Staa wa muziki Bongo, Diamond Platinumz leo amekutana na Ramadhani Kasawa maarufu Kama 'Mzee Makosa' ambaye alitamani Kukutana nae baada ya kutazama interview yake kwenye mitandao ya Kijamii akielezea namna alivyofilisika kutoka kwenye Utajiri wakutupwa aliokua nao.
Diamond kutokana na Kuguswa na Mahojiano Hayo ya Mzee Makosa alitamani Kukutana na Kuzungumza nae Pamoja na Kumshika Mkono kwa Chochote atakachokua amejaliwa.
Your browser is not able to display this video.
Hivyo Mapema Leo ameweza kufanikiwa kukutana na Mzee huyu Maarufu kutokea Mkoani Iringa, ambapo Licha ya Kupata wasaa wa kuzungumza nae kuhusu Maisha Lakini Pia ameweza Kumshika Mkono kwa Kumpatia Kiasi Cha Tsh. Milioni 10.
Hingerackwa Diamond kwa hilo alilofanya,na kwa kusikiliza tu hayo mahojiano mafupi,mzee anaonekana yuko timamu na atarumia pesa hizo kwa busara na yawezekana akachomoka kimaisha tena.Mungu amsaidie.
Huyu mzee miaka ya 2007 alikuwa na mgahawa pale jirani na maktaba kuu, alikuwa anazaa na wafanyakazi wake, kila akiajiri pisi lazima iwe yake kwanza sisi tulikuwa tunakula makombo tu.
Alikuwq na vyombo vya muziki nakumbuka walikuwa wanafanya mazoezi siku moja hawakuwa na muimbaji nikajitosa kuimba Dunia tunapita ya samba mapangala na vile wale wanamuziki nilikuwa nikienda pale luxury bar siku wanapiga napanda kwa stage kuimba copy kumbe wakamwambia mchukue huyu bendi itasimamaa aliponiomba nibaki atanilipa nikaja zangu dar sikurudi tena ila Waliona kipaji changu nami nikapotezea labda leo ningekuwa mbali sana Big up modi