Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Dar es Salaam. Msanii wa muziki wa bongofleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema endapo sheria itamtaka kubadilisha ubini wake anaotumia sasa atafanya hivyo
Ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya Sanura Kassim maarufu mama Dangote ambaye ni mama mzazi wa msanii huyo, kusema baba halisi wa mwanaye ni Salum Iddi Nyange na si Abdul Juma ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifahamika kama baba yake.
Baada ya mama yake mzazi kusema hayo Abdul Juma ambaye alikuwa akijulikana kama baba mzazi wa mkali huyo wa bongo flava alimtaka kuacha kutumia jina lake kama ubini.
Akizungumza leo katika mahojiano kupitia kipindi cha The Switch kinachorushwa na Wasafi Fm, Diamond Platnumz amesema suala la kubadilisha jina limekaa kisheria zaidi.
“Nafikiri ni la kiserikali zaidi na wanasheria wanaweza kulizungumzia suala hili mimi sina tatizo, wakisisitiza hili kisheria sina tatizo kabisa,” amesema Diamond
“Lakini siku zote nitaendelea kumuheshimu kama mzee wangu, kumpenda kama mzee wangu na kumsaidia atakapohitaji msaada kwani hata baada ya kupata taharuki sikuachaga hizi huduma kila niposikia kuna hili na hili natakiwa kufanya,”
Amesema hata alipojua kuwa mzee Abdul siyo baba yake miaka mingi nyuma hakubadilisha wala kumfanya amchukie kwa sababu ni suala la kawaida.
“Kitu ambacho kipo ni mimi na yeye hatukupata ukaribu sana,”
Alipoulizwa kwanini hajabadilisha hadi sasa alijibu kuwa hakutaka kuleta taharuki ya kubadili jina kwa haraka kwa sababu tangu amezaliwa amekuwa akitumia jina hilo.
“Hili ni jina (Naseeb Abdul) ambalo tangu nimezaliwa nimekua nalo sikutaka kuleta tena mambo ya haraka ni kama ushamba,” amesem.
Chanzo: Mwana halisi