiharibika; ina ratiba (kwa masaa) na viwango maalum vya service na matengezo (checks) - hapo ulizia bei ya kila check. Rubani wake naye leseni yake si kama ya daladala; ina gharama zake maalum.

Swali linabakia: katika mazingira ya kiuchumi ya ki-TZ, kuota kununua private jet kwa mtu wa aina ya Diamond (shughuli zake za uchumi) ni ndoto sahihi? Nacho ni moja ya vigezo vya mafanikio vya kujivunia kwa vijana wetu au ni aina nyingine ya ujinga wa kukosa shule ya maana? Tuwahamasishe vijana watafute maendeleo kwa ndoto zenye viwango muafaka sio hizo za kijinga. Nchi yenyewe hata viwanda vya kimataifa haina. Labda kama tunataka kuwaingiza kwenye uchumi wa Medellin!
 
Good for u Diamond wakimbize .....!!ipe roho ile kitu inapenda maisha yenyewe mafupi , wenye chuki roho mbaya na wivu watakuponda sana but keep it up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…