kila mtu ana haki ya kuwa chama anachokipenda yeye!' huwezi ukamlazimisha mtu. lakini yeye alichokosea angetakiwa kunadi chama chake sio kuanza kuleta mambo ya ukabila!' na kama kupiga kazi angepga kazi aache kuongea shit.
Kwa hiyo Lowasa kwa vile anatoka kaskazin hawezi kuongoza nchi!', Nchi inafaa kuongozwa tu na wakwere!' au kabila la mama yake au?! kwa hiyo amewadharau na mashabiki zake wanaotoka ukanda wa kaskazini, umaarufu umevimbisha kichwa!' na domo lake kuuuubwa!'
nilikua namsapiti sana huyu domo kubwa!' search humu utaona post zangu!' nimempgia kura sana, tena nikiwa kwa office nilikua nawahimiza sana wafanyakazi wenzangu muda ambao hawana kazi kumpgia kura mana kuna free internet!' sasa sahivi wamebaki kunicheka, mtu niliekua nampgia kampeni kila siku kumbe ni cho.ko
ENZO,
Kwanza mimi ni mtu wa Kusini na wala sina mpango na hayo mavyaama yenu coz' kwangu mimi, CCM na UKAWA wote ni wezi tu! Lakini pamoja na kwamba mimi sio mtu wa Kaskazini, of course kauli ya Diamond kwamba eti viongozi wa chama wote ni kabila moja ni kauli ambayo hata mimi alinikera na nilimchana pale pale kwenye page yake! Lakini kwanini ile kauli baadae aliifuta? Si aligundua kwamba kweli amepotoka? Hivi nyie wenzetu kwani ni malaika kwamba hamkosei?
Najua kila siku mtakuja na sababu... leo mtasema kaleta ukabila, kesho mtasema amewakashifu watu wa upinzani, mtondogoo mtasema amewakashifu wanawake... kila siku mtakuja na jambo coz' yote hayo si kisa cha ugomvi wenu bali ugomvi wenu ni siasa... kwamba, amekipigia kampeni chama cha wengine na sio chama chenu. Nitarudia tena na tena, hayo mtakayo nyinyi hayawezekani na ndio maana nikasema kwa staili hii mtakuja kuwawatukana hata mama zenu waliowazaa indirectly ili mradi tu uonekane ni mpenda mabadiliko! Manake unakuta mtu na akili zake kabisa anasema "yeyote anayeishibakia CCM ni mpumbavu tu asiye na akili....!" Hivi kweli Tanzania hii kuna familia ambayo baba, mama, shangazi, wajomba, akina dada, akina kaka, bibi na mababu, woooooooote ni UKAWA! Hivi zipo familia za hivi? Na wala usidhani kwamba mie sio mfuatiliaji wa siasa... ni mfuatiliaji kweli kweli kuliko wengi wenu! Na wakati fulani nilikuwa naandikaga hadi makala za siasa kwenye weekly newspapers na ndio maana si upinzani wala CCM wanaoweza kunishikia akili... wote ni wale wale tu!! Nitakaa kusubiri 26/10 largely kwenda kutimiza haki yangu but I do expect nothing from any of them but from my own struggles and hustles!
Wakati nyinyi mnaamini watu kama sisi ndo kikwazo cha mabadiliko; mimi naamini watu kama nyinyi... mashabiki wa CCM na Upinzani ndo kikwazo cha mabadiliko ya kweli! Huwezi kuwa na wananchi wanaoongea lugha moja na wanasiasa halafu hiyo nchi ikawa na mabadiliko, NEVER! Hapawezi kuwa na mabadiliko coz' majority ya wanasiasa wanatoa priority kwa mambo yenye maslahi ya kisiasa, kiutawala na yao binafsi kuliko maslahi mapana ya taifa! Hadi wananchi wa kawaida mtakapokuja kugundua kwamba akina Mnyika, Mbowe, Nape, Kinana na wengine kama wao wapo kazini na wanataka kuwatumia nyinyi kufika ofisini, ndipo nchi hii itakapokuja kupata mabadiliko ya kweli!! Ikiwa wewe ni kiongozi wa kisiasa... I will understand you kwa 100% coz' na wewe utakuwa kazini!