Diamond Platinumz vs Ali Kiba, nani mkali?


Chipa Gm nawewe ni timu gani mkuu?
 
Wasanii waache wivu na badala yake wajifunze kutoka kwa diamond.....diamond ameonyesha ndoto zetu zaweza kutimia bila kujali mtu ametokea au kuzaliwa wapi...miaka mitano iliyopita ilikuwa ndoto kwa msanii wa kibongo kuwa nominated tuzo ya BET lakini diamond ameonyesha inawezekana....so nadhani Ally Kiba na wengine wote tunajua wana vipaji na wanafanya vizuri lakini nadhani badala ya kumuwekea chuki diamond ni vyema wakajifunza ni kitu gani diamond anafanya ambacho wao hawafanyi mpaka anafanikiwa kiasi hicho....binafsi ningependa kuona kila msanii anafikia mafanikio kama ya diamond kwakuwa kipaji kinalipa sana pengine hata kushinda madarasa.....ieleweke lakini kipaji kinashinda madarasa na si elimu
 
Halafu mimi sidhani kama wana ugomvi, haya mambo yote yanachochewa na vyombo vya habari na mashabiki..,mfano juzi kwenye kipindi cha Sporah Show ,sporah alitumia muda mwingi kumuuliza Kiba kuhusu kutokuelewana na diamond halafu muda mchache kuhusu muziki wake...Huoni kama hizi media zinachangia kuwagombanisha? Na mashabiki wachache wasioweza kufikiri sawasawa hasa zile timu zilizoko instagram.
 
Habari za asubuhi wanajamii
Nimekua nikifuatilia habari za wasanii hawa wawli siki za hivi karibuni toka aly atoe single na hasa baada ya diamonf kichkia tuzo mashabiki wamekua wakibishana sana hadi wenhine kufikia hatua ya kuongeleana mbovumbovu kwenye hii mitandao ya kijamii
Naomba wenzangu mnijibu labda mi sielewi
Lini ALY alisem anashindana na diamond?
ALY KIBA alikua kimya kwa mda mrefu sana ametoa single wiki iliyopita wakati diaomnd yupo kileleni kwa mda wote sasa inakuaje mnawalinganisha watu hawa wawili?
Hamuoni kwamba mnachochea ugomvi usio na maana?
Ni km bile MASE kwa USA aliueamua kurudi game umlinganishe na JAY Z au KENDRICK LAMAR ambao wapo wanavuma kwa kipnd hiki
Sikatai wote wana vipaji na wote ni wazuri ila kwa miaka hii miwili kumlinganisha KIBA na DIAMOND ambapo mmoja alikua kimya ni kam vile akili tunajishusha kifikra
Mnataka tuamini kwamba kweli tuna tatizo la IQ waTZ
Tuacheni ushabiki maandazi kwa kweli usio na kichwa wala miguu.
Wapo wanaosema KIBA amepanik nyimbo yake mbaya nyie mlitaka aimbeje labda?yale ndo mahadhi yake na yeye ametoa wimbo kwa mashabiki na wala si kushindana na diamond!
Hv kuna mtu alidhani km dushelele ungevuma au mwingine"msinitenge km napenda kula"
Muda utaongea jamani tusiwapambanishe wakachukiana jamani...!
HONGERA JIDE ANACONDA,HONGERA DIAMOND.
 
Kuna watu wamepaniki na THE RETURN OF KING KIBA......Kimahesabu wanapomlinganisha Ali Kiba na Diamond automatically that means: Nataka kulewa+My no.1+nimpende nani+my no.1 remix+kitorondo+BumBum+Ukimuona+kizaizai+Rich Mavoko+Jux+Bele9+BenPaul+BobJr+Linex+Dully Sykes+Dimpoz = MWANA DAR ES SALAAM
 

hahahaaaaa....!!!mi sielewi yani watu sijui kawakosea nini kiba
 

ha ha ha MwanaDsm ndo habari ya mjini!!
 
Inashangaza sana Kiba yupo kimya 3 yrs af unamlinganisha na dai aliyetamba mda wote huo.... Hii inamaanisha Kiba ni homa ya Tanzania hakuna wa kumfikia.... Akina Ommy, Belle, Ben n.k wametoa nyimbo but bado mnamuwaza Kiba.......The Return of Kiba..
 
list yangu ya wanamzk bora..

1.Ali kiba
2.Belle9
3.Tid(sema hajitambui)
4.ndomo
 
Inashangaza sana Kiba yupo kimya 3 yrs af unamlinganisha na dai aliyetamba mda wote huo.... Hii inamaanisha Kiba ni homa ya Tanzania hakuna wa kumfikia.... Akina Ommy, Belle, Ben n.k wametoa nyimbo but bado mnamuwaza Kiba.......The Return of Kiba..

umeona eeh! mi nashndwa hata kuelewa mbona hapa kati kuna wasanii wengi sana wametoa single bado wanamkomalia kiba
 
Kuna wimbo mmoja unaitwa Daraja la sarenda,ndo kaimba nani kati ya hao?.Basi ndo kula yangu achukue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…