Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

Mi nishawapuuza, sioni ni kwanini niendelee ku argue nao. Jamaa hawaongelei vitu vinavyoonekana utadhani wanaishi nchi ya kusadikika ya mfalme Juha.
Don' worry wangu, muda si mrefu, msimu wa tuzo unakuja! mambo ni full facts with figures! Awali ilikuwa oh, Diamond anabebwa, cku hizi kimya! Mara oh, anatembelea nyota za mademu... watu tukawapa uchambuzi wa haja kuonesha ni namna gani hao mademu ndio wanaotembelea nyota ya Diamond tofauti na madai yao hafifu, yasiyo na weledi wowote wa uchambuzi na hatimae hivi sasa hawasemi tena upuuzi huu baada ya kuona yule waliyedai ndie Diamond anatembelea nyota yake anaanza kufifia taratibu na Zari ambae alikuwa hafahamiki amekuwa ndo talk of East Africa like never before!
 
kujifanya mashuhuri, kumbe chaka wamechakaa, aga wenzenu sisi turufu si garasaaa...wenye nyota ya umaarufu si kupapasa

akome MWANA fulani ona uso ulivyo mbojoka!
......
tena joker la nguvu kwa karata,lile hodari manguvu si kwasakwasa!
 

Huyu dogo ni level nyingine basi tu wabongo hatuna roho za upendo ndio watu wanampiga vita.....Haya mambo anayofanya miaka mitatu tu hapa yalikuwa ni ndoto kwa bongo fleva.

Mungu amzidishie naamini ataendelea kuwaprove wrong waswahili wote tusiopendana. Maana kwa sasa yupo kimya ila muziki wote unauona una gape fulani.

One day huyu dogo ataishangaza mpaka dunia sijui kwa nini naamini hivyo.
 
Wajameni ........sorry.......nauliza swali la kitaalamu............Hivi diamond anaimba mapigo gani.........yaani miondoko ipi?!Maana wadau mnachoonekana kukijua ni kwamba diamond anamba vizuri........but what kind of style au niseme ni genre gani anayoi'icon kwenye tasnia ya mziki hapa bongo...........! Mwenye ufahamu huo please step forward kunijuza please.........!
 
simply bongo flavor, manake kuna ngoma kafanya afro pop, mduara, hip hop, zouk, bolingo n.k. Since mziki wake una uTanzania ndani yake basi ana fall kwene category ya bongo flavor. Speaking of multiple genre music nafikiri ndo kipaji chenyewe especially kama unaweza kukamua kisawasawa kwene kila aina ya genre. Ila to be more specific kama utakataa kua bongo flavor sio genre, basi jamaa ni mwana afropop mzuri tu ukisikiliza ngoma zake almost zote. Unakaribishwa kwa maswali zaidi
 

Umemjibu vizuri sana kama hajaelewa basi coz nilishaandaa a stupid answer kwaajili Yake. Stupid question deserve a stupid answer!. Kichwa cha thread kinasema mashabiki wa diamond platinum tukutane hapa kwa ajili ya kumsapoti, napata ukakasi kuelewa kuwa kwa kuuliza genre ya muziki anayoifanya platinum ye itamsaidia nini? !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…