Niwasalimu wote..... Amani ya bwana iwe nanyi.....
Najua duniani na kwingineko kwingi ligi mbalimbali zimesimama kutokana na jinamizi la covid 19
Huwa natamani kuona timu yetu ya Taifa na klabu zetu za soka Tanzania zikifanya makubwa Africa. Na ndio maana nikaja na huu uzi "Diamond Platinum FC"
Ingetokea matajiri wawili au mmoja ili kufanya "Football revolution in Tanzania" zikatengenezwa timu nyingine mbili nzuri zitakazo endeshwa kisasa. Achana na Azam FC inasadikika pale kuna u father na udini
Kwanini tusiwe na timu ambazo zitaendeshwa kisasa timu ambazo hata refa akileta usimba na uyanga ukizifanyia figisu figisu zitaibuka na zitashinda uwanjani
Ziibuliwe timu ambazo kwa kupenda au kutokupenda watu watajikuta wanazipenda na kuzishabikia....Nimesikia sikia fununu diamond platinum anataka kuanzisha timu ya mpira
Ni kwanini soka la bongo limekua "Domant" kwanin kusifanyike transformation ya soka Tanzania. Ni nini kinacho tukwamisha? Ni jinamizi gani? Huwa najiuliza matumbo ya mama zetu na dada zetu yameacha kuzaa vipaji?