Diamond kwa sasa hana Baba, ukweli mchungu

Diamond kwa sasa hana Baba, ukweli mchungu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
DIAMOND KWA SASA HANA BABA, UKWELI MCHUNGU.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Tahadhari: Makala hii inaweza isimfae kila mtu, kwani lugha iliyotumika humu inaweza kuwa kali na yenye kuumiza kwa baadhi ya watu. Hivyo ikiwa wewe unajijua sio mvumilivu wa lugha ngumu, maneno makali basi nakusihi ishia hapa hapa kusoma. Na kama utaendelea basi ni wazi umejiona kuwa utahimili, hivyo sitahusika na maumivu au athari yoyote itakayokupata kisaikolojia.

Wiki hii kumekuwa na watu wengi mtandaoni hasa Youtube ambao wamemuandama Msanii mkubwa wa taifa hili aitwaye Diamond PLatnum kuhusu sakata lake na Baba yake, Mzee Abdul. Wengi wamekuwa wakimponda Diamond kwa kutomsaidia Baba yake, Mara sijui hamjali, sijui hampendi, sijui hamhudumii basi kila mmoja na maoni yake na jinsi uelewa wake ulivyo. Wanahaki ya kutoa maoni kwa kadiri akili yao inavyowatuma, lakini lazima jambo hili tulijadili kwa mapana yake.

Nimeandika makala hii kwa sababu, sio Diamond pekee ambaye hamtunzi Baba yake, yapo maelfu na maelfu ya vijana wasiotunza wazazi wao kwa sababu zao mbalimbali. Na ndio maana hata Mbunge wa Kahama Mjini, Mhe. Kishimba Mwaka jana kama sikosei alishawahi kupeleka hoja Bungeni kuhusu kuundwa kwa sheria ya lazima kwa watoto kusaidia wazazi wawapo wazee. Lakini leo tujajikita zaidi kujadili wale wasiohudumia baba zao au wazazi kwa sababu ya KUTELEKEZWA NA MMOJA WAZAZI AU WAZAZI WOTE.

Diamond ni kielelezo cha vijana wengi waliomo ndani ya taifa hili waliotelekezwa na Baba kama inavyofahamika na ilivyoelezwa. Hakuna jambo baya kama kutelekezwa iwe kwa sababu au bila sababu maalumu. Kumtelekeza mtoto inamuathiri kimakuzi yake, mtoto anakuwa anaishi bila kujiamini hata kama akiishi maisha ya kuaminishwa kuwa ajiamini. Mtoto anayetelekezwa na Mama au Baba huathitika kisaikolojia na mara nyingi baadaye huwa na roho ngumu mno licha ya kuwa anaweza kuwa na utu lakini kwa sehemu kubwa anaweza kuwa mkatili. Ni watoto wachache ambao wametelekezwa ambao wakiwa watu wazima hawana roho ngumu.

Baba anapomtelekeza mtoto kwa sababu yoyote ile bila kujali ni nzuri au mbaya. Mtoto huanza ku-assume kwamba hana Baba, na Baba yake alishakufa miaka mingi. Na hapa ndipo hatari inapoanza. Baba anaweza kufikiri anamtoto licha ya kumtelekeza lakini kwa upande wa mtoto yeye anajua hana baba, tena anaassume kama alishakufaga miaka mingi mno licha ya kuwa anakutanaga naye iwe barabarani au kwa kuongea na simu mara moja moja. Ukishatelekeza mtoto ni kujitengenezea mazingira ya mtoto kukuona MZIMU unayeishi duniani. Yaani mtoto akikuona anakuchukulia kama mzimu uliyekwisha miaka mingi mno. Kikawaida mtu akishakufa hana sehemu kwa waliohai, hivyo mtoto anakuchukulia kuwa huna msaada wowote, wewe ni mzimu tuu, ulishakufa na kuoza miaka mingi moyoni mwake.

