Diamond ni mchawi, achaneni naye!

Diamond ni mchawi, achaneni naye!

Mond ni leval nyingine nimezunguka mataifa kadhaa lakini sehemu zote hizo nyimbo za mondi zinapigwa na ndo msanii pekee wanayemfahamu kutoka Tanzania.
 
toroka uje mjini,
Samahani mkuu Ni kweli aje ni nzuri ila zaid ya nyumbani kwako umeusikia wapi tena hiyo AJE? Napengine ata haipo kwenye playlist yako
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Uchawi wake unamsaidia anaingiza pesa
Sio wachawi wa kutafutana usiku
Heri uchawi wake
 
Diamond ana sauti mbaya. Vocal bwana anazo King Kiba na ana kipaji zaidi cha kutengeneza muziki mzuri kuliko Diamond. Nyimbo za Diamond ni mbaya na hazipendezi masikioni.

Baada ya yeye kutoa ngoma mbovu hapo juzi aliyoiita 'Baba Lao' ambayo haina chochote cha maana kimuziki zaidi ya kelele zisizotoa msisimko wowote Ali Kiba alifuata na ngoma kali mno inayokwenda kwa jina la 'Mshumaa'. Barnabas, Ommy Dimpoz, Aslay na wataalamu wengine wa masauti na muziki kwa ujumla wameusifu na kuupromote sana wimbo wa King Kiba kuwa ni moto wa kuotea mbali.

Lakini mbaka sasa wimbo mbaya wa Diamond umekwenda zaidi YouTube. Upo namba moja kwenye trending na tayari una views zaidi ya 2M wakati hata ngoma kali zaidi 'Uno' ya Harmonize iliyotoka siku zaidi ya nne kabla ya wimbo wa Diamond haujafika idadi hiyo ya views. Oh sorry nilisahau. Hizi views huwa ananunua. Halafu wala sio kigezo cha kupimia mafanikio ya wimbo.

Lakini waliotazama Wasafi Festival waliona namna Diamond alivyoweza kuwapagawisha washabiki waliofurika viwanja vya Posta Kijitonyama kwa kutumia wimbo wake mbaya.

Kiuhalisia hakuna msanii yeyote aliyeamsha shangwe kumzidi yeye ingawa kulikuwa na Wizkid ambaye ana umaarufu mkubwa zaidi.

Sasa Diamond anawezaje kupendwa na washabiki wengi kiasi hiki wakati uwezo wake wa kimuziki ni mdogo mno? Hata yeye mwenyewe aliwahi kusema kuwa wapo wasanii wengi mno, na wengine hata hawajatoka na hawajulikani na wana uwezo wa kuimba kuliko yeye.

Hapa Diamond alifanya vyema sana kukiri kuwa kipaji chake cha muziki ni cha kawaida mno ukilinganisha na watu waliojaliwa sauti na ujuzi wa muziki.

Unapojaribu kufikiri kuhusu hao wenye vipaji zaidi ya Diamond lisikujie jina la Ali Kiba peke yake kwenye kichwa chako kwa sababu unazozijua mwenyewe.

Ali Kiba ana sauti kuliko Diamond. Lakini hana uwezo wa sauti kumzidi Ibra Nation, Beka Ibrozama, Ben Pol n.k.

Hata huko majuu Justin Bieber ni star na anapendwa zaidi kuliko watu wenye uwezo wa sauti na muziki kwa ujumla kumzidi yeye. Kisauti Justin Timberlake, Adam Levine na wakali wengine wako juu zaidi yake lakini sokoni amewaacha mbali mno.

Kwa hiyo ni wazi kuwa sauti pekee haitoshi. Ni lazima uwe mbunifu kwenye muziki na maisha yako nje ya muziki ili uwe na soko zaidi. Zaidi ya hapo unatakiwa kuwa na mbinu mbadala za kuutangaza muziki wako.

Vinginevyo utaishia kusifiwa tu wakati wabunifu wanaendelea kukuacha mbali kwa mafanikio na umaarufu.

Sasa majaribio ya kuwashawishi watu kuwa eti Diamond hajui kuimba na kuna wakali zaidi yake kwenye swala la muziki kwa lengo la kumshusha hayana maana.

Hao wenye vocal na mashairi mazuri watu wanawafahamu lakini macho yote yapo Kwa Diamond na wengine wenye uwezo wa kawaida kimuziki. Wamiliki wa makampuni ya Pepsi, Parimatch, Niceone na wengine wanaomtumia kama balozi wao na kumpatia mpunga wa maana wanajua kuwa nyimbo zake ni mbaya.

Hata Vodacom, Coca-Cola na wengine waliowahi kumpa dili nono miaka ya nyuma nao wanafahamu kuwa Ibra Nation, Barnabas, Ben Pol, Beka Ibrozama, Christian Bella, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Mario, Aslay na wengine wana sauti nzuri zaidi ya Diamond na wana nyimbo nzuri zaidi ya zile zake.

Lakini dili wanampa Diamond kwa sababu ndiye ambaye muziki wake na habari za maisha yake binafsi ni dili kuliko kiumbe chochote Afrika Mashariki na Kati.

Hata wasiompenda Diamond cha ajabu huwa wanampromote mitandaoni. Mara ooh ameiga wimbo wa mtu, mara ngoma yake hii ni mbaya wakati nyimbo mbaya na zinazoibiwa zipo nyingi lakini za kwake huwa zinaongoza kujadiliwa.

Hii yote kwa sababu Diamond ni mchawi. Na uchawi wake ni ubunifu alio nao. Kumchukia Diamond na kutegemea anaweza kushushwa na binadamu ni kujipa maumivu ya kipumbavu.

Mimi nilikataa upumbavu huu miaka mingi mno. Nawasihi na nyinyi pia, achaneni na Diamond. Huyu jamaa ni mchawi.
Gazeti.... Hahahahahahaaaa
 
Ukitaka kumsaidia mtu afanikiwe mpe mfano wa Alikiba na Diamond.

Alikiba ana sauti nzuri anatunga vizuri ila tatizo lake kubwa na linalofanya asifike alipo Diamond ni tabia ya kujiona mfalme, kujiona yeye anapaswa kukimbiliwa, kujiskia na kuvimba.

Diamond sio muandishi mzuri ila anajua kucheza na akili za watu,anaheshimu mashabiki wake, anawalilia na kuwafanya wajione wanamsaidia, ni mnyenyekevu na anatangaza kazi zake kama vile ni msanii chipukizi. Diamond hana kiburi. Watanzania wengi wanapenda kunyenyekewa na ukilijua hilo utawapata sana.
Kizuri chajiuza bro acha king avimbe anaijua thamani yake... Diamond acha ajitembeze anajijua pia mzee.. usifos B iwe A
 
Me nashangaa sn hizi story za kiba hamuwez diamond mwaka wa tano karibu miaka yote hiyo hamjampata anaemuweza mumshndanishe na huyo diamond??.. Kuna jux,Ben pol(king'ast mkomavu) barnaba,belle9 why always kiba?..NAONA KUNA TATIZO MAHALI.
 
Back
Top Bottom