Diamond Platinumz ampa milioni 10 Mzee Makosa, aliyekuwa tajiri mkubwa Iringa na kufilisika

Diamond Platinumz ampa milioni 10 Mzee Makosa, aliyekuwa tajiri mkubwa Iringa na kufilisika

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Staa wa muziki Bongo, Diamond Platinumz leo amekutana na Ramadhani Kasawa maarufu Kama 'Mzee Makosa' ambaye alitamani Kukutana nae baada ya kutazama interview yake kwenye mitandao ya Kijamii akielezea namna alivyofilisika kutoka kwenye Utajiri wakutupwa aliokua nao.

IMG_0454.jpeg
Soma, Pia: Anaefahamu Makosa, aliyekuwa tajiri mkubwa Iringa mwambieni Diamond Platnumz anamtafuta ampe sadaka yake

Diamond kutokana na Kuguswa na Mahojiano Hayo ya Mzee Makosa alitamani Kukutana na Kuzungumza nae Pamoja na Kumshika Mkono kwa Chochote atakachokua amejaliwa.

Hivyo Mapema Leo ameweza kufanikiwa kukutana na Mzee huyu Maarufu kutokea Mkoani Iringa, ambapo Licha ya Kupata wasaa wa kuzungumza nae kuhusu Maisha Lakini Pia ameweza Kumshika Mkono kwa Kumpatia Kiasi Cha Tsh. Milioni 10.
 
Hingerackwa Diamond kwa hilo alilofanya,na kwa kusikiliza tu hayo mahojiano mafupi,mzee anaonekana yuko timamu na atarumia pesa hizo kwa busara na yawezekana akachomoka kimaisha tena.Mungu amsaidie.
 
Akizingua na hio anafilisika.
Hahaaaa, mwenzangu na mimi ukipoteza elf 50 tu umefilisika.
 
Milioni kumi, kumrudishia utajiri ni ngumu.

Hapo labda angekuwa na kitu anafanya kwa jamii halafu hiyo ikamuongezea mtaji hapo sawa.

Tofauti na hivyo sijui tumshauri tu awekeze vipande ajilie pensheni maaaaaana mmmmmmh! Utajiri ni kutoa sio kupokea
 
Huyu mzee miaka ya 2007 alikuwa na mgahawa pale jirani na maktaba kuu, alikuwa anazaa na wafanyakazi wake, kila akiajiri pisi lazima iwe yake kwanza sisi tulikuwa tunakula makombo tu.
Alikuwq na vyombo vya muziki nakumbuka walikuwa wanafanya mazoezi siku moja hawakuwa na muimbaji nikajitosa kuimba Dunia tunapita ya samba mapangala na vile wale wanamuziki nilikuwa nikienda pale luxury bar siku wanapiga napanda kwa stage kuimba copy kumbe wakamwambia mchukue huyu bendi itasimamaa aliponiomba nibaki atanilipa nikaja zangu dar sikurudi tena ila Waliona kipaji changu nami nikapotezea labda leo ningekuwa mbali sana Big up modi
 
Back
Top Bottom