Ninaongea jambo hili kwa uzoefu, sio kwa kuhadithiwa, naongea kitu ninachokielewa kwani nami ni sehemu mambo haya. Mzazi akishakutelekeza na kukuacha ukiwa tangu mdogo na hapa nazungumzia chini ya miaka saba kama sio kumi.
Baba hajui unasoma au husomi
Baba hajui unakula nini na unavaa nini
Baba hajui lini uliumwa na ulitumia madawa gani
Baba hajui hata bei ya pensel au daftari mapaka unamaliza shule
Baba hajui hata unamiaka mingapi
Baba hana anachojua kuhusu wewe zaidi ya kujua wewe ni mtoto wake

Baba hajali wala kuthamini kuwa wewe ni mwanaye, hajitoi kama Baba ili uone jitihada zake hata kama hana pesa au hana mali, hata kukutafuta na kukusalimia kila mara hiyo tuu hataki. Alafu kuna Mababa wengine mafala sana(Ninaweza kuwa hata mimi pia), unayakuta yanajadili kabisa ati mtoto akikua atakuja mwenyewe, mimi ni Baba yake tuu, Yaani kama punguani au mwehu. Nani aje, labda watoto wehu wasiojitambua, ukizingua unazinguliwa, ukijifanya kidume kutia mimba alafu hujui kulea alafu unasubiri toto likue ndio ulete kaptura yako hutaamini macho yako nakuambia, ukijifanya unatema laana zako uchwara tunakutimua na upuuzi wako, watishe wajinga huko, na huyo mungu mpumbavu aliyekufundisha kufanya upuuzi, mwambie hatumuogopi kwani tunajua hana atakaloweza kutufanya.

Sisi tunamuamini Mungu aliyeumba mbingu na nchi, Baba anayejua majukumu yake, ambaye anakutaka utunze familia yako ikiwemo na watoto. Kama ulimuasi huyo mungu sasa subiri matunda yake, huwezi vuna usipopanda.

Watu wanamtishia Diamond Ujinga ujinga, ati atapata Radhi sijui laana, yaani upuuzi upuuzi tuu. Diamond chochote atakachokifanya kwa Baba yake yupo sahihi, asipomhudumia yupo sahihi kwani naye hakuhudumiwa na wala hatapata radhi wala laana popote pale labda mukamloge ndio muiite Laana, maana waafrika ndio tabia zetu hizi, mnajifanya mnamlaani alafu kwa nyuma mnaenda kumloga ili akidhurika ionekane ni laana. Hakuna cha laana hapo wala ndugu yake Radhi. Huwezi vuna usipopanda, kama alimzaa ndio kisingizio basi naye kamzalia wajukuu, hiyo pia inatosha. Kama kuzaa ndio kigezo hata mbuzi anazaa na ng'ombe.

Wanaume tuache upumbavu wa kuzaa na kutelekeza watoto. Tunawapa shida hawa wanawake na watoto. Unazalisha mwanamke wa watu unamuacha, anahangaika na lawama,majina ya hovyo, kutukanwa huku na huko sijui single mother ni kiwanja chenye mgogoro, sijui mtoto haramu, na upuuzi upuuzi mwingine. Alafu toto limekua limefanikiwa unaleta putura yako bila haya.
Umesahau mwanamke wa watu alivyotukanwa ni single mother kama kiwanja chenye mgogoro.
Umesahau kuwa ulivyomzalisha mwanamke wa watu ukamtelekeza alivyopata tabu kupata mwanaume mwingine wa kumuoa na kujenga uaminifu kwake
Umesahau jinsi ulivyokuwa unapigiwa simu za matatizo ya mtoto utume hata mia ya nguo hupokei simu unajifanya huoni.
Umesahau hayo, alafu unatakwa ukumbukwe kwa mambo yapi?

Umesahau jinsi mtoto wako alivyoitwa mtoto haramu wakati ungemuoa mama yake au kuishi naye wala asingedhalilishwa hivyo
Umesahau jinsi mtoto wako alivyohangaika kujieleza kuwa wewe(Babaake) yupo wapi na anafanya kazi gani pindi alivyokuwa akiuliwa shule za msingi na sekondari, wewe umejificha huko hata hutaki mtoto wako akujue.
Umesahau yote hayo au unajifanya huyajui, sivyo?

Watoto karibia wote waliotelekezwa wanajua nazungumzia nini, wengi mioyo yao ilishasahau habari za wazazi waliowatelekeza, walisha-assume wamekufa na wale wanaowaona ni mizimu.
Hivi Baba mzima unakaa miaka mitano hupigi hata simu kwa mtoto au kwa mama yake unategemea mtoto akikua atakupigia mara kwa mara. Watu hawajui kuwa input is equal to output. Au hawajui kuwa maisha hutumia kanuni ya KIOO. Ukisimama mbele ya kioo, ukicheka na taswira yako itacheka, ukinuna tawira yako itanuna.
Huwezi mtelekeza mtoto miaka nenda rudi alafu kwa upumbavu wako utegemee mtoto akiwa mkubwa atakutafuta mara kwa mara, hiyo haipo na haijawahi kuonekana.

