Wakati anatoka na album yake ya kwanza na hit song ya nenda kamwambie sikumwelewa sana nilijua ni upepo utapita, hata ntarejea nilidhan kabahatisha bila kusahau mbagara niliielewa lakini nikaona album ya kwanza wengi uwa wanafanya vizuri.
Baadae likaja bifu kati yake na producer wake wa awali bob jr nikaona dogo ndo mwisho wake ila kumbe ndo kwanza safari inaanza yani kama ni series tungesema ndo kwanza tuko epsode ya tatu kati ya epsodes 85 za series nzima.
Nikasikia kitu Regreema, sijui nimepatia kwenye lile goma alilopika producer Lamar lijulikanalo kama moyo wangu. Ngastuka, machale kundesa !!!! Nikaona huyu kijna kumbe hana utani na video safi plus madansa na madam sepetunga pale katikati nikaoni huyu kijana is here to stay.
Sijakaa vizuri nikaona teaser ya mawazo akiwa na watoto ambao kwa wakati ule walionekana ni level mbaya si rahisi kuwatumia kama ma video queen nkimaanisha jokate na lisa jensen. Duuh nikazidi shangaa huyu dogo mbona anajua sana hivi.
Mara mambo ya tour wapi sijui kitu kikaja kizai zai, mara lala salama akaja nimaliza na UKIMUONA, huu wimbo ni mkali sana. Wakati umetoka kuna mnigeria, mcameroon na mrussia walikuwa kila wakaniona nakuwa nausikiliza hadi wakaupenda wakaniomba niwawekee kwenye laptops zao.
Kumchukia huyu kijana ni kutafta maradhi ya moyo