Take this 'HARD WORK PAYS'' and thas DIAMOND.
Hard Work pays, hilo halina ubishi lakini mwenye mapenzi (sio ushabiki) na Diamond hawezi kufurahia hata siku moja kuona mtu wake anaingia kwenye mabifu yasiyo na tija... watu tunao-dis hii kitu kuna wengine wanadhani tunamtetea Davido kumbe tunamtetea mtu wetu asijiingize kwenye mambo yasiyo na tija! Leo hii mashabiki wa Kiba hapa Bongo hata wamchukie vipi Diamond bado haitamuathiri coz' tayari Diamond ana mashabiki kibao nyuma yake hapa TZ! Hali kadhalika, leo hii mashabiki wa Diamond hata wamchukie vipi Kiba, haitamuathiri Kiba coz' tayari ana mashabiki kibao nyuma yake! Kuna watu leo hii wanamchukia Kiba kwa sababu tu wao ni watu wa Diamond na kinyume!!!Tutake tusitake, mashabiki wa Diamond wanaishia kwenye mipaka ya East Africa!
Wakati mashabiki wake wanaishia East Africa, hivi sasa ndio alikuwa anajenga base kwenye maeneo mengine ya Africa, hususani NIgeria! Leo hii nitakuwa mtu wa ajabu sana nikikataa ukweli kwamba featuring yake na Davido ndiyo iliyomfanya atambulike nchini Nigeria na sehemu zingine Afrika! Wakati haya yanatokea, Diamond sio msanii wa kwanza TZ kufanya featuring na wasanii wa Nigeria... wapo AY, Mwan-FA na Ommy Dimpoz! Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua tofauti ya featuring za akina Dimpoz na hii ya Diamond... wakati za wenzake zilibaki kama ushirikiano wa kikazi tu, hii ya Diamond ikageuka ikawa ushikaji!
Kwa upande mwingine, kuna mashabiki kibao TZ ambao walimfuata Chibu kwavile tu wao wana mahaba na Wema na kv Wema na Diamond walikuwa ni dam dam, nao wakapeleka mapenzi yao na kwa Diamond vile vile! Hali kadhalika, wapo mashabiki kibao ambao walionesha love kwa Wema lakini root ya mapenzi yao ilikuwa kwa Diamond! Ukiangalia ukweli huo, bila shaka wapo mashabiki kibao wa Nigeria ambao walianza ku-show love kwa Chibu kwavile tu wao ni mashabiki wa Davido na kwa kuwa Davido na Chibu wanaonekana ni washikaji wakapeleka mapenzi yao kwa mshikaji wa mtu wao... kama ambavyo hivi sasa wabongo wanavyoonesha love kwa Zari!!
Kama ilivyotokea kwa mashabiki wa Wema ambao walikuwa wanaonesha love kwa Chibu kwa ajili ya Wema na sasa kuwa maadui wa Chibu kwavile tu Wema na Chibu sasa si wamoja... ndivyo hivyo itakavyotokea kwa mashabiki wa Davido ambao waliamua ku-show love kwa Chibu kwa ajili ya Davido na ikiwa kutakuwa na chuki kati ya Davido na Chibu, mashabiki hawa hawatakuwa tena na sababu ya ku-show love kwa Chibu!
Mashabiki wa Wema hata wakiamua kumgeuka Chibu bado Chibu hawezi kutetereka kv tayari ana base ya kutosha hapa East Africa... lakini kule Nigeria, hiyo base Chibu hana... ndo kwanza alikuwa anaanza kuijenga!
UKiangalia ukweli huo, mtu mwenye mapenzi ya dhati kwa Diamond hawezi kufurahia kuona uhasama huu wakati ndo kwanza alikuwa anaanza kujenga base kule Nigeria! Anaweza kufanya featuring na other Naijas lakini Chibu na Davido ilikuwa ni zaidi ya uhusiano wa kikazi!!! Leo hii naona mashabiki wa Diamond na wale ambao wala sio wa Diamond wanafurahia... tukubali tusikubali, wala hatumsaidii!! Hawa hawa ambao leo hii wanajifanya kum-support Chibu wakati huko nyuma wala hatujaona wakim-support zaidi ya kumponda, ndio kesho watageuka kuwacheka nyinyi ambao mmekuwa mkim-support Chibu since then!!
Niishie tu kusema kwamba, waungwana wanashabikia kujenga na sio kubomoa! Hakuna ubishi kwamba Diamond ni hard worker but unless kama tunaamini nchi hii tangu ianze hajatokea hard worker kweney sekta ya muziki zaidi ya Diamond, ndipo tunaweza kuwa na kiburi na kutamba it's only his hardworking ndiyo imemfikisha pale alipo!