Hata walioko kwenye ndoa wenyewe ni mashahidi, mzazi mwenye mazoea na watoto(wengi huwa kina mama), mtoto akikua humtafuta mama zaidi kuliko Baba, na wapo watoto ambao huwatafuta baba zao kuliko mama zao na hii ni kutokana na mazoea tangu utotoni.

Kuna watu wanasema Diamond amsamehe Baba yake, wako sahihi kabisa.
Lakini nataka kuwaambia, na waliotelekezwa wote na wazazi wao ni mashahidi hapa; hata umsamehe mzazi aliyekutelekeza bado hamtakuwa na mazoea kama ilivyokawaida, kama mlikuwa hamuongei hamtaongea kabisa. Kwanza mtaongea nini na mtu ambaye hamna mazoea naye tangu ukiwa mdogo kabisa, mtaongea nini hasa. Unajua watu wanamlaumu Diamond lakini hawajui tuu mambo haya.

Kuhusu Kumtunza;
Diamond na watu wa aina yake wanayohiyari ya kuwatunza wazazi wao waliowatelekeza. Diamond anaweza akamtunza au asimtunze Baba yake. Kama Baba yake hakuchukua kuwa ni wajibu kumtunza mwanaye, Diamond yeye akiwa kama Baba, akafanya ni hiyari yake. Basi hata Diamond anaweza kuona sio wajibu wake kumtunza Baba yake bali ni hiyari yake.

Kuna watu wanadhani Diamond ataumia kama baya lolote litampata Baba yake, kama wewe ni mmoja wao basi unakosea sana. Watu kama Diamond waliotelekezwa na wazazi wao hakunaga upendo tena kwa Baba zao, yaani tayari wanaona kama hawana Baba, Baba zao walishakufa miaka mingi sana. Hawapati maumivu yoyote kwa lolote litakalo wapata Baba zao ikiwa tuu waliwatelekeza. Hivyo mtu anayedhani Diamond ataumia siku Baba yake akipata madhara ni kwamba haelewi mambo haya.
Moyo uliokufa hauwezi kuumia.

Diamond anamchukulia Baba yake kama watu wengine, wala hana kinachomuuma, hata akimsaidia, Baba Diamond asidhani anasaidiwa na mtoto wake bali ajue anasaidiwa na mtu baki.

Ukiona mtu alitelekezwa na mzazi wake iwe ni Baba au Mama na anajifanya anaupendo na Baba au Mama aliyemtelekeza wengi huwa ni wanafiki, wengi wanafanya hivyo kuogopwa kusemwa na jamii.

Wewe kama unauchungu na Baba, mhudumie Baba yako na Mama yako, usijifanye una uchungu wa mzazi kwa wazazi wasiokuhusu.

Tena Diamond alitakiwa asiwasiliane kabisa na Baba yake ili iwe fundisho kwa sisi wanaume wengine kuwa tutunze watoto wetu. Tena angetakiwa aende kumshtaki mahakamani kwa kumtelekeza ili atie adabu.
Lakini kusema amsamehe ni kufundisha vijana wadogo kutelekeza watoto alafu wanajua mwisho wa siku wataomba msamaha na watasamehewe..
Hatuwezi ishi hivyo, niliwahi sikia habari za Mwana FA ambaye sasa ni Mbunge wa Muheza naye alimzingua Baba aliyejitia ni Baba yake.

Wewe kama unauchungu na Baba wa mtu badala ya Baba yako, kamsaidie wewe.

Kuhusu laana ya Mungu, tutakutana kwa Mungu huko, mbele kwa mbele.
Waafrika wengi bado tuna mambo ya kipuuzi na kutishana kusiko na sababu, ati mzazi hakosei, hakosei yeye ni Mungu?
Mimi ni mzazi ninakosea mara kwa mara, kama ninyi wazazi msiokosea shauri yenu waambieni watoto wenu wajinga hivyo. Maana kuna viwazazi mshenzi vinajifanya miungu watu havikosei. Upumbavu mtupu. Mungu ndio hakosei sisi wengine Garagaja. Watoto wangu mimi Baba yenu ni mzazi lakini pia nakosea.
Nikizingua mnayohaki kunizingua mkinisamehe hiyo ni neema mmenipa. Nimemaliza.

