Sote tumeangalia majuzi wakati Diamond akiwa ni mmoja wa wa wanamuziki wachache Afrika walijinyakulia tuzo nyingi kule SA kwenye TV ya Channel O. Ni mwanamuziki wa kwanza kutoka Tanzania, sijui katika nchi za jirani, kujizolea tuzo tatu nje ya nyumbani kwao kwa mpigo katika event moja. Anatakiwa kupongezwa sana na watanzania wote hata wanaomchukia kwa sababu binafsi: ni lazima tujifunze kutenganisha maji na mafuta.
Tuzo hizo alizopata zimemuinua na kumpa power fulani katika jamii hii. Ni muhimu kuangalia tena kuwa Diamond ana sifa nyingi sana nzuri na vile vile sifa nyingi sana mbaya kwa jamii, mbaya zikiwa zinatokana zaidi na utoto. Kwa vile power huja na responsibility, ninawaomba washauri wa karibu na Diamond wamfundishe aweze kuchangia kama role model katika jamii hii ambayo imaevurugwa sana na wanasiasa wetu wenye ubinafsi. Role model siyo kutoa michango na misaada tu kama ambavyo wasanii wengi hufanya; ni pamoja na kufanya kazi zao ziwe za kufundisha jamii hata kama hazilipi sana- ni swala la kuchanganya tu. Vile vile ni kuhakikisha kuwa matendo yao binafsi yale wanayofanya hayatakuwa na madhara kwa wale watakaowaiga. Mwisho zaidi ni kujifu\za kuwa-accomodate watu wa namna nyingi hata wale wanaopingana nao; after all ukishafika juu huna haja ya kushindana na aliye chini yako.
Just my few words to our Diamond's success