Mkuu izo ni nchi za wengine.... Nchini kwako sheria inakutaka utoe elfu 70,000tu kwa kila mwezi...Hivi unadhani hii ni kesi ya kisiasa au ya kibiashara?
Dunia mzima demu akikupandisha mahakamani kwa issue ya child support labda uwe mchovu ndio salama yako.
Kama Diamond anawashauri wazuri na anawasikiliza hizi ni issue za kumaliza nje ya mahakama.
Tena kwa nchi kama Marekani ndio usiombe child support unakatwa juu kwa juu kwenye source zako inaenda kwa mama.
Shabikieni mambo mengine lakini siyo Child support muulizeni Le Mutuz kakimbia nini Marekani.
Duh... Ila bora huyu jamaa angezaa na MTU wa nje, wabongo dahhhhHahaaa. Haswa pale mnapokosa pa kuingia kuteseka lazima jirani.
Hahaaaa. Wabongo siku zote huwa tunajua kuzitumia fursa jirani yaani mtu anasubiri uteleze au anakutelezesha makusudi ili yeye apatie hapo hapo.Duh... Ila bora huyu jamaa angezaa na MTU wa nje, wabongo dahhhh
Amezaa na Wangapi jameni huyu atakua wana magomvi na kuna lundo la wanawake wanashitaki watu msiongee hili saaana kwasababu tu Dimondo ni star...ila wapo wengi na kesi ziko nyingi sana..Sema huyo manzi Hamisa ana njaa kali sana, yaan yeye timing yake ni kuzaa na wenye pesa tu, hana shughuli maalum mjin
hataki hizo anataka milion 5 kwa mweziInamana hata zile laki mbili hapewi tena? Au anaona hazitoshi?
Hiyo kwa wewe masikini hela inategemeana na kipato chakoNakumbuka matunzo ya mtoto ilikuwa ni sh elfu hamsini(50,000) kwa mwezi.
Aangalie asije kuambulia elfu hamsini tu!
Ina maana wewe ulikuwa unajuwa Zari ni mke wa Diamond? Basi Watanzania mna poor IQ kama mnashangaa Diamond kutowa kauli hiyo.Kaniacha hoi alivyosema ' hajaoa daaahhh' Zari ajue yeye sio mke kumbe.
Matumizi kama hatoi na kipato anacho ni mahakamani tu hamna namna.
Hapa ni jukwaa la siasa. Kwa nini hapa haya mambo ya nyumbani na watoto?Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa mahakama ya watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.
Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mabetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
Wakili Zulu akizungumza na Gazeti la Mwananchi leo Alhamisi amesema mteja wao Hamisa Mobetto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.
“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.
Zulu amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.