ZINGATIA, Makala hii haimuhusu Baba Diamond na Diamond pekee bali jamii nzima, inahusu sisi wababa wote tuache kutelekeza watoto. Pia Makala hii imemchukulia Baba Diamond kama mtu aliyemtelekeza Diamond kutokana na kile kinachoendelea mitandaoni hivyo inaweza kuwa kweli au sio kweli. Kuhusu Wamama nitaandika siku nyingine.

WITO: Wababa tuache kutelekeza watoto kwa matokeo yake huweza kuja na athari mbaya. Pia watoto tuliotelekezwa tunaweza kusamehe kama inawezekana lakini tujiepushe na unafiki, kama huwezi kusamehe ni bora usisamehe kuliko kujifanya umesamehe alafu ukabaki na kinyongo ndani kwa ndani.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam
 
Wengi wenu hamjui ukweli kuhusu baba yake na diamond platnum ila kuna mengi anayo yaongea ni uongo na machache yanaweza kuwa na ukweli.

Kwa mimi ambae namfahamu vizuri yule mzee na alikua jirani yangu kweli ukiwa na mzazi kama yule ni shida,kwanza mzee kutwa akishapata pesa ,anashinda kwenye vibanda vya gongo.

Mzee yule akikosa pesa ya kwenda kwenye hivyo viringe anajifanya anaumwa na kumlaumu mwanae kuwa hamsaidii na mguu unamsumbua lakini yote ni uongo ana matumizi mabaya ya pesa na mnywa gongo mbobezi.kwa hiyo amegundua akilalamika kwenye vyombo vya habari wake zake wa zamani wa diamondakiwepo wema,hamisa na wengineo wanamsaidia kumpa pesa kwa huruma zao lakini kipindi hicho hawajui ukweli sahihi
 
Wababa wa kiafrika ni moja ya watu wapumbavu kwenye hii dunia. Kwanza utafiti unaonyesha katika mtu anayefanya kazi kwa masaa machache kwa siku duniani ni mwanaume wa kiafrika.

Utamaduni wetu upo hivi toka zamani. Unaoa wake wengi halafu kila mtoto anakula kwa mama yake na kulima huko. Kwahiyo mama na watoto wanakuwa wanakulisha baba, umazunguka kula kwa zamu, bado hatujaacha hayo mambo. Umaskini wa Afrika unatokana na mwanaume wa Afrika.
 
Wengi wenu hamjui ukweli kuhusu baba yake na diamond platnum ila kuna mengi anayo yaongea ni uongo na machache yanaweza kuwa na ukweli.
Kwa mimi ambae namfahamu vizuri yule mzee na alikua jirani yangu kweli ukiwa na mzazi kama yule ni shida,kwanza mzee kutwa akishapata pesa ,anashinda kwenye vibanda vya gongo.Mzee yule akikosa pesa ya kwenda kwenye hivyo viringe anajifanya anaumwa na kumlaumu mwanae kuwa hamsaidii na mguu unamsumbua lakini yote ni uongo ana matumizi mabaya ya pesa na mnywa gongo mbobezi.kwa hiyo amegundua akilalamika kwenye vyombo vya habari wake zake wa zamani wa diamondakiwepo wema,hamisa na wengineo wanamsaidia kumpa pesa kwa huruma zao lakini kipindi hicho hawajui ukweli sahihi

Ukishamtelekeza mtoto jua umegeuka mzimu wake
 
Hebu soma hiki kisa halafu niambie huyo mtoto akaja kukua na kisha baba yake akajitokeza unadhani nini kitatokea..?

2020

18 September 2020 majira ya saa 5 asubuhi,nikiwa kazini kwangu alikuja mdada wa umri wa miaka 22(sitamtaja jina) alikuja akiwa na lengo la kutoa mimba.Ukweli sikupendezwa na hiko kitendo ukitegemea niliwahi kuapa sitafanya hilo jambo katika taaluma yangu mpaka mwisho wa pumzi zangu,lakini ikabidi nimuhoji kwanini amefika hatua ile ya kutaka kutoa mimba.

Dada alianza kueleza yeye kwao ni Makambako alikuja Dar akiwa na umri wa miaka 14 kwa ajili ya kazi za ndani,baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmoja Boss wake alikua mkarimu sana kiasi alimchukulia kama binti yake hapo basi akamtafutia sehemu ya kujifunza ushonaji na baada ya muda kwa kua binti alikua muislam na boss ni mkristu,bint alimuomba ampeleke madrassa ili asome dini yake.

