Diamond Platinumz amiliki gari ya thamani kubwa


Unaposema msaada kwa jamii sijui unamaanisha nini ndugu..tuache kutumia maneno ndivyo sivyo...hivi wewe umeisaidia hiyo jamii kwa kiwango gani ? au unadhani wewe ndio unapata thawabu zaidi ya Diamond kwa kuwa tu yeye kanunua V8 na wewe hujanunua ?...

Hata hao wafalme kina Suleiman walikuwa wanamiliki dhahabu za thamani kubwa..sasa je kwa tafsiri yako wao hawakuwa na thawabu ndani ya jamii zao ?

Ngoja nikwambie kitu ndugu...kuna uwezekano kuwa Diamond ana faida kubwa kwa jamii yetu kuliko uwepo wako wewe usiyenacho..kwani yeye kwa kutumia pesa alizozivujia jasho kwa kujituma na sasa kwa kununua hiyo V8 amechangia pakubwa kupitia kodi ya kununulia hiyo V8 kuliko wewe uliyeishia kununua jiko la mchina...na bado ataendelea kulipa road licence na mengine mengi kuchangia mfuko wa taifa watu wapate dawa maji na barabara.

Pia tusijidanganye kuwa kuisaidia jamii ni kupitia pesa peke yake....je wewe kwa upande wako umefanya mangapi ? au unasubiri hadi upate pesa kama za Diamond ? ni lini umechukua jembe ukaenda shambani ukalima na baada ya kuvuna ukaenda kutoa hayo mazao kwa jamii isiyonacho ? au kwako huo utakuwa sio msaada ?

Nadhani mnaostahili kuwahoji na kuwawajibisha zaidi ni viongozi wenu waliokuja kwenu na kuomba muwachague kwa ahadi kuwa watazimaliza shida zenu badala yake wanaishia kuzitumbua hizo pesa zetu wote kwa kulipana posho, kuandaa semina zisizo na vichwa wala miguu na safari za nje za kila siku.... badala ya kuishia kumlaumu mtu aliyechuma kwa jasho lake na kutaka awasaidie hata wale wasiojitumikisha.

Kusaidia kwake inabaki kuwa ni hiyari zaidi kuliko wajibu.

Mwisho wa siku Diamonda anatuburudisha....weye je ?
 
Kweli kila kitabu na zama zake,siku hizi kuvaa sarawale za vitambaa vya kushona magauni ndio fashoo,ingekuwa zamani huyu bwana angeitwa mtoto si riziki
 
Unajua maana ya PLC!?
Kwani kuna benki Tanzania ambayo sio PLC??

1. Sio bank zote ni PLC; PLC ni CRDB, NMB, DCB na KCB tu.
PLC - Public Listed Company maana yake ni kampuni ambayo imesajiri mtaji wake kwenye soko la mtaji, kwa Tanzania tuna DSE, ambapo kila mtu (Public) anaweza kununua hisa na kuwa mmliki wa kampuni hiyo.

2. Benki nyingi zimebadilisha majina kwa kuondoa virefu, so CRDB, KCB, DCB, DTB, NBC, NMB ni stand alone names, sina uhakika kwa benki kama BOA, BBT, SCB etc na zinginezo.

NOTE: NBC Bank Limited inatumika interchangeably na National Bank of Commerce so do NMB to National Microfinance Bank.

CC: Moudy Boka
 
Asante kwa taarifa mkuu Kanigini, tole shihamo nkoyi.
 

Ahsante,waambie hao wamezidi WIVU,fanya yako Diamond mia mia.
 

WIVU mbayaaaaaaaaaaaaa!haa haa
 
Tatizo mnapamba sana! Hongera yake ila hiyo gari siyo mpya ina number B ya mwaka juzi, inamaana amenunua kwa mtu, pia hiyi haifiki thamani hiyo, mpya ni 120 - 160.
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…