Diamond: Niliwatolea nje Roc Nation ya Jay-Z

Diamond: Niliwatolea nje Roc Nation ya Jay-Z

Yaani kwa hiyo diamond anatuambia salama Na tale Na felaa wana network ya kumwezesha yeye kufanikiwa kuliko Jay z huyu Wa Beyonce yaani amekataa kufanya kazi Na rihana DJ khaled Jay z hayo malengo gani yeye aseme washauri wake bila yeye hawatoboi tena kwa hiyo hawatamshauri vizuri zaidi ya wcb tu ila nao mkono uende kinywani hila hakuna mafanikio yoyote ata hao akina Chris Brown Drake rihana nao wanasimamiwa Na label kubwa japo ni mastaa wakubwa Na wameshafika malengo
 
Diamond Platnumz alitosa kusainishwa na label inayomilikiwa na Jay Z, Roc Nation

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, staa huyo alisema hiyo ni moja tu ya label kubwa za Marekani alizozitolea nje. “Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata wakitaka wanisaini,” alisema Diamond.

“Acha Roc Nation kuna baadhi ya record label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi, wananifuata na ofa,” aliongeza.

“Lakini kila kitu ni target, mimi siku yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili upate hela, ukanye show yeye anafaidika na nini?”

Kingine Diamond alisema kama ni msanii mkubwa inakuwa rahisi kupata collabo za aina hiyo.

“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki wangu uuzike kama wanavyouza akina Jay Z, Kanye West. Sitoingia eti Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri.”
kijana ana akili sana japo wenye wivu humponda
Interesting
 
Aise wewe ni ******** dogo ...sasa ukinitukana ndo utabadilisha mawazo ama alichokisema mr diamond? Kipi ambacho kimekukera sana we masikin had unatukana watu usiowajua...mana kama umefikia hatua ya kutukana kisa thread bas una mawazo ya kimasikini sana ..jibu kwa hoja ama pinga kwa hoja ...najua kejeli zipo lakin sio matusi..nikiamua kukufatilia wewe dogo nafikir unaweza kua mfano, sijawa chokoraa ktk maisha yang so nakuonya kwa mara ya mwisho.
Msamehe mkuu, nadhani amejua kosa
 
Nilivomuelewa jamaa yeye hataki kua akisainiwa aingiliwe katika anachofanya ama kuongozwa na label ambayo atasainishwa nayo,anataka afanye kaz mwenyewe bila kuingiliwa (which is impossible) anataka tu wamsaidie muziki wake ukue kidunia, pengine ameona mifano kama lil wayne bifu lake na birdman kuhusu hayo hayo mambo had saiv wana kes mahakaman..we unataka album itoke siku flan lakin recod label yako wanakuambia bado muda subiri...mfano mwingine ni davido hadi akawa anaonesha stress zake kwenye media, ila ku-turn ofa ya jay z mhhhhhh...
 
Binafsi naamini, tukiacha wivu na kujidharau, ukweli Diamond anashine sana, ananyota kali.. So far amafika mbali sana, na anatupeleka mbali sana.

Hivi utafananisha zama za hapo kati na hizi za kwake? Anabidii na Kazi yake, kuna kipindi alitangaza kua hafanyi kazi jukwaani bila 10mil kuna watu waliongea sana, ila leo wako wapi?

Ifike mahali tukubali kua tunazidiana, wewe ukijua mbele wenzako wanajua nyuma. Najua wengi wanabeza kwa kufikiria kua Jay Z ni Mungu flani hivi.

Kazana Diamond.. Utafika Mbali.. Hawa wa kutembea na bahasha za kaki achana nao
Umetoka nje ya mada
 
Sioni ajabu kwa sababu Jay Zee ni mtu mdogo sana ukilinganisha na kina Richard Turnbull,Donald Cameroon lakini walikuja Africa na kutafuta watu wa kuwatimia katika malengo yao.Jay Zee ni mfanyabiashara na Diamond ni bidhaa kwa hiyo si kitu cha ajabu kuona Jay Zee akitaka kupata faida zaidi kupitia Almasi Platinum.Kinachomdatisha Jay Zee ni followers na Africa inakuja juu sana katika biashara ya music.Bila kusahau Illumin.....ati
Followers youtube au insta??
 
point taken unamawazo makubwa sana bila shaka ulikua wa kwanza darasani Big appreciate

watu wanamuona j zee km mungu vile wamesahau kua hata mbuyu ulianza kama mchicha

mwacheni bwana almasi afanye yake kwanza HAPPY BIRTHDAY TO HIM
Wewe ni mtaalamu?Ulijuaje kuwa nilikuwa nashika namba moja?[emoji4] Umetisha.
 
Yaani kwa hiyo diamond anatuambia salama Na tale Na felaa wana network ya kumwezesha yeye kufanikiwa kuliko Jay z huyu Wa Beyonce yaani amekataa kufanya kazi Na rihana DJ khaled Jay z hayo malengo gani yeye aseme washauri wake bila yeye hawatoboi tena kwa hiyo hawatamshauri vizuri zaidi ya wcb tu ila nao mkono uende kinywani hila hakuna mafanikio yoyote ata hao akina Chris Brown Drake rihana nao wanasimamiwa Na label kubwa japo ni mastaa wakubwa Na wameshafika malengo
Unatakiwa ujue maana ya neno mafanikio ndio uanze kulipuka.Mafanikio si utajiri au mali pekee bali hata kufikia malengo binafsi.Sasa kama hiyo Roc nation haipo kwenye malengo Pla TZ De Monde ni lazima akubali?Kwani hujawahi kuona mtu ambaye kwao kuna mali nyingi lakini amejikita katika kufanya biashara zake hata kama ni ndogondogo?Hiari hushinda utumwa.Jitambue ndugu yangu.
 
Sasa shida nn asiseme anacho penda kwani jayz ndo nani duniani safi chibuu komaa kuna watu wapenda mtelezo wangapi mziki wao umebuma mbayaa
Angekua kakataa colabo hata mim ningemuona boya mwacheni ajisimamie mwenyewe
 
Back
Top Bottom