Boss alikubali na akampeleka alisoma madrassa kwa mwaka mmoja huko huko akapata Mwanaume wa kumuoa alipofikisha miaka 17 akaolewa,Boss kwa kushirikiana na ndugu zake akamuozesha.Maisha ya ndoa yalikua magumu kwa jambo moja yule bwana alikua mlevi sana japo alimjali kwa kila kituila dosari ilikua ulevi na baadae akaanza mambo ya kumpiga,..baada ya kuishi kwa miaka 2 ndani ya ndoa walipata mtoto wa kike.

Siku moja alikua ameenda mjini aliporudi alikuta mwanaume amehamisha kila kitu kwenye chumba walichokua wanakaa na mbaya zaidi alikuta talaka ikiwa imeshaandikwa na hakujua mahala yule mwanaume alipoelekea na ukizingatia hata mwenye nyumba alijua tu wanahama na mkewe japo kodi yao ilikua imebaki miezi 5 kuisha,,pigo lingine ilikua yule boss wake alihamia mwanza miezi 6 tu tangu alipoolewa hivyo kwa Dar akawa hana ndugu.

Mama mwenye nyumba akamwambia akae tu pale alimpa msaada wa kumpa godoro dogo na maisha yalianzia hapo..maisha yakawa magumu kwakua hakua na kipato na kazi hana kula yake ikawa ya tabu na baada ya muda alipata kibarua cha kuuza maji kwa mama mmoja na malipo yalikua 2500 kwa siku kazi ilikua ngumu sana kwake lakini hakua na chaguo ukizingatia alikua na mtoto mdogo baada ya kuhangaika sana kwa muda mrefu kuna kipindi mtoto wake aliugua hivyo akijikuta akitumia pesa ndogo kumtibia.Akajikuta anadaiwa kodi ya miezi 7 katika nyumba akawa na hofu kubwa ya kufukuzwa lakini Mama mwenye nyumba wala hakua akipiga kelele.

Mwaka 2020 February mama mwenye nyumba alifiwa na baba yake hivyo alisafiri kwenda kwao kigoma alikaa huko miezi 2..huku nyuma alikosa msaada siku moja wakati anatembeza maji alikutana na boda boda aliyekua amemzoea sana akamwambia shida yake kua anaumwa na hana pesa yakwenda hospital anaomba amkopeshe hela na angemlipa kidogo kidogo.Yule boda boda alikubali lakini kwa sharti moja alale nae na angempa elfu 30 bila kutaka kurejeshewa.Alikubali na wakaenda kulala lakini baada ya tendo asubuhi alipewa elfu 10 na alipohoji jamaa akamwambia kubali uwe mpenzi wangu nitakuhudumia.

Mwanamke alikubali lakini ndani ya wiki moja aligundua mwanaume alikua malaya sana hivyo akaomba waachane baada ya kumfumania mara mbili,jamaa kwa nyodo akasema sawa baada ya mwezi aliona mabadiliko na baada ya kupima akajikuta mjamzito alipomfuata jamaa alikataa akasema sina mpango wa mtoto chukua 10 ukanunue vidonge utoe.Kweli yule bint akaenda kutafuta vidonge(Misoprostal) akapata kwa elfu 15 akaweka lakini aliona damu kidogo sana akajua imetoka akendelea mambo mengine lakini baada ya miezi miwili akaona bado tumbo linakua na haelewi..alipopima tena akakuta bado mjamzito akazidi changanyikiwa akamfuata tena mwenye mimba yake.

Jamaa yule alimkana kua hamjui kwani alishampa hela ya kutoa na alishamwambia imetoka hivyo akamtafute mwenye hiyo mimba,aliendelea kumsumbua mpaka jamaa siku moja akampiga na jamaa kuhama kijiwe na mtaa.Alijatibu majaribio mengi ya kutaka kuitoa lakini ikashindikana hivyo alijichanga na ilipofika elfu 18 akaja kituoni ninapofanya kazi kujaribu.Aliponieleza hayo nikamuhurumia lakini bado sikumuamini nikamwambia mimi sitoi mimba na hapa haturuhusu kutoa mimba na kwakua umejaribu kuitoa hiyo mimba bila mafanikio usiitoe fanya uzae..alibembeleza sana ila nikasimamia msimamo wangu.Nilimpa elfu 5 kumuongezea pesa akaondoka.

Baada ya siku nne akarudi tena akiwa analia nimsaidie hana ndugu na maisha yanazidi kua magumu ana mtoto mdogo na bado mimba inamsumbua kisha hata kazi zake za kuuza maji za juani ni ngumu kuzurula ,,nikamwambia tena siwezi kufanya hilo jambo..nikamuuliza tena kipato chako kwa siku sh ngapi? Akasema 2500 ndo anayolipwa nikamwambia basi aache kutembeza maji mimi nitakua ninampa kila wiki elfu 30 kama pesa ya kujikimu.,ikiwemo na kumlipia kodi ,hapo akakubali nikaanza kumchunguza kidogo kidogo nikakuta kweli ana maisha magumu kuliko yale aliyonihadithia nikamuanzisha clinic kituoni kwetu ila jambo nina hofu nalo ameandika jina langu la kwanza kama jina la baba(na nilipohoji akanambia kwake ni kama shukrani na kwa kua mtoto hana baba basi jina langu lingefaa)..Mwezi wa kumi na moja zilinyesha mvua nyingi nyumba anayoishi iliporomoka akawa hana pa kukaa nikamshauri aende kwao akajifungulie na kipindi hiko chote mama ake na ndugu zake niliwasiliana nao wakiwa huko kijijini na wanajua yote, na sikuona busara akajifungulie huko maana najua changamoto zake,ila baada ya changamoto ya makazi ikabidi nimsafirishe hadi kwao na imebaki kumuhudumia kila ninapoweza.

Kufupisha stori .Jambo hili ndugu zangu staff wenzangu na marafiki wengine wanajua ila sijawahi mwambia mpenzi wangu kwakua yuko mbali ila akirudi nitamueleza kila kitu..nilishangaa kujikuta tu nafanya yote hayo lakini nina furaha nimeokoa maisha ya yule mtoto na tunatarajia mwezi huu ajifungue salama.Sijui ni kwa vipi itakuaje kuhusu baba yake mtoto lakini mimi kwa kiasi fulani najisikia amani nimetimiza majukumu yangu na huko alipo nadhani baada ya kujifungua atamlea vyema na nitatoa msaada kadri ninavyoweza japo sina kipato kikubwa.

Yapo mambo mengi yaliyotokea kwa mwaka 2020 lakini hili ndo jambo la kwanza nimelipa uzito mkubwa sana.

Nb:Sijasimulia kisa hiki kujisifu ila nimeona nishee nanyi ndugu zangu wa humu ili kama kuna mahala nimekosea nielezwe na pia kutoa angalizo kwa wanaume wanaokataa mimba zao ni wanasababisha matatizo makubwa sana kwa wasichana.

#Ndefu ila tuvumiliane
 
Ila yote kwa yote inabidi asamehe tu Bwana Almasi hakuna namna itabaki kua wana uhusiano wa damu.
 
Tatizo ni uelewa wa mtu, na msimamo huwezi kukubali maisha ya mzazi kuishi na kijana mwenzio tena kwenye paa la nyumba yako. Vilevile si lazima ulipe au ukumbuke yaliyo kwisha pita, you need to be very smart yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Mwisho hakuna mtoto aliezaliwa bila Baba.
 
Hebu soma hiki kisa halafu niambie huyo mtoto akaja kukua na kisha baba yake akajitokeza unadhani nini kitatokea..?

2020

18 September 2020 majira ya saa 5 asubuhi,nikiwa kazini kwangu alikuja mdada wa umri wa miaka 22(sitamtaja jina) alikuja akiwa na lengo la kutoa mimba.Ukweli sikupendezwa na hiko kitendo ukitegemea niliwahi kuapa sitafanya hilo jambo katika taaluma yangu mpaka mwisho wa pumzi zang

Kuna watu wabaya sana, hakika wanapaswa kupewa haki inayowatakiwa
 
Mzazi ni mzazi tu...
Kutosamehe ni dhambi na huwezi kumuazibu mzazi.

Hata umsamehe hakuna mabadiliko ndani ya moyo zaidi ya unafiki, amini ninachokuambia.

Mzazi ni mzazi ndio hakuna anayekataa, kama aliona wajibu basi watoto wataona wajibu, kama hakuona wajibu asilaumu watoto wasipoona wajibu.

Ushaambiwa mwana wa nyoka ni nyoka
 
Back
Top Bottom